Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,812
- 11,989
Serikali kupitia Shirika la Reli Tanzania ilifanya manunuzi ya vichwa vipya 17 na mabehewa mapya 59 ya abiria kwa ajili ya uendeshaji wa reli ya kiwango cha kimataifa SGR. Mpaka sasa Shirika limepokea vichwa vya treni ya umeme vinne (4) kati ya 17 kutoka kampuni ya Hyundai Rotem na mabehewa 56 kati ya 59 kutoka kampuni ya 'Sung Shin Rolling Stock Technology' (SSRST) ya nchini Korea Kusini.
Mabehewa matatu (3) yaliyosalia yanatarajiwa kuwasili nchini Februari, 2024. Vichwa 13 vilivyobaki vinatarajiwa kuwasili kwa awamu kama ifuatavyo, vichwa sita (6) vitawasili mwezi Machi na vichwa saba (7) vitawasili Aprili, 2024.
TRC itaanza kupokea Seti ya kwanza (1) kati ya Seti 10 za treni za Kisasa (EMU) mwezi Machi 2024 Mei seti 2, Juni seti 2, Julai seti 2, Septemba seti 2 na seti ya mwisho mwezi Oktoba 2024.
Vichwa vilivyopokelewa, kiutendaji vina mwendokasi wa kilomita 160 kwa saa. Mabehewa 27 katika madaraja ya Uchumi na Biashara. Daraja la biashara (Business class) ni mabehewa 13, kila behewa lina uwezo wa kubeba abiria 45 na mabehewa ya daraja la Uchumi (Economy class) ni 14, kila behewa lina uwezo wa kubeba abiria 78 kwa kuzingatia viwango vya kimataifa kumuwezesha abiria kusafiri kwa amani na salama.
Shirika la Reli Tanzania linaendelea kupokea kwa awamu vitendea kazi kwa ajili ya uendeshaji wa reli ya kiwango cha kimataifa (SGR). Zoezi la majaribio ya vitendea kazi linaendelea kwa mujibu wa mkataba ili kuhakikisha vinaendana na mifumo ya miundombinu iliyojengwa nchini kabla ya kuanza uendeshaji wa kibiashara.