Uchaguzi 2020 Je, Halima Mdee amefanya nini Kawe kwa miaka 10 ya ubunge wake kustahili kuendelea? Sikia ya Askofu Gwajima, 28 Oktoba fanya uamuzi sahihi

Nadhani swali ni serikali imefanya nini kwenye jimbo la Kawe maana jukumu la kuleta maendeleo ni serikali na sio la mbunge. Kama katika miaka 10 ya ubunge wa Halima hapajakuwa na maendeleo Kawe inayopaswa kuhojiwa ni serikali na sio mbunge.

Swali kwa Halima ni je katika muda wake huo amewapigania watu wa Kawe na Tanzania ili wapate maisha bora zaidi? Kwa vile chama chake hakikuwa madarakani, wananchi wanapaswa kuwauliza waliokuwa madarakani kwa nini hawakutilia maanantaina kilio cha mbunge wao?

Kumchagua mtu kwa vile ana pesa za kuchonga barabara ni kujidhalilisha maana mtakuwa mmenunuliwa. Chagueni mtu atakayewapigania ili mtendewe haki kutokana na kodi mnayolipa. Maendeleo sio fadhila, ni haki yenu.
Amandla...
well said .

Tunataka watu makini kama "Fundi mchundo" na si akina Njaa.
 
Hivi we P mzima kweli ? Halima mdee ndio anakusanya kodi yaani wakusanye kodi wengine , Halima mdee ndio alete maendeleo ? Kama vile hujui kazi za mbunge ? Kumbe unafanya makusudi , kwahiyo wanakawe unawashauri wachague mcheza sinema za utupu sio ? We si mtu mzima kabisa eti msomi ?View attachment 1558786


Kama unaweza kutuletea nyengine yenye maandishi ya CCM badala ya KAWE ningalikushukuru sana
 
Kaka Paskali, siku utakayokuja kukumbuka kuwa maendeleo yetu hayaletwi na Mbunge bali ni kodi zetu ndipo mtakapoacha kumwambia Baba yenu kuwa hii sio nchi ya chama kimoja.

Maendeleo ya jimbo la kawe yanaletwa na kodi zetu, na siku mtakayokuja kutuambia kwenye kampeni eti hamleti maendeleo kwa kuwa tumechagua upinzani, nisione TRA wala manispaa kwenye biashara yangu..watakuwa halali yangu.
 
Uko sahihi mkuu,huyu Pascal badala ya kumjadili mgombea wao kigeugeu unamrukia Halima hivi wamelogwa??Halafu mccm analeta mada hapa tumfanyie assessment Halima kwa lipi watamfanyia fair??wazinzi na wakabila hawawafanyii assessment mimi nadhani huyo na hao waliompitisha mzinifu ndio wakufanyiwa assessment maana huyo mgombea wao hata wajumbe walimkataa vitu vya ajabu kabisa hivi.

Mkuu nakubaliana nawe.

Nadhani huyu Pasacali tangu njaa ya Corona na pia alipojisajili rasmi mboga mboga yafuatayo yanamsibu:

1. Inabidi afanye yote kuchekechea uteuzi.
2. Hana uhuru wa kuanzisha au kuchangia mada akiwa huru kama kina sisi.

Kimsingi hana amani kabisa anakufa na tai shingoni tu.

Hii ni tathmini kumhusu bwana Pasacali. Akitaka tutamletea ya huyo askofu uchwara kabla ya Kamanda Halima.
 
Hahaha yani hata wewe unaweza kuuliza swali hili, kwamba Halima Mdee kaifanyia nini kawe kwa miaka 10?

Haya maswali tuachie sisi siyo wewe.

Unazijua kazi na majukumu ya mbunge?!

Au nawe ndio wale kwamba Mbunge
ajenge madaraja, au alete maendeleo?!

