Je, ile 'confidence' ya Kuongea Kiingereza 'fluently' bila kuandikiwa au kusoma akina Nyerere na Mkapa waliitoa wapi nami nikajifunze?

2006 UNESCO iliitangaza Uganda kama nchi yenye grammar bora katika nchi za Afrika zinazoongea Kiingereza. Binafsi nilidhani Botswana wanaongoza lakini nilishtuka kusikia ni Uganda.
Napenda sana MTU akijenga hoja aweke reference, hii reference hata mi naikumbuka miaka kadhaa iliyopita nilipata kupitia BBC
 
Kuna stori zilizowahi kuvuma kuwa alipokuwa Chancellor wa UDSM wakati anatunuku digrii kwenye mahafali fulani kati ya mwaka 1986 na 1989, alipewa kadi imeandikwa "kwa mamlaka niliyopewa nawatunuku wale wote miliotajwa shahada ya B.Sc(Eng)." Mheshimiwa akaisoma vizuri tu kuwa "kwa mamlaka niliyopewa nawatunuku wale wote miliotajwa shahada ya Bachelor of Science in English"
Hahahaha ukiachana na UDSM ,tofauti na UDSM chuo nilichosoma mie majuzi kinatumia kiingereza hizo phrase huwa zimeandikwa kwenye kijitabu maalumu anasoma vizuri tu "By power ,virtue and moral authority held in ,,,, "
 
The lady it speak very tough English. Eye am told she educated Canada for PhD. Eye arm also told she pay many money of school fees for daughter educate outside of Tanzania.
Hahahahahaha jamani hebu acheni kunimalizia jokes zangu
 
Na huwezi Kusoma nchini Uganda iwe ni Primary School au Secondary School au University kisha ukawa Mpumbavu ( Popoma ) na usikijue vyema kabisa Kiingereza halafu pia usiwe 'Genius' katika Jamii.

Katika Elimu Uganda wametuacha mbali sana na Hongera kwa Elimu ya Uganda ambayo si tu naikubali ila naipenda kuliko hata ya Kenya na Tanzania.
Uganda sio ishu ya elimu kule wanatumia kuongea kiingereza hata mitaani.
Ingawa wako na lugha yao ya Luganda lakini wanaongea kiingereza pia mitaani kwa muda mwingi na wala haihusiani na elimu

Sent from my SM-C7000 using JamiiForums mobile app
 


sidhani unajua unachokisema wewe. Sikiliza matamshi ya kila neno analoongea, chaguzi ya maneno yake na ufasaha wa uwasilishaji halafu unasema kiingereza chake kilikuwa poor?
Nimemsikiliza nimeona anaongea standard english ambayo mtu yeyote msomi ambaye si kilaza anaweza kuiongea.
Sio ya kuisifia kwamba anajua sana.

Sent from my SM-C7000 using JamiiForums mobile app
 
Mie pia nataman sana kua fluent kwenye kingereza. Bado napambana and I can see some improvements. Cha msingi wewe endelea kujifunza huku uki practise na kujichanganya na wanaoongea kingereza kdogo kdogo utajikuta upo vizuri.All the best
Ukishakijua halafu unataka ukakitumie wapi na kwa manufaa gani?

Sent from my SM-C7000 using JamiiForums mobile app
 
Angalizo lako halina ukweli wowote, katika uwanja wa kimataifa unaheshimika zaidi ukikumbatia lugha yako. Mataifa mengi yenye heshima zake kama ufaransa, china, urusi n.k. Watu wanazungumza lugha zao na mitaala yao yote wameweka kwenye lugha zao.

