Je, huu ni ukweli uliofichwa kwa miaka mingi?

Je, huu ni ukweli uliofichwa kwa miaka mingi?

Aisee naona nikuache tu maana huna hoja.so wewe huoni jinsi binadam tulivyoumbwa na mengi mazuri,tunaweza kucheka,kusema,kutembea kutambua mema na mabaya wewe umeona tu mapungufu kwanini "tunaenda choo"?

Nathubutu kusema wewe ni hasara ya dunia hamna namna,nikusema ulitaka tuumbwe kama robots eti?mkuu hivi unatumia kichwa kweli kufikiri!?
Kama watu tungekuwa tumeumbwa na Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, tusingeumwa na kufa.

Badalayake, tunaumwa magonjwa mengina kufa.

Ushahidikwamba hatujaumbwa na Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote.

Tena vitoto vingine vinaumwa na kufariki kabla ya kutimiza siku tano.

Mungu gani huyoanaruhusu vitoto vife hivyo?
 
Ndio hivyo Mkuu biblia kuna mengi inakataza tu ila kuna jamii zinayafanya na bado wanafika mbinguni maana kuna sheria zingine walipewa watu wa eneo husika na si applicable kwa maeneo yote..... Mfano kufunika nywele,kunyoa,wanawake kukaa kimya kanisani,wachungaji wanaume tu n.k shida ya sisi waafrika tumechukua kama yalivyo badala ya kuangalia reference na relevance ya hadhira iliyolengwa na ndio maana tunapotezana kila cku.

Sasa mkuu nikuulize..... Biblia inaruhusu utumwa yaani sex slaves na wajakazi kuuzwa na kununuliwa je nikifanya sex slavery ntakuwa na dhambi au lah?? Embu nisaidie hapo kwanza ndio utaelewa nachotaka kusema.
Kuhusu slaves, mkuu nilivyosoma biblia ina nyakati zake yaani kuna vipindi vya sheria na maongozi kulingana na wakati. Mfano kulikuwa na nyakati zisizo pungua kama saba hivi na ktk kila nyakati kulikuwa na maongozi yake. Naamini suala la utumwa lilikuwa ktk nyakati fulani na likapita. Ni sawa na suala la kuuwa mtu kafiri mpinga Mungu au wale machotara kipindi cha nabii fulani walikamatwa wakauliwa kisa tu walichanganya damu ya ki Israel na mataifa mageni. Ktk kipindi cha agano jipya hii haipo ndo maana huwezi kuta mkristo anaua kafiri au chotara na akawa na utetezi wa kibiblia. Nyakati zina sheria zake the same kuhusu utumwa uwe wa kutokuweza kulipa madeni, njaa nk
 
Nimekwambia utoe uthibitisho ulio logically consistent.

Unaweza ukawa si wa maelezo, ukawa ni wa hesabu za Roger Penrose vile vile.

Sijakupangia namna, mradi unaweza kuwa logically consistent na haupoself contradicting.

Hujathibitisha.
Ndiyo maana nikakwambia isije ikawa unaimba tu uthibitisho,ni wazi hujui ni namna gani huyo Mungu anaweza kuthibitishwa.
 
Ndiyo mkuu mtu anayeenda mbinguni unamuona hta kabla hajafa na kuna mmoja mpaka wine alikuwa anakunywa kabisa na mikutano yake Roho mtakatifu anashuka mkuu nikagundua haya mambo ya imani sio kukariri vifungu vya biblia bali nikwenda mbele kabisa.... Hata wachungaji wanawake huku bongo hawataki kisa tu bible ilikataza but huko nje wazungu wameweka na wanasogeza gombo si kidogo kina joyce meyer n.k sasa unajiuliza kivp wao waliowaza nje ya bible wanatuzidi kiroho sio tuliokariri bible!!!

Na hiyo amri inayosema mwanamke asivae mavazi ya kiume unaweza tuelezea wapi biblia inasema mavazi ya kiume ni yapi na ya kike ni yapi?? Je yale madira waliokuwa wakivaa kina Yesu ni mavazi ya kike au kiume??
Yesu au vazi la kiume ni kanzu, Over. Suti ni ushetani tu.
 