Bandika hapa kazi na majukumu ya mbunge kisha utaelewa logic yangu.
Nimependa sana mtazamo wako. Aina ya watu kama wewe ndio wakazi wa Kawe bravo. Umewakilisha mawazo yangu kwa ufasaha sana na briefly
 
Nadhani swali ni serikali imefanya nini kwenye jimbo la Kawe maana jukumu la kuleta maendeleo ni la serikali na sio la mbunge. Kama katika miaka 10 ya ubunge wa Halima hapajakuwa na maendeleo Kawe inayopaswa kuhojiwa ni serikali na sio mbunge.

Swali kwa Halima ni je katika muda wake huo amewapigania watu wa Kawe na Tanzania ili wapate maisha bora zaidi? Kwa vile chama chake hakikuwa madarakani, wananchi wanapaswa kuwauliza waliokuwa madarakani kwa nini hawakutilia maanani kilio cha mbunge wao?

Kumchagua mtu kwa vile ana pesa za kuchonga barabara ni kujidhalilisha maana mtakuwa mmenunuliwa. Chagueni mtu atakayewapigania ili mtendewe haki kutokana na kodi mnayolipa. Maendeleo sio fadhila, ni haki yenu.
Amandla...
Zaidi ya kutukana Bungeni, kufungiwa Bungeni kutokana na utovu wa nidhamu, kususia kikao cha Bajeti hayo ndiyo nimeyaona amefanikiwa kwa kiwango kikubwa kuibana Serikali.
Nb: Ukweli hakuna alichokifanya
 
Ataku prove wrong very soon ila Mkuu Pascal Mayalla umeonyesha kiwango cha juu cha unafiki. Unataka Halima Mdee atoe fedha zake mfukoni kufanya shughuli za maendeleo?

Au tayari umeona Msukuma mwenzio amepitishwa kugombea Kawe kupitia CCM ndipo unasahau hata imani yako ya Ukatoliki na kuanza kumpigia kampeni huyu PornStar Gwajima?

Kweli umesahau kauli za Magufuli kuwa a hapeleki maendeleo kwenye Jimbo lililo chini ya upinzani kama Kilwa kwa Bwege
 
Ndugu Mayalla. Baadhi ya wanachadema wengi uwezo wao wa kufikiria ni Mdogo sana. Na chadema imetumia uwezo mdogo wa wafuasi wao kufikiri kujipatia Madaraka.

Hili unalolizungumza la Mbunge Anae maliza Muda wake wa kawe halipotu kawe lipo kwenye Majimbo yote yaliyochukuliwa na Upinzani.

Wabunge wao hawajishugulishi hata kuchimba tundu la choo cha Shule ya msingi wanachowadanganya wananchi wao ni kwamba wao Hawakusanyi kodi. Lakini wana sahau wamepewa PESA ya Mfuko wa jimbo.

Mimi nakubaliana na WOTE wanao kuwa mstari wa Mbele kuwaletea wananchi Maendeleo na sio Maneno matupu.

Huwezi kumchagua Mbunge Ambae Kila siku ni kususa Susa na kuitukana Serikali utegemee Kwenye jimbo lenu mtapata maendeleo.

Lakini nikishukuru chama changu cha mapinduzi kimekua na Upendo hata kwa Yale majimbo Ambayo hawakuchaguliwa wamepeleka Maendeleo.
 
Mkuu nakubaliana nawe.

Nadhani huyu Pasacali tangu njaa ya Corona na pia alipojisajili rasmi mboga mboga yafuatayo yanamsibu:

1. Inabidi afanye yote kuchekechea uteuzi.
2. Hana uhuru wa kuanzisha au kuchangia mada akiwa huru kama kina sisi.

Kimsingi hana amani kabisa anakufa na tai shingoni tu.

Hii ni tathmini kumhusu bwana Pasacali. Akitaka tutamletea ya huyo askofu uchwara kabla ya Kamanda Halima.
Njaa inamsumbua
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom