Sasa sisi tunaotawaliwa na wake zetu leo tunacomment wapi?Habari za jioni wana JF mada ya leo ni sensitive kidogo hivyo ningependa tuisome kwa umakini,tujifikirishe na tujadiliane kwa mapana bila kashfa za kidini,kejeli,matusi,hasira n.k maana mada hii ni kwa ajili ya kujifunza na kubadilishana mawazo,maarifa,elimu n.k sio uwanja wa vita
View attachment 828516
Mada ya leo ni kuhusu ukweli wa mzazi halisi wa Cain ama tuseme kizazi cha nyoka na kizazi cha Adam. Ikumbukwe nyoka anyeongelewa hapa sio nyoka huyu wa sasa anayetambaa naongelea yule wa kabla ya tunda kuliwa.
Reference yangu itakuwa vitabu vya dini kadhaa kuanzia uyahudini,biblia,apocrypha,pseudipigraphi, maandishi ya wanatheolojia na vitabu vya kihistoria.
UTANGULIZI
Kupitia nadharia hii, yote yanaanzia kwenye bustani ya Eden ambapo tunaona shetani kupitia nyoka akimshawishi Hawa "kula tunda" na katika tunda hilo inaaminika linahusianisha ngono ambapo nyoka alimlala Hawa na kumpachika mimba ambayo baadae alikuja kuzaliwa Mtoto wa uzao huo yaani kizazi cha nyoka yaani Cain ili shetani aweze kuharibu uumbaji wa Mungu.
KWANINI NADHARIA HII?
Ili tuamini Nyoka alilala na mwanamke tunaweza tumia vigezo vifuatavyo
1. Adhabu kubwa ya Mungu kwa mwanamke ilikuwa ni kwenye sekta ya ngono sababu ndipo alipoanguka ndio maana Mungu akamhukumu sababu ya tendo la ndoa na mimba aliyobeba pia.
Mwanzo 3:
16 Akamwambia mwanamke, Hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako; kwa utungu utazaa watoto; na tamaa yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala
Pia shetani tukisoma kwenye kitabu cha biblia (madhehebu kadhaa hukitumia) cha Apocalypse of moses 26:1-4 tunaona hukumu ya Mungu kwa shetani kuwa atamtoa masikio,mabawa na UUME!!!!
Hivyo nadharia hii kuwa ngono ilihusika inapatiwa nguvu kupitia mistari hii
NANI BABA WA CAIN?
Biblia ya kiswahili inasema
Mwanzo 4:1
1 Adamu akamjua Hawa mkewe; naye akapata mimba, akamzaa Kaini, akasema, Nimepata mtoto mwanamume kwa BWANA
Lakini tafsiri iliyofanyiwa uhakiki kupitia New jerusalem Translation inasema hivi kwa kiswahili
...... Nimepata mtoto kutoka kwa malaika wa Bwana
Hivyo kama tafsiri hii ya NJT ina maanisha Adam alikiri kuwa mtoto sio wake ila wa MALAIKA ambaye kwa muktadha huu ni lucifer.
Kwenye biblia ya kiebrania neno lililotumika kwa KUMJUA ni Yada na Eth ambapo Yada baada ya kufanyiwa utafiti mpya limeonekana haimaanishi tu ni kumlala mwanamke bali inamaanisha KUTAMBUA KITU na Eth ina maanisha ALAMA FULANI(mabadiliko) hivyo tukiuandika mstari huu upya kutumia tafsiri ya maneno haya itakuwa hivi;
Adamu akatambua alama/ishara ya mabadiliko juu ya Hawa mkewe; naye akapata mimba, akamzaa Kaini, akasema, Nimepata mtoto mwanamume kutoka kwa malaika wa BWANA
Kwahiyo mpaka hapa tumeshapata maana tofauti kabisa ya mstari huu si ndio wakuu??
JE KWANINI NASEMA CAIN SIO MWANA WA ADAM
1. Biblia huko mbele inamtaja Cain kama alitokana na ''yule mwovu'' yaani shetani
1 Yohana 3:12
12 si kama Kaini alivyokuwa wa yule mwovu, akamwua ndugu yake. Naye alimwua kwa sababu gani? Kwa sababu matendo yake yalikuwa mabaya, na ya ndugu yake yalikuwa ya haki.