Kwa nini unafikiri wewe ndiye una uwezo na ujuzi wa kunishauri mimi na si vinginevyo?
hakuna aliyekuvuta shati wala kukulazimisha kuukataa au kuupokea ushauri wangu. na wala hakuna aliyekukataza au kukuzuia wewe kunishauri mimi .......

hizo ni hisia ulizoamua kujijengea mwenyewe na kisha kuzifanya ni hali halisi pole sana......
Kwa nini unafikiri mimi nasoma kwa kunyofoa nyofoa?
Kwa nini unafikiri mimi sijui kwamba Adam na Eva walikuwa na watoto zaidi?
ni kwasababu ya aina ya maswali uliyouliza.
Mimi nimesoma si tu Biblia, nimesoma vitabu vya jinsi ya kusoma Biblia, cha mwisho kukisoma ni cha James L. Kugel, a Harvard Professor of Hebrew and Hebrew Bible specialist "How To Read The Bible: A Guide to Scripture, Then and Now" wewe umesoma nini? Utaweza kunifundisha kusoma Biblia kuliko Professor Kugel?
kutokujua unasoma nini na kwanini ni tatizo kubwa zaidi ya kutokusoma......

Hivi unajua kusoma
ndio
Umesoma nilichoandika?
umesoma nilichokujibu ??
Ulichonukuu umekisoma kwa kituo?
nilichokujibu umekisoma kwa kituo ??
ungekisoma kwa kituo usingeuliza maswali haya ambayo nishayajadili katika ulichonukuu
hakuna mahala nimekuuliza swali lolote na wala sina mpango wa kukuuliza swali lolote kwa sababu najua uwezo wa kunijibu unachoulizwa HUNA
 
Jibu ni hilo la pili Tunda sio ngono, tuelewane na aliyemwendea Hawa ni Lilith sio Shetani og
 
hakuna aliyekuvuta shati wala kukulazimisha kuukataa au kuupokea ushauri wangu. na wala hakuna aliyekukataza au kukuzuia wewe kunishauri mimi .......

hizo ni hisia ulizoamua kujijengea mwenyewe na kisha kuzifanya ni hali halisi pole sana......


ni kwasababu ya aina ya maswali uliyouliza.

kutokujua unasoma nini na kwanini ni tatizo kubwa zaidi ya kutokusoma......


ndio

umesoma nilichokujibu ??

nilichokujibu umekisoma kwa kituo ??

hakuna mahala nimekuuliza swali lolote na wala sina mpango wa kukuuliza swali lolote kwa sababu najua uwezo wa kunijibu unachoulizwa HUNA
Hujajibu swalila mwanzo kabisa.

Kwa nini unafikiri wewe ndiye una uwezo na ujuzi wa kunishauri mimi na si vinginevyo?
 
Hakuna Mwenye ujuzi zaidi ya Mungu na lusifer mwaasi alieasi huko mbinguni yakamkuta ya kumkuta sasa hasira zote tumehamishiwa binadamu
 
