Je, ile 'confidence' ya Kuongea Kiingereza 'fluently' bila kuandikiwa au kusoma akina Nyerere na Mkapa waliitoa wapi nami nikajifunze?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,551
108,888
Natamani sana nami GENTAMYCINE nijue Kuongea Kiingereza kizuri kama cha akina Nyerere na Mkapa na siyo nije nikijue vizuri baada ya Kustaafu Majukumu yangu au niwe nakiongea kwa kutegemea Kuandikiwa kisha kila nikiwa nahutubia niwe 'nazuga' kwa Kukiongea kwa Sekunde Tano, nakunywa Maji na nakohoa ili kuwaonyesha wanaonisikiliza kuwa nakijua kisha narejea tena Kusoma huku nikiwa natetemeka na kila mara.

ANGALIZO
Kujua Kiingereza si lazima kwani Kiswahili, Kizanaki na Kinyarwanda kinatosha na wala kujua Kiingereza si kipimo cha ama Mtu kuwa Msomi (Intellectual) au Mwerevu (Brainiac) katika Jamii ila katka Uga wa Kimataifa na kwa Heshima ya Lugha ya Kiingereza tokea enzi na enzi kutokujua Kiingereza (Kiswahili cha duniani kama alivyowahi kusema Mwalimu Nyerere) wakati hata 'Mitaala' yetu ya Elimu ni ya Kiingereza kunaweza Kutafsiriwa ni Uwendawazimu na Unafiki usiovumilika.
 
Lugha yoyote ukiipenda....ukijitoa kuipenda kwa kutaka uijue vyema kwa ARI KUBWA NA KUJIFUNZA basi utaifahamu vyema tu....

Kuna watu wana ufaswaha mwepesi wa kutamka maneno ya lugha ya kigeni kuliko wengine....inaonekana "brain centers" zao za lugha ziko "strong" kuliko wengine, hawa hawatumii nguvu kubwa iliyopitiliza kuliko makundi mengine.

Kwa makundi mengine wasio wao huhitajika kujitoa mno....mno haswa ikiwa hiyo lugha ya kigeni anajifunza mtu akiwa ukubwani.

Ninaamini mbali na JUHUDI KUBWA aliyokuwa nayo mathalani hayati Ben.Mkapa ila pia "language center yake upstairs" ilikuwa iko vyema sana.

Hayati Mkapa alikuwa anapenda sana kusoma lugha ya KIINGEREZA kupitia vitabu vya tamthilia za kiingereza,michezo,riwaya na hadithi.Alipenda makala tofauti kupitia lugha hiyo....yuko mzee mmoja alipata kuhadithia kuwa huko Makerere hayati Mkapa alikuwa moto mno.....sawa na jamaa wa Kijaluo kutoka nchini Kenya WALIOKUWA huko chuoni.

Kiufupi hayati Mkapa alikuwa CHARISMATIC aliyependa sana "kumaintain classy" driving force aliyokuwa nayo ilitoka moyoni (passion).

Kuhusu hayati baba wa taifa JKN "ugenius wake" charisma yake ya kiuongozi ,kupenda sana kusoma ,kupata elimu MAKERERE na EDINBURGH kulimsaidia sana....alijiandaa kujua mengi ili kuwakabili wazungu kwa HOJA ZA MOTO.

#KaziIendelee
 
Lugha yeyote ukiipenda....ukijitoa kuipenda kwa kutaka uijue vyema kwa ARI KUBWA NA KUJIFUNZA basi utaifahamu vyema tu....

Kuna watu wana ufaswaha mwepesi wa kutamka maneno ya lugha ya kigeni kuliko wengine inaonekana "brain centers" zao za lugha ziko "strong" kuliko wengine...hawa hawatumii nguvu kubwa iliyopitiliza kuliko makundi mengine...
Umedadavua / Kuchambua vyema mno.
 
Back
Top Bottom