View attachment 828519
2. Biblia inamtambua seth kama mtoto pekee wa Adam maana inadai Henoko alikuwa mtu wa 7 baada ya Adam na ukihesabu utagundua imetaja uzao wa seth peke yake na imemuacha Cain peke yake hivyo ikimaanisha Cain hakutambuliwa kma mwana wa Adam
Yuda 1:14
14 Na Henoko, mtu wa saba baada ya Adamu, alitoa maneno ya unabii juu ya hao
View attachment 828520
3. Tunaona hata seth ndio biblia inaonyesha alizaliwa kwa mfano wa sura na mfano wa adam
Mwanzo 5
3 Adamu akaishi miaka mia na thelathini, akazaa mwana kwa sura yake, kwa mfano wake, akamwita jina lake Sethi
Hii yote ikimaanisha Cain hakuwa uzao wa Adam ndio maana hakufanana naye Adam kwa lolote hivyo muandishi hakuona sababu ya kujumuisha jambo hilo alipozaliwa cain.
4. vitabu vinavyotambuliwa na dini ya kiyahudi kama Zohar Pekudei 21:5 kinakubali hoja hii.
Baada ya adam na mke wake kufanya dhambi, na shetani kumjua Hawa na kumnajisi, Hawa alimzaa Cain. Alikuwa na umbo la duniani na kuzimu. Hivyo,alikuwa wa kwanza kuleta kifo duniani,iliyosababishwa na upande wake wa kuzimu,sababu alitokana na uchafu wa najisi ya nyoka (kwa hawa). Asili ya nyoka(shetani) ni udanganyifu,mauaji,na Cain,alijifunza nyendo zake. (Utafsiri binafsi)
HITIMISHO
Kupitia hayo maandiko machache nlioweza kupata ninaweza kufikia hitimisho kuwa kuna uwezekano tumefichwa kwa muda mrefu kuhusu uhalisia wa kilichotokea Eden nikaona nilete nadharia hii JF ili tuweze kufikiri pamoja na kupata ukweli wa jambo hili.
NB: Naomba Moderator msiunganishe nyuzi hii na zingine juu ya bustani ya edeni maana hii imejikita zaidi kwa Cain na sio maisha ya bustanini
Naomba kuwasilisha
Aliyemdanganya Hawa alikuwa nyoka au ni shetani alimwingia nyoka na kisha kumdanganya Hawa?Habari za jioni wana JF mada ya leo ni sensitive kidogo hivyo ningependa tuisome kwa umakini,tujifikirishe na tujadiliane kwa mapana bila kashfa za kidini,kejeli,matusi,hasira n.k maana mada hii ni kwa ajili ya kujifunza na kubadilishana mawazo,maarifa,elimu n.k sio uwanja wa vita

i wish hii post ungeifungulia thread. bonge moja ya post.Umechambua vizuri Sana but ukija kwenye uhalisia wenyewe kuna mambo mengi sana yamefichwa hasa kwenye biblia takatifu,nchi kama ulaya huko wameamua kuachana kabsa na mambo ya dini hasa dini zenye kutumia biblia kama chanzo cha kujua ukweli...tumebaki sisi Africa kutumia biblia kama reference ya chimbuko la uhai wa human race katika ulimwengu huu...kama ni hivyo kwanini sasa nchi zilizoendelea zimeachana na habari kama hizo za kutumia bible kama reference point ya kukuonesha original ya mwanadamu?? do you think kuna uhalisia hapo,?? kama maandiko menyewe kuyaelewa mpaka uconnect dot flan ndo unaanza kupata ukweli..!! kwanini kama ni uhalisia usiwekwe na mwandishi mmoja ila et ukweli mpaka uanze kugess maandiko ya flani na flani ndo unapata connection..dont we see that we are wrong from point of contradiction...??
