Je, hili limewahi kukutokea?

Je, hili limewahi kukutokea?

Ila nadhani selifika "pameibua vipaji sana"
emoji3.png
tafsida zako sasa 😂😂😂😂 Vipaji mara kuwekana🙌🙌🙌😁😁😁🤣
 
Acha tu mie hadi tulionana hadi Raha kabisa anajua kitu caring Ile kukataa atakacho basi
Hongera walau ulipiga hatua moja mbele.

Mie mdau wangu niliyemuongelea akili yake ina uwezo mkubwa wa kupambanua mambo haraka mno, imebidi niandike kwa tahadhari kubwa na nitumie ID mbadala. Hapa nikithubutu kutaja tukio moja tu, lazima agundue namuongelea yeye. Sijui ingekuwaje kama tungepata fursa ku-consume lile penzi!

J jamani, so romantic, so briliant. Mwanadamu anayejitambua nafsi yake. Hatimaye imebaki stori.
 
Kwamba hamkuonana kabisa? Nimecheka asee!!
Ukumbuke tuliamini kwamba kila mmoja ndio kafika. Hatukuwa na haraka wala papara. Picha tulibadilishana chache (Carefully selected 😛) kwa madai ya kuvizia kutovuruga suprise ya kukutana ana kwa ana (which never came to pass 😂😂😂)na tulizoea kutumiana voice notes mara kwa mara. Kiujumla ukaribu 'wenye afya ' ulikuwepo.
 
Maisha ni fumbo ndugu zangu. Mimi niliwahi kumpenda mwananchi mmoja humu humu jf, na ilinoga hasa. Najua hata hapa atakuja kusoma, anyway!

Iliniumiza mno kutengana naye japokuwa haikuwa na jinsi - tofauti ya umri ilikuwa ni kubwa mno. Hilo jambo niligundua mwenyewe bila yeye kunijulisha. Ila usiombe, ni huzuni, tulikuwa tume-share mengi mno. Kama ni Long distance relationship isiyo na upweke wowote ndio ile sasa. Mdau alijua kupenda kwa kalamu, alionekana ni perfect match kama vile kuokota embe chini ya mnazi. Tulizoea kuongea mengi na kukubaliana lakini utata ukaanza pale tulivyoahidiana kukutana live maana tuliishi mikoa tofauti.

Imagine enzi hizo ilikuwa meseji zake nazisubiri huku kimoyo kinapwita! Na nikipokea ujumbe wake napata nguvu ya ajabu kuwajibika kwa ajili ya familia tarajiwa

Alinijulia yule mtu, na alionekana ni 'jiniasi'. Pia kuna stori najua alidanganya na alijua nikijua lazima nitam-mind, ikafika mahali mawasiliano yakaanza kuisha polepole....hebu fikiria miezi minne ya raha za maandishi zikakatika ghafla!

J kokote uliko, maisha hayana fomula. Leo mwenzio nimekukumbuka na kukuenzi kwa maandishi haya.
Kwa hiyo mliachana bila kuonana kabisa? Aisee
 
He! Leo ndo najua kuna haya maajabu jf. Au namimi uskute kuna mtu ananipenda na sijui.. Anaenipenda awe wazi nimjue 🤣😂
 
Back
Top Bottom