Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 11,185
- 18,930
Kulikuwa na ubishi humu ndege za Dreamliner na Airbus ziliponunuliwa, kwamba hilo lilikuwa jambo la manufaa kwa wananchi wa Tanzania. Hilo nimelipinga siku zote, kwa sababu unaposema manufaa kwa Watanzania, Watanzania wepi wanaopanda hizo ndege? Na hata ukisema wengine wanafaidika indirectly, kuna siku ATCL imepata faida ili hata Watanzania wasiopanda ndege wafaidike na mapato yanayoingizwa na hizo ndege?
Siku zote nimefikiria kwamba tuna reli ambayo ndio inafaidisha watanzania wote - wale wanaopanda first class, second class na hata third class. Lakini huduma za reli nchini ziko taabani. Treni ya abiria kwenda Kigoma ni mara mbili kwa wiki - kwa kuwa hatuna mabehewa na vichwa vya kutosha.
Sasa hawa viongozi, huyu Magufuli, alihitaji degree ngapi kutambua kwamba ilikuwa afadhali kununua mabehewa hata 200 na vichwa vya treni vya kutosha ili kurudisha hali ya zamani kwamba treni zinafanya safari za mikoani kila siku? Kweli hilo lisingekuwa bora sana kuliko hizi ndege ambazo kila siku zinapaki bila kufanya kazi au zinakamatwa kwa sababu za mambo ya kilevi tu yanayofanywa na viongozi?
Kwa kuwa tulinunua hizi ndege kwa cash, mie ninapendekeza ziuzwe zote ili tukanunue mabehewa na vichwa vya treni vya kutosha kuanza safari za treni za kila siku na kuwanufaisha Watanzania wa aina zote na kuchangia mapato ya serikali. Hili sio suala la Chadema au CCM, ni suala ambalo viongozi wenye busara wataliona liko wazi kabisa.