Unajua kuna point mimi najaribu kujiuliza kwanini mzungu kaachana na mambo ya bible kwenye kutafuta reality that put human being into existance ila kajikita zaidi na evolution ya cosmos ilivyotokea..?? binafsi swala la biblia kama reference ya kunifanya nidig where I evolved nishaanza kuiacha kabsaa make kuna nadhalia nyingi sana zinaelezea jinsi bible ilivyokuja kuvurugwa na mrumi na kupelekea kufanya inversion na edition tofauti za kurasa ,kitu kilichopelekea watu kutokuielewa vizuri bible kwa undani zaidi...
kuna documentary moja nimeisoma inagusia jinsi vatcan alivyokuja kuedit baadhi ya verses katika bible na kufanya msomaji kupata difficultness namna ya kuelewa the real chronological order ya bible ilivyokuwa...inasemekana kuwa, the real original bible was written in ascending order of knowlege yani imeanza kuelezea namna how the universe arose,na how cretures got into existance and finally how human races got to evolve in this world( universe) ,lakini kutokana na hao mageniuz wa dunia ambao hawakutaka kuuruhusu msahafu huo kusomwa na kila mtu ndo wakaugawanya into different categories na kuchanganya chapters kias kwamba ukisoma mstari wa matayo pekee huwezi kuuelewa mpaka ukajazilizie kwa marko ndo unaanza kupata picha na badae uende matendo ya mitume mpaka waefeso ndo upate half of its reality and robo ya ukweli (truth),,hatuoni kuwa ukweli kuwa bible was real put under several manipulations and editions za kufa mtu ndo mana tunakesha kuujua ukweli...nanukuu maneno ya papo John Paul the second anasema" The bible under its verses has a meaning inside " ndo mana kumepelekea waumiza vichwa nchi za wenzetu kushitukia mchezo huo make unashangaaa watu wanaumiza vichwa miaka nenda rudi lakini hakuna mtu anayeweza kuconnect dots kwenye bible na kucome up na general consensus juu ya uhalisia wa kilichoandikwa kwenye bible...ila inawezekana kabsaa ni kweli the reality was put through the bible but manipurated to loose its truth to the people but for the sake of few ones to understand how nature is.....
Lakini ndo tuseme kuwa bible iwe ngumu kueleweka kiasi hicho kuzidi syllubus ya masomo ya engenering na medicine ambayo ni magumu lakini watu wanasoma wanaelewa na wanaput into practise na kuelewa mfumo mzima wa mambo yaliyoelezewa kwenye mitaala hiyo lakini kwanini bible imekuwa kitendawili kuelewa ukweli wa mambo ndani yake.?? kwanini bible imechanganya zaidi!?? inanifanya nianze kuamini documentary inayosema kuwa ni kweli the bible was written explaining everything what happened since bustan ya eden mpaka anguko la dhambi but it was reversed and edited and some points were hidden to make a meaning got lost ....
Naumiza kichwa sana juu ya tafsiri ya maneno yaliyomo ndani ya biblia ya sasa inapojaribu kuelezea jinsi uzao uliopo ulipotoka lakini stili inafell kuelezea how different races zilivyokuja kutokea au ndo kusema kwamba shetani aligawanya hizi race katika hali tofauti tofaut kulingana na pendekezo lake...?? ngumu kumeza hii ...sometimes if you stick yourself to get the meaning from the bible you will finally land into errors when comes a matter to understand how the reality is....
Ila kuna principle ambayo binafsi naiamini na inasema kuwa ," aliyekuzidi kukutangulia pia ,tukiangalia watu waliokuletea bible ndo kwanza waiweka mbali na upeo wa macho yao and they are busy to open another window to know the reality ,why are we still finding the unknown inside the edited writtings...?? do you think kwamba tutaweza kuupata ukweli namna uzao huu ulipotoka kupitia maneno yalioandikwa ndani ya biblia ya leo..?? najaribu kujiuliza kwa kichwa tu....
Mwisho nahitimisha kwa kusema kuwa " inasemekana lakini eti kuna kiwango ambacho ukifikia hasa katika mambo ya dini unapewa some real documentary ya mshahafu mzima unavyoelezea how descendant of human race came to arise ...
