nyabhingi
JF-Expert Member
- Oct 12, 2010
- 15,638
- 20,254
mkuu gamba nakuheshimu,but dwelling into biblical cheap propaganda itanifanya niquestion umakini wakoMkuu zitto junior asante kwa kunikaribisha katika uzi wako mwingine tena. Lakini nitaandika kwa kifupi tu, ni hivi; hoja hiyo ya kusema eti lile halikuwa "tunda la mtini" bali lilikuwa ni tendo la ndoa mimi binafsi nakataa hasa kutokana na NENO la MUNGU halidanganyi. WARUMI 3:4 "MUNGU ajulikane kuwa mkweli na wanadamu wote waongo"..... Pia soma ZABURI 116:11
Kwa kuwa MUNGU siyo muongo na Musa alikiandika kitabu cha MWANZO kwa kuambiwa na MUNGU mambo yote yaliyotukia, hivyo yote yaliyoandikwa kwenye BIBLIA ni KWELI tupu pasipo shaka yoyote ile!
Ili tujue kwamba lile lilikuwa ni tunda la mti kweli na siyo vinginevyo hebu soma MWANZO 3:6 .."mwanamke alipoona ya kuwa ule mti wafaa kwa chakula, wapendeza macho nao ni mti wa kutamaniwa kwa maarifa, basi alitwaa katika matunda yake akala, akampa na mumewe naye akala".
Nime-highlight hayo maneno hapo juu kwa rangi nyekundu ili tuyajadili na kupata majibu...."ule mti wafaa kwa chakula"... sentensi hii inatosha kabisa kutonesha kuwa ule ulikuwa ni mti wa matunda kama miti mingine ndiyo maana Eva aliona unafaa kwa chakula. Kama tunda lingekuwa ni "uchi" wa Eva au "uchi" wa Nyoka, Je! uchi unafaa kwa chakula? Au tendo la ngono linafaa kwa chakula?
...."basi alitwaa katika matunda yake akala, akampa na mumewe naye akala"...hapa tunaona wazi kabisa ni kitu alikula kwa kutumia mdomo wake, maana baada ya kula alimpatia na mumewe naye akala. Je! kama tunda lingekuwa ngono angewezaje kula "uchi" wake na kumpa mumewe naye ale?
Kuna watu watabisha na kusema; "oooh, hiyo ni lugha tu ilitumika kuficha ukweli". Mimi nasema hapana, kama kitendo cha ngono kingefanyika basi BWANA MUNGU angesema kuwa ni ngono ilifanyika wala asingeficha ukweli. Ngono ilipofanyika kati ya malaika waasi na wanadamu BWANA MUNGU hakuficha bali alisema wazi;
Baadhi ya Malaika walipoacha viti vyao Mbinguni na kuja duniani kufanya ngono na binti za wanadamu, BWANA MUNGU alisema bila kificho, MWANZO 6:1-2 ..".........Wana wa MUNGU waliwaona hao binti za Wanadamu ya kuwa ni wazuri, wakajitwalia wake wowote waliowachagua". Tukubali tu kuwa MUNGU haufichi UKWELI.
Sasa hebu ona ushahidi mwingine kutoka kwenye Biblia kuwa lile lilikuwa ni tunda la mti na siyo tendo la ngono. Soma MWANZO 3:22-24 ... "BWANA MUNGU akasema basi huyu mtu amekuwa kama mmoja wetu kwa kujua mema na mabaya, na sasa asije akanyoosha mkono wake akatwaa matunda ya mti wa uzima akala akaishi milele................akamfukuza huyo mtu, akaweka Makerubi upande wa mashariki wa bustani ya Edeni na upanga wa moto uliogeuka huko na huko kuilinda njia ya mti wa uzima".
Baada ya Adamu na Eva kula matunda ya mema na mabaya, kulikuwa na mti mwingine wenye matunda ya Uzima, ambao sasa ikabidi BWANA MUNGU auwekee ulinzi ili Adamu na Eva wasije wakaenda na kunyoosha mikono yao na kuchuma matunda yake na kula. Kwa mistari hii tunaona UKWELI ni upi na uongo ni upi. MUNGU hasemi UONGO hata siku moja, wala Biblia haijadanganya wala kuuficha UKWELI.
Shetani ni mjanja sana na anatumia ujanja wake kuwadanganya na kuwarubuni Wanadamu ili waone kuwa MUUMBA wao ni muongo. Lengo la Shetani ni kutuaminisha kuwa MUNGU ni muongo na alitumia ujanja huo huo kumfanya Eva amuone MUNGU ni muongo. Shetani amewasaidia Wanadamu kuandika vitabu vingi sana vyenye maudhui ya kupingana na Biblia ili tu kuwafanya wanadamu wamuone MUNGU ni muongo.
Vitabu hivi vyenye maudhui ya kudanganya vipo vingi sana na viliandikwa miaka mingi sana nyuma, enzi za mfalme Nimrodi wa Babeli ya kwanza kabisa. Hapa ndipo palipokuwa chimbuko la dini zote za KIPAGANI na maandiko yenye kupotosha.
biblia ina magepu mengi saaaaan in the first place
sio kitabu reliable for any discussion,kipo shallow,so is quran