Je, hili limewahi kukutokea?

Je, hili limewahi kukutokea?

Hahaha, mkuu tangu ulipoacha kukwoti hutaki tena..hekaheka za humu labda zinataka uwe underground ndio utafaidi...LABDA..mimi haya mambo pia kwangu magumu🤣🤣
Kabesaaaaa sitaki hata kusikiaaaaa😁😁😁🤣🤣🤣🤣! Heko kwa wanaoziweza walaii auuuwiiiii!!
Tinsley dear njooo ufongoke hukuuu😂😂
 
Sijapenda hapo pa kuzimia sekunde 3 ungefanya hata 10...ulimpenda kweli??
Sikumpenda kweli, nilimtamani tu

Sasa nikaogopa kumchezea kaka wa watu, hivyo nikaacha hata sikuwahi mfanya anotice
 
Umewahi mpenda mtu humu Jamii Forums ukaona huyu kakupenda kweli na ukampenda kweli halafu mlipoachana ikakuuma roho? Mimi ndiyo.

Niliwahi kumpenda mwanaume humu na hakuniacha, ila nilishindwa masharti, ila waleo namkumbuka sana. Ila yeye ndiyo basi tena, hajali tena, kipindi cha 2019 nilipofungua Unique Flower.

Je, wewe iliwahi kukutokea hali hii?
Maisha ni fumbo ndugu zangu. Mimi niliwahi kumpenda mwananchi mmoja humu humu jf, na ilinoga hasa. Najua hata hapa atakuja kusoma, anyway!

Iliniumiza mno kutengana naye japokuwa haikuwa na jinsi - tofauti ya umri ilikuwa ni kubwa mno. Hilo jambo niligundua mwenyewe bila yeye kunijulisha. Ila usiombe, ni huzuni, tulikuwa tume-share mengi mno. Kama ni Long distance relationship isiyo na upweke wowote ndio ile sasa. Mdau alijua kupenda kwa kalamu, alionekana ni perfect match kama vile kuokota embe chini ya mnazi. Tulizoea kuongea mengi na kukubaliana lakini utata ukaanza pale tulivyoahidiana kukutana live maana tuliishi mikoa tofauti.

Imagine enzi hizo ilikuwa meseji zake nazisubiri huku kimoyo kinapwita! Na nikipokea ujumbe wake napata nguvu ya ajabu kuwajibika kwa ajili ya familia tarajiwa 😇

Alinijulia yule mtu, na alionekana ni 'jiniasi'. Pia kuna stori najua alidanganya na alijua nikijua lazima nitam-mind, ikafika mahali mawasiliano yakaanza kuisha polepole....hebu fikiria miezi minne ya raha za maandishi zikakatika ghafla!

J kokote uliko, maisha hayana fomula. Leo mwenzio nimekukumbuka na kukuenzi kwa maandishi haya.🥰
 
Back
Top Bottom