Na miongoni mwa watu waliosoma baadhi ya mtiririko huo ni Leonardo DA VINCI na ISAAC NEWTON as one of the former seminarians walioaminika na kuambiwa watunze siri hiyo ,mtu mwingine aliyesoma mtiriko huo ni bwana mdogo Raphael aliyekuwa geniuz wa kudraw huko Basilia,Roma....haya maneno niliambiwa na jamaaa mmoja yupo mwaka wa 6 upadri na alinidokezea sana kwa hiyo ilikuwa ni katika kujaribu kuelezea how the truth is inside the current bible...
Nimekuvulia kofia mkuu, umechambua vizuri sana. Na ndiyo ukweli.Mkuu zitto junior asante kwa kunikaribisha katika uzi wako mwingine tena. Lakini nitaandika kwa kifupi tu, ni hivi; hoja hiyo ya kusema eti lile halikuwa "tunda la mtini" bali lilikuwa ni tendo la ndoa mimi binafsi nakataa hasa kutokana na NENO la MUNGU halidanganyi. WARUMI 3:4 "MUNGU ajulikane kuwa mkweli na wanadamu wote waongo"..... Pia soma ZABURI 116:11
Kwa kuwa MUNGU siyo muongo na Musa alikiandika kitabu cha MWANZO kwa kuambiwa na MUNGU mambo yote yaliyotukia, hivyo yote yaliyoandikwa kwenye BIBLIA ni KWELI tupu pasipo shaka yoyote ile!
Ili tujue kwamba lile lilikuwa ni tunda la mti kweli na siyo vinginevyo hebu soma MWANZO 3:6 .."mwanamke alipoona ya kuwa ule mti wafaa kwa chakula, wapendeza macho nao ni mti wa kutamaniwa kwa maarifa, basi alitwaa katika matunda yake akala, akampa na mumewe naye akala".
Nime-highlight hayo maneno hapo juu kwa rangi nyekundu ili tuyajadili na kupata majibu...."ule mti wafaa kwa chakula"... sentensi hii inatosha kabisa kutonesha kuwa ule ulikuwa ni mti wa matunda kama miti mingine ndiyo maana Eva aliona unafaa kwa chakula. Kama tunda lingekuwa ni "uchi" wa Eva au "uchi" wa Nyoka, Je! uchi unafaa kwa chakula? Au tendo la ngono linafaa kwa chakula?
...."basi alitwaa katika matunda yake akala, akampa na mumewe naye akala"...hapa tunaona wazi kabisa ni kitu alikula kwa kutumia mdomo wake, maana baada ya kula alimpatia na mumewe naye akala. Je! kama tunda lingekuwa ngono angewezaje kula "uchi" wake na kumpa mumewe naye ale?
Kuna watu watabisha na kusema; "oooh, hiyo ni lugha tu ilitumika kuficha ukweli". Mimi nasema hapana, kama kitendo cha ngono kingefanyika basi BWANA MUNGU angesema kuwa ni ngono ilifanyika wala asingeficha ukweli. Ngono ilipofanyika kati ya malaika waasi na wanadamu BWANA MUNGU hakuficha bali alisema wazi;
Baadhi ya Malaika walipoacha viti vyao Mbinguni na kuja duniani kufanya ngono na binti za wanadamu, BWANA MUNGU alisema bila kificho, MWANZO 6:1-2 ..".........Wana wa MUNGU waliwaona hao binti za Wanadamu ya kuwa ni wazuri, wakajitwalia wake wowote waliowachagua". Tukubali tu kuwa MUNGU haufichi UKWELI.
Sasa hebu ona ushahidi mwingine kutoka kwenye Biblia kuwa lile lilikuwa ni tunda la mti na siyo tendo la ngono. Soma MWANZO 3:22-24 ... "BWANA MUNGU akasema basi huyu mtu amekuwa kama mmoja wetu kwa kujua mema na mabaya, na sasa asije akanyoosha mkono wake akatwaa matunda ya mti wa uzima akala akaishi milele................akamfukuza huyo mtu, akaweka Makerubi upande wa mashariki wa bustani ya Edeni na upanga wa moto uliogeuka huko na huko kuilinda njia ya mti wa uzima".
