Kwani Rais Samia si aliapa kulinda Katiba? Maandamano ni HAKI ya Kikatiba

deblabant

JF-Expert Member
Oct 7, 2022
901
1,334
Suala la maandamano ni la kikatiba na Rais Samia aliapa kulinda katiba tena akishika Quran kabisa. Iweje atake kuvunja kiapo chake tena kwa kulishirikisha jeshi waivunje pamoja. Hivi yeye isingekuwa kulinda katiba angekuwa raisi kweli?

Jeshi letu mbona liko tofauti na majeshi mengine duniani. Kwingine jeshi lisingekubali katiba kuvunjwa hata nukta. Jeshi ni wananchi siyo la serikali.

Jeshi lijitafakari na Rais Samia ajitafakari kama anastahili kuwa rais.
 
Maandamano yasiyo na tija wacha yadhibitiwe tu. Amewaruhusu wafanye mikutano ya kisiasa lakini kutuletea ujinga wa maandamano kama ya Kenya HATUTAKI.
 
Nani karuhusu kufanya mikutano. Ni Samia au katiba? Kwani maandamano yaliyoruhusiwa na katiba ni maandamano Gani! Umeshawahi kuona maandamano ya kuisifia serikali eti ndo yanaruhusiwa? Nchi Gani! Na mbona haijaandikwa kwenye katiba kwamba maandamano ya dini au ya kuisifu serikali ndo yanaruhusiwa tu ili tujue Hilo.
 
Swala la maandamano ni la kikatiba na Samia aliapa kulinda katiba tena akishika Quran kabisa. Iweje atake kuvunja kiapo chake tena kwa kulishirikisha jeshi waivunje pamoja...
Kwaiyo mnataka shughuli za kiuchumi zisimame kisa nyie mnataka kuandamana?
 
Naona siku hizi Mbowe kaacha kutumia chawa, sasa anatumia mende.

Mleta mada unaweza kuweka ushahidi kuwa ni wapi raisi Samia amevunja katiba kwa kukataa maandamano kufanyika ili na sisi tujiunge katika umende?
 
Kumbuka mkuu wa mkoa popote alipo anafanya kazi kwa niaba ya rais hawezi kufanya ya kwake
 
Nani karuhusu kufanya mikutano. Ni Samia au katiba? Kwani maandamano yaliyoruhusiwa na katiba ni maandamano Gani! Umeshawahi kuona maandamano ya kuisifia serikali eti ndo yanaruhusiwa? Nchi Gani! Na mbona haijaandikwa kwenye katiba kwamba maandamano ya dini au ya kuisifu serikali ndo yanaruhusiwa tu ili tujue Hilo.
Mbona Magufuli alipiga marufuku mikutano ya vyama vya siasa? Au umesahau haraka hivi?? Kama huwezi kutambua uungwana wa Samia kwenye hili wewe siyo mtu makini
 
Ndo mana mungu alitoa adhabu ya kifo instantly mana aliapa kwa kushika biblia na akavunja katiba hiyo hiyo aliyoapa kaayo. Mungu hapendi katiba ivunjwe. Hata Samia akicheza mungu atafanya yake.
 
😜
 
Attachments

  • IMG_20240113_003425.jpg
    IMG_20240113_003425.jpg
    31 KB · Views: 1
Ndo katiba iliruhusu hivyo unless bunge ingefuta hicho kipengele ili tusiwe na gats zote za kusema katiba inavunjwa.
Sema hakuna mtu wa kuandamana labda wachache wasiozidi 10 ambao ni wala keki ya taifa kupitia ruzuku za chama
 
Kwani una level Gani ya elimu mana nisiwe na hart na mtoto au zero brain
Acha ujinga.. hapa unazungumzia namna raisi alivyovunja katika, na namna maandamano yalivyozuiliwa, na mimi nahitaji fact namna hiyo katiba ilivyovunjwa, na namna hayo maandamano yalivyozuiliwa.

Swala la elimu utalianzishia uzi wake baadae.
 
Back
Top Bottom