Yapo pia mataifa madogo kama uholanzi, norway n.k. Mataifa yao wanasomesha watoto wao lugha ya kiengereza, ni maamuzi ya mtu kuamua kurahisisha kutumia kiengereza. Lakini hii haina uhusiano wowote na heshima, ni maamuzi ya mtu na confidence yake.
Kwa kifupi mimi naona ni utumwa tu kutumia miguvu mingi kujifunza lugha ya nchi za wazungu bila manufaa maalumu

Sent from my SM-C7000 using JamiiForums mobile app
 
Sikiliza mzee: lafudhi ya kiingereza siyo monolithic. Kwa marekani lafudhi ya kiingereza kinachoongewa New York ni tofauti kabisa na ile inayoongewa Texas na pia ni tofauti kabisa na ile inayoongewa Minnesota au Washington. Vile vile kwa Uingereza kwenyewe, lafudhi ya kiingereza cha England, ni tofauti kabisa na ile ya Scotland au ya Ireland. Ukiwa katika level ya dunia, pia utagundua kuwa lafudhi ya kiingereza cha Marekani ni tofauti kabisa na ile ya Australia, au ya New Zealand au ya UK. Sasa wewe katika variations hizo za lafudhi ya kiingereza ni ipi unathamini kiasi cha kudai kuwa lafudhi za waongeaji wengine siyo za kiingereza.

ndiyo maana nikaamini kuwa huenda wewe hujui kiingereza. Hata Tanzania kwenyewe, kiswahili cha Mmasai ni tofauti na kiswahili cha mchaga au cha mhaya au cha mndengereko. Je wewe unadhani kati ya makabila hayo kuna wanajua kiswahili zaidi ya wengine?
Mkuu kiingereza ni lugha ya asili ya uingereza.
Sasa je uingereza ni wapi?
Na kitu kingine kiswahili asili yake ni pwani ya afrika mashariki.
Kwa hiyo ukiuliza wenye kiswahili ni wandengereko jibu lake kama wandengereko ni watu wa pwani ni kweli kiswahili ni chao wala hujakosea.
Wengine ambao wako nje ya pwani tunaassume wanajifunza kiswahili ila hawawezi kuwafikia wale wenyewe wa pwani.

Sent from my SM-C7000 using JamiiForums mobile app
 
Mimi nilidhani kwa neno hilo ungeacha kuandika kumbe wajifanya mjuaji!!

Ulitaka nikuonyeshe kosa lako la kiswahili na nikakuonyesha lakini ukajifanya hamnazo kutokuliona, sasa angalia kosa lako uliloandika, nanukuu; "
Kudadeki JF sihami.
Naona umemuonjesha kidogo ladha ya kiingereza.
 
Walisoma Arts mpaka chuo kikuu na walikazania kiingereza na kukimudu. Angalia Tundu lissu anavyoongea kwa kujiamini, alichukua Arts na akaweka mkazo katika kiingereza ili kimsaidie katika fani yake. Ukiwa na nia ya dhati utakimudu kiingereza.
 
Mkuu kiingereza ni lugha ya asili ya uingereza.
Sasa je uingereza ni wapi?
Na kitu kingine kiswahili asili yake ni pwani ya afrika mashariki.
Kwa hiyo ukiuliza wenye kiswahili ni wandengereko jibu lake kama wandengereko ni watu wa pwani ni kweli kiswahili ni chao wala hujakosea.
Wengine ambao wako nje ya pwani tunaassume wanajifunza kiswahili ila hawawezi kuwafikia wale wenyewe wa pwani.

Sent from my SM-C7000 using JamiiForums mobile app
Kwa hali hiyo watu wote duniani hajaui kiingereza kwa vile hawana lafudhi ya England? Huwezi kumpata mtu ambaye hakukulia England akajua kuongea kwa lafudhi ya England. Hata Tanzania hapa, watu waliokulia mikoa mbalimbali wana lafudhi zao anbazo hazifanani.Kanuni kuu ya lugha ni isimu; nimeshawasikia wandegereko wanaosema "nyimbo ile nimeipenda sana" ambayo ni makosa katika lugha ya kiswahili.
 
Kiingereza cha Nyerere kilikuwa poor, Kiingereza kilikuwa na Augustino Mahiga.
Poor based on what, alikuwa anaongea Kiingereza fasaha with confidence.
Umenifanya nimeingia You Tube kumsikiliza huyo Mahiga, Kiingereza chake ni cha kawaida sana na ana accent vile vile. Acha ushabiki wa kijinga.
 
Back
Top Bottom