Baada ya Adamu na Eva kula matunda ya mema na mabaya, kulikuwa na mti mwingine wenye matunda ya Uzima, ambao sasa ikabidi BWANA MUNGU auwekee ulinzi ili Adamu na Eva wasije wakaenda na kunyoosha mikono yao na kuchuma matunda yake na kula. Kwa mistari hii tunaona UKWELI ni upi na uongo ni upi. MUNGU hasemi UONGO hata siku moja, wala Biblia haijadanganya wala kuuficha UKWELI.
Shetani ni mjanja sana na anatumia ujanja wake kuwadanganya na kuwarubuni Wanadamu ili waone kuwa MUUMBA wao ni muongo. Lengo la Shetani ni kutuaminisha kuwa MUNGU ni muongo na alitumia ujanja huo huo kumfanya Eva amuone MUNGU ni muongo. Shetani amewasaidia Wanadamu kuandika vitabu vingi sana vyenye maudhui ya kupingana na Biblia ili tu kuwafanya wanadamu wamuone MUNGU ni muongo.
Vitabu hivi vyenye maudhui ya kudanganya vipo vingi sana na viliandikwa miaka mingi sana nyuma, enzi za mfalme Nimrodi wa Babeli ya kwanza kabisa. Hapa ndipo palipokuwa chimbuko la dini zote za KIPAGANI na maandiko yenye kupotosha.
Kibiblia nyoka wa mwanzo anadaiwa kuwa ni shetani!!Aliyemdanganya Hawa alikuwa nyoka au ni shetani alimwingia nyoka na kisha kumdanganya Hawa?
Ila aliyepewa adhabu ni nyoka, kwamba atatembea na tumbo na kula mavumbi, kwanini nyoka atajwe kwenye adhabu na sio shetani ?
Kumbuka Biblia humtaja shetani kama 'joka' wa zamani audanganye ulimwengu, je huyu 'joka' ndiye aliyemdanganya Hawa ?,
Au nyoka alikubali kutumika na shetani kumharibia 'maisha' mwanadamu (kumbuka alitajwa kama mwerevu), hivyo tukisema aliadhibiwa kwa kukubali kwa hiyari yake kutumika na shetani kumharibia 'maisha'mwanadamu tupo sawa ?
yaani nilitaka niseme hivo hivo na mm....nyoka fala kweli huyu...Nimesoma intro nilipofika kwa huyo mdada nikatulia kidogo, kwanini huyo nyoka kakaa hapo si angekaa juu ya mti mtu.😡
Huu ni ugaidii.
BTW.
Ngoja wajuvi waje tuone wanasemaje..

Hadithi za kitotoBaadhi tuna jua habari hii kuwa kulikuwa na ulimwengu wa majini kabla yetu sisi binadamu
Walimuasi M/Mungu na ndipo ghasia ikatokea ya kuwaadhibu majini wote katika Ardhi wengi walikufa na wengine kukimbilia misituni, kwenye majabar, na sehemu za maji mengi na machache kunusuru Nafsi zao.
Ila mmoja tu mtoto mdogo Sana aliponyeka na akaenda na malaika katika mbingu na kuishi miongoni mwa malaika baada ya Mola wa Ulimwengu kuruhusu. Lakini hakuwa malaika Bali Jinni. Na utashi wake haukuwa ukifanana na Malaika japo alikuwa miongoni mwao, alikithiri kwa ibada na kumsifu Mola katika kipindi chote
Tambua, Malaika Hana sifa za jinsia, matamanio, na mipango yeye hufata amri ya Mola wake na kutii tu tofauti na Jinni
Hivyo siku ile ile Moja siku Mwenyezi mungu alipouumba Adam kwa mkusanyiko wa Udongo mweusi na kadha wa kadha aliita malaika wake pamoja na Jinni Yule aliyelelewa mbinguni.
Malaika wakamwambia si anaenda kumleta kiumbe atakae leta ufisadi, kufru na Kila aina ya balaa katika Ardhi
( Malaika waliona mbele kwa kulinganisha wale majini waliowangamiza kipindi kile na baadhi yao kwenda jificha sehemu sehemu)
Mola aliwajibu nayajua msiyo yajua je yapi hayo.
