zitto junior
JF-Expert Member
- Oct 7, 2013
- 18,914
- 28,524
Habari za jioni wana JF mada ya leo ni sensitive kidogo hivyo ningependa tuisome kwa umakini,tujifikirishe na tujadiliane kwa mapana bila kashfa za kidini,kejeli,matusi,hasira n.k maana mada hii ni kwa ajili ya kujifunza na kubadilishana mawazo,maarifa,elimu n.k sio uwanja wa vita
Mada ya leo ni kuhusu ukweli wa mzazi halisi wa Cain ama tuseme kizazi cha nyoka na kizazi cha Adam. Ikumbukwe nyoka anyeongelewa hapa sio nyoka huyu wa sasa anayetambaa naongelea yule wa kabla ya tunda kuliwa.
Reference yangu itakuwa vitabu vya dini kadhaa kuanzia uyahudini,biblia,apocrypha,pseudipigraphi, maandishi ya wanatheolojia na vitabu vya kihistoria.
UTANGULIZI
Kupitia nadharia hii, yote yanaanzia kwenye bustani ya Eden ambapo tunaona shetani kupitia nyoka akimshawishi Hawa "kula tunda" na katika tunda hilo inaaminika linahusianisha ngono ambapo nyoka alimlala Hawa na kumpachika mimba ambayo baadae alikuja kuzaliwa Mtoto wa uzao huo yaani kizazi cha nyoka yaani Cain ili shetani aweze kuharibu uumbaji wa Mungu.
KWANINI NADHARIA HII?
Ili tuamini Nyoka alilala na mwanamke tunaweza tumia vigezo vifuatavyo
1. Adhabu kubwa ya Mungu kwa mwanamke ilikuwa ni kwenye sekta ya ngono sababu ndipo alipoanguka ndio maana Mungu akamhukumu sababu ya tendo la ndoa na mimba aliyobeba pia.
Mwanzo 3:
16 Akamwambia mwanamke, Hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako; kwa utungu utazaa watoto; na tamaa yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala
Pia shetani tukisoma kwenye kitabu cha biblia (madhehebu kadhaa hukitumia) cha Apocalypse of moses 26:1-4 tunaona hukumu ya Mungu kwa shetani kuwa atamtoa masikio,mabawa na UUME!!!!
Hivyo nadharia hii kuwa ngono ilihusika inapatiwa nguvu kupitia mistari hii
NANI BABA WA CAIN?
Biblia ya kiswahili inasema
Mwanzo 4:1
1 Adamu akamjua Hawa mkewe; naye akapata mimba, akamzaa Kaini, akasema, Nimepata mtoto mwanamume kwa BWANA
Lakini tafsiri iliyofanyiwa uhakiki kupitia New jerusalem Translation inasema hivi kwa kiswahili
...... Nimepata mtoto kutoka kwa malaika wa Bwana
Hivyo kama tafsiri hii ya NJT ina maanisha Adam alikiri kuwa mtoto sio wake ila wa MALAIKA ambaye kwa muktadha huu ni lucifer.
Kwenye biblia ya kiebrania neno lililotumika kwa KUMJUA ni Yada na Eth ambapo Yada baada ya kufanyiwa utafiti mpya limeonekana haimaanishi tu ni kumlala mwanamke bali inamaanisha KUTAMBUA KITU na Eth ina maanisha ALAMA FULANI(mabadiliko) hivyo tukiuandika mstari huu upya kutumia tafsiri ya maneno haya itakuwa hivi;
Adamu akatambua alama/ishara ya mabadiliko juu ya Hawa mkewe; naye akapata mimba, akamzaa Kaini, akasema, Nimepata mtoto mwanamume kutoka kwa malaika wa BWANA
Kwahiyo mpaka hapa tumeshapata maana tofauti kabisa ya mstari huu si ndio wakuu??
JE KWANINI NASEMA CAIN SIO MWANA WA ADAM
1. Biblia huko mbele inamtaja Cain kama alitokana na ''yule mwovu'' yaani shetani
1 Yohana 3:12
12 si kama Kaini alivyokuwa wa yule mwovu, akamwua ndugu yake. Naye alimwua kwa sababu gani? Kwa sababu matendo yake yalikuwa mabaya, na ya ndugu yake yalikuwa ya haki.
2. Biblia inamtambua seth kama mtoto pekee wa Adam maana inadai Henoko alikuwa mtu wa 7 baada ya Adam na ukihesabu utagundua imetaja uzao wa seth peke yake na imemuacha Cain peke yake hivyo ikimaanisha Cain hakutambuliwa kma mwana wa Adam
Yuda 1:14
14 Na Henoko, mtu wa saba baada ya Adamu, alitoa maneno ya unabii juu ya hao
3. Tunaona hata seth ndio biblia inaonyesha alizaliwa kwa mfano wa sura na mfano wa adam
Mwanzo 5
3 Adamu akaishi miaka mia na thelathini, akazaa mwana kwa sura yake, kwa mfano wake, akamwita jina lake Sethi
Hii yote ikimaanisha Cain hakuwa uzao wa Adam ndio maana hakufanana naye Adam kwa lolote hivyo muandishi hakuona sababu ya kujumuisha jambo hilo alipozaliwa cain.
4. vitabu vinavyotambuliwa na dini ya kiyahudi kama Zohar Pekudei 21:5 kinakubali hoja hii.
Baada ya adam na mke wake kufanya dhambi, na shetani kumjua Hawa na kumnajisi, Hawa alimzaa Cain. Alikuwa na umbo la duniani na kuzimu. Hivyo,alikuwa wa kwanza kuleta kifo duniani,iliyosababishwa na upande wake wa kuzimu,sababu alitokana na uchafu wa najisi ya nyoka (kwa hawa). Asili ya nyoka(shetani) ni udanganyifu,mauaji,na Cain,alijifunza nyendo zake. (Utafsiri binafsi)
HITIMISHO
Kupitia hayo maandiko machache nlioweza kupata ninaweza kufikia hitimisho kuwa kuna uwezekano tumefichwa kwa muda mrefu kuhusu uhalisia wa kilichotokea Eden nikaona nilete nadharia hii JF ili tuweze kufikiri pamoja na kupata ukweli wa jambo hili.
NB: Naomba Moderator msiunganishe nyuzi hii na zingine juu ya bustani ya edeni maana hii imejikita zaidi kwa Cain na sio maisha ya bustanini
Naomba kuwasilisha