Mwanzo 4:16:Kisha Kaini akaondoka mbele ya Mwenyezi-Mungu, akawa anaishi katika nchi ya Nodi, upande wa mashariki wa Edeni. 17 Kaini akamjua mkewe, naye akapata mimba, akamzaa Henoki.
Hapa tunaoneshwa kulikuwa na mji mbele ya Edeni.Ukifikiri kwa haraka haraka kama mimi ni kuwa mpaka muda ule Kaini anamuua nduguye kulikuwa na watu wanne tu duniani.Yaani Hawa,Adam,Kaini na Abel..baada ya kifo cha Abel walibaki watu watatu tu.Na ikumbukwe ukisoma kimtililiko Kaini alifukuzwa mbele ya Uso wa Bwana na kwa wazazi pia.
Matatizo mengi hukwepwa hapa,Mke wa Kaini alitokea wapi?Na alizaliwa na nani?Ndio maana ukirejea nyuma kuna wenzangu waliotangulia ukisoma Mwanzo Sura ya 1:20-31 na Sura ya 2:1-25..je biblia inajieleza kinyume nyume.Utaona Siku ya Sita nini kilifanyika.Na baadae utaona siku ya saba Mungu alipumzika,lakini hapa Sura ya pili inaeleza tena nini Mungu alifanya.
Kuna shida nyingi sana katika Uandaaji wa hivi vitabu,kama mnakumbuka kuna Biblia flani unapooenda nunua unaambiwa hii si nzuri sana.Versions za biblia,tukipata muda wajuvi watuelezee.
Mleta mada umeleta kitu ambacho ni fikirishi kama utakuwa unapenda kusoma na ku judge kwa akili za vitabu na ufahamu wa kawaida tu.Shida ni moja tayari tumekua kwenye mazingira amabyo hayaruhusu ku judge kabisa.Ndio maana hata wenzetu mpaka sasa wanatuachia maswali kwa nini Moshi huenda kwa Pope Mweupe tu?Je Mungu haoni uwepo wa Mtu Mweusi?Kwanini tuende Macca Madina tu Kwamba kule ndio kuna Uwepo kushinda pahala pengine?Ina maana Mungu wa wote anafanya Selection kwa Makundi flani tu sasa kuna haja gani ya sisi kumlilia kila siku ikiwa tayari kuna watu ni chosen?
Kuna mtu mmoja tuliwahi bishana sana,nakumbuka ilikuwa miaka kama 8 nyuma,Tarehe 31 kuingia mwaka mpya,aliniambia niape na kama nitavuka basi.Niliapa na Mpaka sasa nipo naandika uzi.Haya haya mambo.Tumepewa maarifa,saa nyingine si mbaya tuvuke kuona je hili ni sawa au ni kwa sababu tu?Binafsi nimesoma hicho kitabu kama taaluma.Kwa madhehebu ya Ukristo ...ukisoma una stress zako za maisha.Kamwe hutoelewa hii dunia ilivyo.Ukisoma una maumivu yako ya kuachwa,huna pesa,umeibiwa basi utaona jinsi kilivyo.
Ilimu iliyopo mfano kwa Upande wa Kitabu takatifu Quran ni pana sanaa...sasa shida si kitabu shida ni watumiaji na wanaotafsiri.Hapo ndipo fujo ya dunia inapoanzia.
Adamu alizaa watoto 40 kila uzao jike na dune, sasa Walipokuwa wajubwa Cain hakuwa mwelewa, hadi abili alipokuwa na kutaka kuoa, Abili/Abel akamwambia Cain muoe dadangu na Mi nimuoe wako, Cain akakataa kwa sababu dadake/pacha wa Cain alikuwa mzuri wa sura na umbo kuliko Abili sasa Cain akasema oa dadako na Mi nioe dadangu, Abel akamwelewesha Cain akakataa, wakapeleka kesi kwa babao, baba akasema Abel uko sahihi, Cain akahisi kaonewa, Adam akasema tumuombe Mungu atujibu nani yupo sahihi wakafanya sala wakatoa na sadaka kwa makubaliano, itakayochukuliwa ndiye yuko sahihi, sadaka ya Abel ikapokelewa ya Cain ikabaki ndipo Cain akachukia akapata hasira kisha shetani akapata nafasi ya kumjaza ukatili Cain mbinu na namna ya kumuua ndugu yake, hakuna aliyetoa sadaka nzuri kuliko mwenzake hii ni swaga ya walioleta biblia lengo lao limekaa kimaslahi, kwahyo Hapo ndipo Cain alipofukuzwa na akaondoka na dadake wakaenda kufanya yao na kuanza kuzaana, tuelewane kabisa Shetani hana uwezo wa kuzaa na binadamu hii ni kwa jinsi ya uumbwaji kati yetu na yeye,.. Maswali mengine nitajibu kesho
 
Hujajibu swalila mwanzo kabisa.

Kwa nini unafikiri wewe ndiye una uwezo na ujuzi wa kunishauri mimi na si vinginevyo?
ondoa ilo neno nililolibold kisha uulize tena hapo swali lako ndo litakuwa linamaa (kwa sababu hakuna aliyekuzuia wewe kunishauri mimi)
 
ondoa ilo neno nililolibold kisha uulize tena hapo swali lako ndo litakuwa linamaa (kwa sababu hakuna aliyekuzuia wewe kunishauri mimi)
Hapana, unapojitia ujuaji kuanza kumshauri mtu, bila hata kuanza kuuliza kwanza, maana yake wewe umejivika uwezo wa kumshauri huyo mtu.

Umejuaje mimi nahitaji ushauri wako?

Umejuaje wewe una uwezo wa kunishauri mimi?

Umejuaje kwamba wewe siye unayepaswa kushauriwa na mimi ila wewe ndiye unaweza kunishauri mimi?
 
Adamu alizaa watoto 40 kila uzao jike na dune, sasa Walipokuwa wajubwa Cain hakuwa mwelewa, hadi abili alipokuwa na kutaka kuoa, Abili/Abel akamwambia Cain muoe dadangu na Mi nimuoe wako, Cain akakataa kwa sababu dadake/pacha wa Cain alikuwa mzuri wa sura na umbo kuliko Abili sasa Cain akasema oa dadako na Mi nioe dadangu, Abel akamwelewesha Cain akakataa, wakapeleka kesi kwa babao, baba akasema Abel uko sahihi, Cain akahisi kaonewa, Adam akasema tumuombe Mungu atujibu nani yupo sahihi wakafanya sala wakatoa na sadaka kwa makubaliano, itakayochukuliwa ndiye yuko sahihi, sadaka ya Abel ikapokelewa ya Cain ikabaki ndipo Cain akachukia akapata hasira kisha shetani akapata nafasi ya kumjaza ukatili Cain mbinu na namna ya kumuua ndugu yake, hakuna aliyetoa sadaka nzuri kuliko mwenzake hii ni swaga ya walioleta biblia lengo lao limekaa kimaslahi, kwahyo Hapo ndipo Cain alipofukuzwa na akaondoka na dadake wakaenda kufanya yao na kuanza kuzaana, tuelewane kabisa Shetani hana uwezo wa kuzaa na binadamu hii ni kwa jinsi ya uumbwaji kati yetu na yeye,.. Maswali mengine nitajibu kesho
Unaweza kutoa source ya haya maelezo yako kama hutojali
 
Habari za jioni wana JF mada ya leo ni sensitive kidogo hivyo ningependa tuisome kwa umakini,tujifikirishe na tujadiliane kwa mapana bila kashfa za kidini,kejeli,matusi,hasira n.k maana mada hii ni kwa ajili ya kujifunza na kubadilishana mawazo,maarifa,elimu n.k sio uwanja wa vita
View attachment 828516
Mada ya leo ni kuhusu ukweli wa mzazi halisi wa Cain ama tuseme kizazi cha nyoka na kizazi cha Adam. Ikumbukwe nyoka anyeongelewa hapa sio nyoka huyu wa sasa anayetambaa naongelea yule wa kabla ya tunda kuliwa.

Reference yangu itakuwa vitabu vya dini kadhaa kuanzia uyahudini,biblia,apocrypha,pseudipigraphi, maandishi ya wanatheolojia na vitabu vya kihistoria.

UTANGULIZI
Kupitia nadharia hii, yote yanaanzia kwenye bustani ya Eden ambapo tunaona shetani kupitia nyoka akimshawishi Hawa "kula tunda" na katika tunda hilo inaaminika linahusianisha ngono ambapo nyoka alimlala Hawa na kumpachika mimba ambayo baadae alikuja kuzaliwa Mtoto wa uzao huo yaani kizazi cha nyoka yaani Cain ili shetani aweze kuharibu uumbaji wa Mungu.

KWANINI NADHARIA HII?
Ili tuamini Nyoka alilala na mwanamke tunaweza tumia vigezo vifuatavyo

1. Adhabu kubwa ya Mungu kwa mwanamke ilikuwa ni kwenye sekta ya ngono sababu ndipo alipoanguka ndio maana Mungu akamhukumu sababu ya tendo la ndoa na mimba aliyobeba pia.

Mwanzo 3:
16 Akamwambia mwanamke, Hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako; kwa utungu utazaa watoto; na tamaa yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala

Pia shetani tukisoma kwenye kitabu cha biblia (madhehebu kadhaa hukitumia) cha Apocalypse of moses 26:1-4 tunaona hukumu ya Mungu kwa shetani kuwa atamtoa masikio,mabawa na UUME!!!!

Hivyo nadharia hii kuwa ngono ilihusika inapatiwa nguvu kupitia mistari hii

NANI BABA WA CAIN?
Biblia ya kiswahili inasema

Mwanzo 4:1
1 Adamu akamjua Hawa mkewe; naye akapata mimba, akamzaa Kaini, akasema, Nimepata mtoto mwanamume kwa BWANA

Lakini tafsiri iliyofanyiwa uhakiki kupitia New jerusalem Translation inasema hivi kwa kiswahili

...... Nimepata mtoto kutoka kwa malaika wa Bwana

Hivyo kama tafsiri hii ya NJT ina maanisha Adam alikiri kuwa mtoto sio wake ila wa MALAIKA ambaye kwa muktadha huu ni lucifer.

Kwenye biblia ya kiebrania neno lililotumika kwa KUMJUA ni Yada na Eth ambapo Yada baada ya kufanyiwa utafiti mpya limeonekana haimaanishi tu ni kumlala mwanamke bali inamaanisha KUTAMBUA KITU na Eth ina maanisha ALAMA FULANI(mabadiliko) hivyo tukiuandika mstari huu upya kutumia tafsiri ya maneno haya itakuwa hivi;

Adamu akatambua alama/ishara ya mabadiliko juu ya Hawa mkewe; naye akapata mimba, akamzaa Kaini, akasema, Nimepata mtoto mwanamume kutoka kwa malaika wa BWANA

Kwahiyo mpaka hapa tumeshapata maana tofauti kabisa ya mstari huu si ndio wakuu??

JE KWANINI NASEMA CAIN SIO MWANA WA ADAM
1. Biblia huko mbele inamtaja Cain kama alitokana na ''yule mwovu'' yaani shetani

1 Yohana 3:12
12 si kama Kaini alivyokuwa wa yule mwovu, akamwua ndugu yake. Naye alimwua kwa sababu gani? Kwa sababu matendo yake yalikuwa mabaya, na ya ndugu yake yalikuwa ya haki.
View attachment 828519


2. Biblia inamtambua seth kama mtoto pekee wa Adam maana inadai Henoko alikuwa mtu wa 7 baada ya Adam na ukihesabu utagundua imetaja uzao wa seth peke yake na imemuacha Cain peke yake hivyo ikimaanisha Cain hakutambuliwa kma mwana wa Adam

Yuda 1:14
14 Na Henoko, mtu wa saba baada ya Adamu, alitoa maneno ya unabii juu ya hao
View attachment 828520


3. Tunaona hata seth ndio biblia inaonyesha alizaliwa kwa mfano wa sura na mfano wa adam

Mwanzo 5
3 Adamu akaishi miaka mia na thelathini, akazaa mwana kwa sura yake, kwa mfano wake, akamwita jina lake Sethi

Hii yote ikimaanisha Cain hakuwa uzao wa Adam ndio maana hakufanana naye Adam kwa lolote hivyo muandishi hakuona sababu ya kujumuisha jambo hilo alipozaliwa cain.

4. vitabu vinavyotambuliwa na dini ya kiyahudi kama Zohar Pekudei 21:5 kinakubali hoja hii.

Baada ya adam na mke wake kufanya dhambi, na shetani kumjua Hawa na kumnajisi, Hawa alimzaa Cain. Alikuwa na umbo la duniani na kuzimu. Hivyo,alikuwa wa kwanza kuleta kifo duniani,iliyosababishwa na upande wake wa kuzimu,sababu alitokana na uchafu wa najisi ya nyoka (kwa hawa). Asili ya nyoka(shetani) ni udanganyifu,mauaji,na Cain,alijifunza nyendo zake. (Utafsiri binafsi)

HITIMISHO
Kupitia hayo maandiko machache nlioweza kupata ninaweza kufikia hitimisho kuwa kuna uwezekano tumefichwa kwa muda mrefu kuhusu uhalisia wa kilichotokea Eden nikaona nilete nadharia hii JF ili tuweze kufikiri pamoja na kupata ukweli wa jambo hili.

NB: Naomba Moderator msiunganishe nyuzi hii na zingine juu ya bustani ya edeni maana hii imejikita zaidi kwa Cain na sio maisha ya bustanini

Naomba kuwasilisha
Chakula cha kiroho..... Unlocking the untold secrets.... Mada yako hii imejibu maswali mengi sana niliyokuwa nauliza kupitia mada zangu... Umelitendea haki jukwaa na alfajiri yangu imekuwa njema... [emoji120] [emoji120] [emoji120] [emoji120]
 
Back
Top Bottom