Adivatise, aliwaletea vitu na kuwataka wavitaje walishindwa kwa kukosa elmu peke yake Adam alikuwa akijua na kuwatajia vitu walivyokuwa wakiishi navyo pasina wao kujua majina yake
(Mola alijua na alikuwa kwenye kuyakamilisha wasiyoyajua)
Alipo waamrisha wamsujudie Adam sijda ya heshima na ubora baada ya kupuliziwa roho malaika wali tii lakin Yule Jinni alikataa
Kwanini?
Kwa sababu ya matashi yake ya Uhuru wa machaguzi na matamanio aliumbwa hivyo, isitoshe udhaifu wa Adam kwa pande la nyama lenye vizuizi.
Na uwezo wa Jinn kuweza kupita Kila Kona ya mwili wa Adam na mishipa yake. Aligundua udhaifu mkubwa wa Adam akajiona Bora kumzidi Adam.
Alikataa kusujud sijda ya heshima. Ndipo Mola akamlaan vikali akaitwa Ibilisi/shetan na yeye akaomba kuto patwa na umauti mpka umma wote utakapo Isha alikubaliwa. Na akaahidi kupoteza Ummat wote ila Yule mwenye akili tu hatoweza kumpoteza.
Haya, Adam akawa mbinguni Akiishi wakat ibilis ameshafukuzwa na anachuki na Adam. Mola akamuumba Hawa mwanamke tokea katika asili ya ubavu wa kushotoni. Ili awe wa aina yake atakae mliwaza.
( Tunaona hapa udhaifu wetu wetu wanaume upo kwa wanawake) sehemu iliyotoka kwa mwanamke ndio ukamilisho wa mwanaume)
Mola akawaambia kuleni kuleni nendeni fanyeni chochote ila ule mti msiusogeleee Wala kula matunda yake.
Haya, Ibilisi akampitia Hawa kwa sababu aliamini ndiye dhaifu kuliko Adam na Adam ndio sehemu ya Udhaifu wake. Alijua tu
Hivyo Hawa alikubali na akamshawishi Adam wakizani Kuna neeema ambayo Mola kawaficha hataki waijue.
Yale Yale ya matashi na tamaa walizoumbiwa, Adam akashawishika kupitia Hawa aliyedhaifu zaidi kwa Ibilisi
Wakamkosea Mola, wakajikuta aibu zao zikiwa wazi, wakaziona tupu zao ambazo hawakuzijua kabla..Walipatwa na aibu. Mola akawaambia Sasa nawatoa kwenye neema niliyowaweka akarudisha Dunia ambako ndiko majini waliianza kuishi kabla ya Adam.
Huku akiwaambia mmemjua Adui yenu katika Ardhi na salama yenu Ni kwangu. Atawafata kuwapoteza Kama alivyowapoteza.
Cha kujifunza na kujiuliza
1) Kwanini Mola alimuumba mwanamke (Hawa) kutoka sehemu ya mwili wa Adamu??
2) Je Ibilisi kwa Nini alipitia njia ya kumshawishi Hawa na akafanikiwa na sio Adam?
3) Imekuwaje Hawa kumshawishi Adam kwa urahisi kuusogelea ule mti na kula tunda?
4) inamaana wasinge usogelea Mti ule Ulimwengu huu wa Ardhi binadamu tungefikaje?
Kwa maana ya haraka haraka
Ibilisi alitegwa akategeka na Adam na Hawa nao walitegeka pasina kujua. Kuwa Mola wa Ulimwengu anajua wasiyoyajua. Ibilisi akajiona mjanja
Yote ya yote Mwenyezi Mungu ndiye anayejua tusiyoyajua Kama alivyo alivyo waambia Malaika wake.
Hicho ndicho ninachokijua, kujua zaidi pekua maandiko ya iman zote utajua zaidi ya elmu hi ndogo niijuayo.
Mola anasili kubwa Sana kwa viumbe wake
Asanteni sana
Tatizo Eva na nyoka walijua wanapigwa picha.yaani nilitaka niseme hivo hivo na mm....nyoka fala kweli huyu...
Sahihi kaleta vyemaDu umeichambua vema mkuu maada hii.inawezekana ni kweli maana baadhi ya maandiko husema enyi kizazi cha nyoka.