Kadogosa: Safari za SGR kutoka Dar - Moro zimechelewa kwasababu ya hatuna Vichwa vya Treni

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa amesema ujenzi wa reli ya kisasa kipande cha Dar es salaam - Morogoro umekamilika kwa 100% na mabehewa zaidi ya 45 tayari yamewasili nchini lakini kilichosimamisha safari kuanza ni kuchelewa kwa vichwa vya treni ambapo hadi sasa kimefika kichwa kimoja huku vingine vikitarajiwa kuletwa siku za karibuni.

Akiongea leo Ikulu Dar es salaam wakati Viongozi mbalimbali wakitoa taarifa kwa Waandishi kuhusu ziara za Rais Dkt. Samia Morocco na Saudi Arabia, Kadogosa amesema;

“Ujenzi wa reli hususani Dar es salaam - Morogoro kwa sehemu kubwa tumekamilisha takribani 100%, kuna sehemu chache sana ambazo nafikiri hata nyinyi mtakuwa mnaziona pale Vingunguti, Nyerere na Banana kuna kumalizia, then kuna ujenzi wa kuingia Bandarini ambao hautuzuii sisi kuanza uendeshaji kwa maana ya Dar es salaam kwenda Morogoro.

“Kitu ambacho kimetusimamisha kwa muda ni kwasababu tulikuwa hatujapata vichwa hilo tu, sasa hii inaweza kuwa na maelezo mengi sana kwamba kwanini vichwa vimechelewa lakini tumekuwa na changamoto hiyo ya kutokupata vichwa vya treni, mabehewa yapo pale Pugu mengi zaidi ya 45 mapya yote lakini kichwa tulikuwa hatuna, kwa mara ya kwanza kichwa cha kwanza kimeingia hivi karibuni.

“Kwanza wanaoleta kichwa kwasababu ni kichwa kipya kabla hawajatupa lazima wakifanyie testing, wamekifanyia majaribio kwao kwenye reli yao na ujue reli sio zinafanana, ya kule tofauti na huku kwahiyo ni lazima afanye testing pia hapa kujihakikishia kile kichwa kinaenda KM 160 kwa saa na tutawaita Waandishi wa Habari mshuhudie hilo.”
 
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa amesema ujenzi wa reli ya kisasa kipande cha Dar es salaam - Morogoro umekamilika kwa 100% na mabehewa zaidi ya 45 tayari yamewasili nchini lakini kilichosimamisha safari kuanza ni kuchelewa kwa vichwa vya treni ambapo hadi sasa kimefika kichwa kimoja huku vingine vikitarajiwa kuletwa siku za karibuni.
Aseme wazi tu kwamba hawakuwa na nia ya dhati kuliharakisha hili jambo ili kuwalinda waarabu wanaomiliki mabasi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom