Uchaguzi 2020 Je, Halima Mdee amefanya nini Kawe kwa miaka 10 ya ubunge wake kustahili kuendelea? Sikia ya Askofu Gwajima, 28 Oktoba fanya uamuzi sahihi

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,007
112,463
Wanabodi,

Mimi ni mkazi wa Kawe, kwa vile sasa tuko kwenye kampeni za uchaguzi, ili tumtendee haki Mbunge wetu aliyemaliza muda wake, Mhe. Halima Mdee, ambaye, baada ya kuwa Mbunge wa Kawe kwa vipindi viwili mfululizo, na sasa anaomba tena tumchague, hivyo nauliza kama kuna mtu yoyote anaweza kutueleza humu, hata jambo moja tuu, Jee Mbunge wetu Mhe. Halima Mdee, amelifanyia nini jimbo la Kawe katika kipindi chake chote cha miaka 10?, ili tumfanyie assessment kama anastahili jee anastahili kuongezewa miaka mitano mingine, or she did nothing hivyo anastahili apumzishwe?

Declaration of Interest
Japo mimi Paskali Mayalla kwa sasa ni kada wa Chama Cha Mapinduzi, CCM, lakini bandiko hili sio la ukada au propaganda za kampeni za uchaguzi, bali ni bandiko hojaji ya halali na swali la ukweli la mwana Kawe, kuuliza Mhe. Halima Mdee ameifanyia nini Kawe in the past 10 years kustahili kuendelea?

Rais John Kennedy wa Marekani aliwahi kusema, " usijiulize Marekani imekufanyia nini, bali ujiulize, wewe utaifanyia nini Marekani". Mhe. Halima Mdee ndie Mbunge wetu Kawe kwa kipindi cha miaka 10, naomba kuuliza kwa anayejua, Jee Halima Mdee ameifanyia nini Kawe?.

Najua kuna watu watasema kazi ya kuleta maendeleo ni kazi ya serikali, kazi ya Mbunge ni kuisimamia serikali, tumekuwa tukishuhudia wabunge wa majimbo mengine wakipigamia majimbo yao Bungeni, Jee Mbunge wetu Mhe. Halima Mdee, aliwahi kupigania nini cha maendeleo ya Kawe?. Kama kuna anayejua humu, atuambie hata kitu kimoja tuu cha Kawe ambacho Halima Mdee alikipigania?.

Kuna zile fedha za Mfuko wa Jimbo. Jee kuna mwana Kawe yoyote, aliwahi kumshuhudia Mbunge wetu Mhe Halima Mdee akija eneo lolote la Kawe na kuchangia shughuli zozote za maendeleo kupitia fedha za mfuko wa Jimbo?.

By the way: Leo nilikuwa mahali nikamsikia Askofu Gwajima, kumbe huyu Askofu ni mdau mkubwa wa maendeleo ya watu wa Kawe kwa kipindi kirefu na ameisha fanya mambo makubwa kwa wana Kawe kama Mwananchi tuu wa kawaida bila hata kujua kuwa kuna siku atakuja kugombea ubunge wa Kawe.

Kumbe Askofu Gwajima baada ya kuhamia Kunduchi Salasala, alikuta kuna tatizo la maji. Na kufuatia eneo la Kunduchi ni eneo la pembezoni mwa bahari, ukichimba visima vifupi, utapata maji ya chumvi, Hivyo Askofu Gwajima kwanza alichimba visima virefu 12 vya mita 300 kwenda chini ili kupata maji safi na salama kwa ajili ya wana Kawe!. Miongoni mwa wafaidika wa visima hivyo virefu, kwenye misikiti 7 ya Salasala hivyo kuwapatia maji Waislamu, maji ya kutawadha kabla ya kuswali.

Kisha akayatafuta maji ya Dawasco, yanapita mbali, akaomba kibali Dawasco, akanunua manomba kama ya Dawaco ya kusambaza maji, akayatandika kuwatumia mafundi wa Dawasco, anunua pump ya mamilioni kutoka Ujerumani, akanunua mita za maji kama za Dawasco na kusambaza maji kwa kaya 250 za majirani wake wanaomzunguka, sasa wanapata maji safi na salama!.

Askofu Gwajima tayari ameisha saidia magari 7 ya ambulance za wagonjwa kwa hospitali mbalimbali, na kuahidi atazipatia magari ya wagonjwa hospitali za Kawe na Kinondoni.

Gwajima amesema, kazi ya kuwaletea maendeleo Watanzania sio kazi ya serikali pekee, ni kazi ya wananchi kwa kushirikiana na serikali, hivyo hapo alipo, tayari ameagiza tinga tinga la kuchonga barabara na malori mawili ya tipper, ambapo barabara zote za Kawe na Kinondoni zitachongwa, vijana wa Kawe watapatiwa ajira za kuchimba mitaro ya maji, hivyo kama ni serikali, itabaki kazi ya kuziwekea tuu lami!.

Mwana Kawe yoyote akiyasikia haya Askofu Gwajima aliyoyafanya Kawe, kabla hata hajawa Mbunge, ukilinganisha na alichofanya Mhe. Halima Mdee kipindi chake chote cha miaka yake 10!, ukiambiwa umchague mmoja kati ya hawa wawili, utamchagua nani?.

Utakubaliana na mimi kuuliza, Jee is it, it's high time, tumshukuru Mhe Halima Mdee kwa utumishi wake wa miaka 10 Kawe?, na tumuage kwa upendo, heshima na taadhima kwa kumwambia, Bye Bye Mhe. Halima Mdee Kawe, asante sana kwa utumishi wako wa miaka 10 Kawe?, na Jee sasa tumkaribishe Askofu Dr. Josephat Gwajima kwa kumwambia, "karibu, Kawe Askofu Gwajima ili kuikamilisha kazi nzuri ulioshaanza kuitenda kabla hata hujawa Mbunge?.

Kama kuna mtu yoyote ana video clip yoyote ya Mbunge wetu Mhe. Halima Mdee akishiriki shughuli yoyote ya maendeleo Kawe, naomba aielete ili angalau tumuone!
Shuhudia mwana Kawe huyu anavyojituma kwenye kuleta maendeleo

View attachment 1558915

Nauliza tuu!.

Paskali
 
Paskali nisiwe mnafiki siwezi mchagua Gwajima kwakuwa alishasema anataka kuigeuza misikiti kuwa Sunday schools, nikiwa kama muislam nawaza huyu hakuwa na madaraka aliongea vile je nikimkabidhi madaraka itakuwaje? Mimi ni muislam na najivunia kuwa muislam
 
Naona mlioshindwa kura za maoni mnatekeleza agizo la Mwenyekiti wenu kuwapigia debe waliopita!Hapa unajiwekea kafursa ili ukumbukwe kwenye teuzi kwa kutii maagizo ya mwenyekiti!Huwezi kutenganisha ukada wako na mawazo yako,kwa wanaJF utakuwa mnywa maji ya kijani tu!

Kujijengea heshima fulani na kuaminika inachukua muda mrefu,ila kuvivunja vitu hivyo ni ndani ya sekunde moja tu!

Ulishapoteza hilo na huenda mpaka unaingia kaburini,level ya heshima uliyokuwa nayo JF isirudi tena!

Ni bora ukubaliane na hali na uwe kijani kweli kweli,,kuwa kama polepole tu!
 
Nadhani swali ni serikali imefanya nini kwenye jimbo la Kawe maana jukumu la kuleta maendeleo ni la serikali na sio la mbunge. Kama katika miaka 10 ya ubunge wa Halima hapajakuwa na maendeleo Kawe inayopaswa kuhojiwa ni serikali na sio mbunge.

Swali kwa Halima ni je katika muda wake huo amewapigania watu wa Kawe na Tanzania ili wapate maisha bora zaidi? Kwa vile chama chake hakikuwa madarakani, wananchi wanapaswa kuwauliza waliokuwa madarakani kwa nini hawakutilia maanani kilio cha mbunge wao?

Kumchagua mtu kwa vile ana pesa za kuchonga barabara ni kujidhalilisha maana mtakuwa mmenunuliwa. Chagueni mtu atakayewapigania ili mtendewe haki kutokana na kodi mnayolipa. Maendeleo sio fadhila, ni haki yenu.
Amandla...
 
Naona umeamua kufanya kampeni kwa Gwajima. Sasa kwa taarifa yako ni kuwa Kunduchi ina maji ya Dawasco na bahati mbaya sana mimi ni mtaalam kwa hiyo maji ya kisima cha chini Kunduchi ni maji ya chumvi sana hivyo naamini hayapo kwa matumizi sasa.

Halafu kutoa pump za maji ya Kisima cha chini Ujerumani nayo ni ishu? Vile vi pamp vipo hata Kariakoo vimejaa tele!

Mkuu emb kuwa na adabu na kichwa chako na ujue kuwa unaleta mada zako kwa wataalam!
 
Naona mlioshindwa kura za maoni mnatekeleza agizo la Mwenyekiti wenu kuwapigia debe waliopita!Hapa unajiwekea kafursa ili ukumbukwe kwenye teuzi kwa kutii maagizo ya mwenyekiti!Huwezi kutenganisha ukada wako na mawazo yako,kwa wanaJF utakuwa mnywa maji ya kijani tu!..
Ask what u will do for Tanzania and not what Tanzania will do for u!! HILI NDIO NDIO MSINGI WA SWALI LA PASCAl Je mdeee Kalifanyia nini jumbo LA Kawe kama sio Kuomba Seikali kila siku pamoja na kwamba serikali inajukumu kuhusu wana kawe Je mbunge Wa wanakawe pasipo Serikali kafanya nini
 
Hivi we P mzima kweli ? Halima mdee ndio anakusanya kodi yaani wakusanye kodi wengine , Halima mdee ndio alete maendeleo ? Kama vile hujui kazi za mbunge ? Kumbe unafanya makusudi , kwahiyo wanakawe unawashauri wachague mcheza sinema za utupu sio ? We si mtu mzima kabisa eti msomi ?
IMG_20200824_163047.jpg
 

Similar Discussions

42 Reactions
Reply
Back
Top Bottom