Je, chatu anaweza kuua jamii ya paka (Simba, Chui, Duma)?

Je, chatu anaweza kuua jamii ya paka (Simba, Chui, Duma)?

Simba nimewaweka kwenye kundi la mabomu sio wanyama wa kawaida maana muda wowote wanafanya chochote na kwa yeyote yule ni mnyama asie na hata chembe ya woga anawinda hadi wale wanyama wenye miba mwili mzima na anajua atashinda tuu ingawaje nimeona wakiferi sana

Hapana mkuu hawa wataalam wa wanyama wanasema simba jike ndiyo mkali zaidi kuliko simba dume! Kwa sababu simba jike ndilo linalowinda na ndilo linalowatafutia chakula familia yake!

Simba dume linaogopwa sababu tu ya muonekana wake na sababu lenyewe ndiyo huunguruma kwa sauti kubwa zaidi! Ila unaambiwa mara mia ukutane na simba dume kuliko jike yaani jike hata likiwa limeshiba halikuachi litakuua hata lipelekee familia yake kitoweo!

We hata katika kuangalia video za wanyama unaonaga masimba dume yanahangaikaga kukimbiza wanyama! Hilo ni jukumu la jike yaani dume kukuua labda uzame kwenye makazi yake!

Wanasema simba ukimkuta ameshiba wala hana shida mnaweza hata mkapishana na asikufanye chochote! Lakini siyo jike aise!
Mkuu hivi tukimpa Simba dume ng'ombe wawili,kisha ukathibitisha amekula mpaka kusaza,ukiambiwa upelekwe ukapishane utakubali?
 
Ukisoma order Carnivora ziko familia nyingi Kama felidae,viveridae,canidae nk

Tukizungumzi neno PAKA tunawagawa kwenye makundi matatu ambayo yako kwenye felidae family ( familia ya mapaka)

Kuna paka wakubwa big cats,mfano Simba,chuimilia, leopards, jaguars, cougars au mountain lions au puma na snow leopard)

Paka wa saizi ya Kati hapa caracal(Mondo),serval cat no

Paka wadogo hapo Kuna small spotted cat, domestic cat, African wild cat nk


Utashangaa Ni kwanini sikumtaja cheetah au Duma(acinonyx jubatus)!!


Huyu hana sifa zote za kuwa paka kwa sababu zifuatazo ndio maana yupo kwenye genus yake mwenye Kama impala alivyotengwa na swala wengine


Sababu Ni zifuatazo:

(1)Anategemea Kasi speed kukamata windo
(2)Yuko active mchana tofauti na paka wengine wanawinda usiku sana
(3)kucha zake hazifunguki na kufunga Kama paka wengine ziko Kama za fisi au ma mbwa
 
Chatu kama moja ya mnyama anayekula wanyama wengine hakuna utata kuwa chatu anaweza mshambulia na kumla Mbuzi, Mbwa, Swala nk.

Swali: je, chatu mkubwa anaweza mshambulia mnyama jamii ya paka akamla mfano Simba, chui na Duma?
Hiyo ni timing kama mdau nyoka na chura
 
Panther ni jamii hata chui nae ni Panther pia
Panther linatokana na neno panthera ambayo Ni genus kwenye felidae family (familia ya mapaka) hapa ukifanya classification iko hivi
Mfano panthera leo ni Simba (panthera imebeba genus na leo lmebeba specie
Panthera leo=Simba
Panthera pardus=chui
Panthera tigress tiger

Panther inamaanisha mapaka makubwa(big cats)

Black panther Ni leopards na jaguars waliopata makosa kidogo ya kimelanin wakawa weusi
 
Kwanza nasikia chatu anatisha usoni na ana macho makali! Kwahiyo ikitokea ukabahatika kujitupa chini kabla hajakuviriga nasikia hakati tamaa kirahisi atakutambaa mwili mzima akifika usoni anakutazama kama mtu!

Sasa ukiweza vumilia ndiyo pona yako maana ana nguvu na ni mzito sasa imagine anakutambaa! Ni kama simba vile wanasema ukimuona jifanye umekufa maana hali mizoga naye nasikia hakati tamaa kirahisi atakunusanusa kuhakikisha kuwa kweli umekufa sasa uvumilivu wako ndiyo pona pona yako!
nimeogopa....uzur dar hakuna chatu[emoji28]

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Kiswahili kina misamiati michache , hivyo ni lugha amabayo haijitoshelezi , hata unapotafsri toka kingereza kwenda Kiswahili ukienda neno Kwa neno lazima usande , sometyme inabid usikilize senetesi nzima ili upate maana kamili ......

Kuna mnyama anaitwa Paka , wote tunamfahamu mana tukisema Paka moja Kwa moja akili inaenda Kwa Paka wa nyumbani , lakni neno Hilo ni mjumuisho wa wanyama wa Aina hyo na sifa hzo kama za Paka wa nyumbani na wala hawafanani kwa kila kitu Ila Wana common characteristics ( watu waliosoma animal science au Tourism watanisaidia) ... Kuna small cats na hapa ndo Paka wetu wa nyumbani anaangukia ( indoor cats) na wengineo kama Paka shume n.k...kuna medium size cats mfano Caracaras ( Kiswahili hapa sjui kinasemaje).... Na kuna big cats , hapa tuna Lion ( Simba ) , Jaguar (Kiswahili kinamis ) , Tiger ( Kiswahili kinamis pia) , Cheetah ( Duma), Leopard ( chui)..... N.k

Mfano wa Big cats
Simba ,( Lion) Chini😋😀
Dk4pPY6Y3BA.jpg



DlCOrbzYTw4-1075x414.jpg


Jaguar
jaguar-1310184-1.jpg

Black jaguar kama wa kwenye movie ya Apocalipto
images (40).jpeg


Tiger
Medium_WW226365.jpg


Leopard ( Chui ) Vanny boy mtu mbaya 😀😀
leopard-africa-safari.jpg


Cheetah (Duma)
encounter-cheetah-in-wild.jpg


cheetah-on-a-hill-namibia-1024x768.jpg


N.k
 
Chatu hupenda kumeza wanyama wakubwa na wadogo. Kawaida hula panya, ndege, mijusi, nguruwe, nyani na hata swala. Lakini chatu wanaweza pia kushambulia jamii ya paka wakubwa, pamoja na simba, ikiwa fursa sahihi itajidhihirisha. Inawezekana kwamba simba anayepambana na chatu porini angeweza kukimbia, au kushinda, lakini inawezekana kwamba wakati mwingine nyoka anaweza kuwa na njia yake.
 
Nenda kagoogle vizuri mkuu.
View attachment 1732176
Jaguar

TigerView attachment 1732184
Huyo Jaguar moto kama pasi, anaruka ndani ya Amazon River anatoka na crocodile/Mamba aina ya Caiman na kakamata kisawasawa, buruta hadi nchi kavu, yuwaenda mla solo, dah acha kabisa huyo.
Anaconda(wa Amazon pia) ndio nao huwaweza Mamba wasize medium pia lakini hii kabila ya mapaka paka hayana mchezo, hayafi kirahisi hivyo sawa na paka wa mtaa tu, jaribu mfungie kwa chumba empty mkiwa nyote mtoke sparring ukiwa na gogo au ufagio, alafu ilitwe mrejesho hapa jf, 🤣🤣🤣
 
Kwa hapa Tanzania tuna rock python,ziko species Kama tatu hivi nimesahau kwenye pythonidae family ziko duniani!
Tukisema chatu tusiweke majoka mengine Kama anakonda kwa sababu anakonda sio python Ni anakonda wapo sijui huko Brazil!!

Ila chatu Ni ambusher anavizia swala la kusema eti ulale chini hakumezi Ni sawa na kumpakia mwenye njaa mkate blue band!

Chatu Ni mla nyama Kama nyoka wote na Hana sumu,na huwa ana Target windo analojua Lina mfit

Unaweza naukibonge wako ukakatiza mbele yake aka mute coz sio saiz yake unless umprovoke Vita vitaanza!


Chatu ana meno mengi membamba yako Kama ndoano ya kuzuia kitu kilichoingia mdomoni kisitoke

Ukilazimisha kutoa utaacha vipande vya nyama huku damu ikikutoka


Achilia mbali ajaku coil bado
 
Kwanza nasikia chatu anatisha usoni na ana macho makali! Kwahiyo ikitokea ukabahatika kujitupa chini kabla hajakuviriga nasikia hakati tamaa kirahisi atakutambaa mwili mzima akifika usoni anakutazama kama mtu!

Sasa ukiweza vumilia ndiyo pona yako maana ana nguvu na ni mzito sasa imagine anakutambaa! Ni kama simba vile wanasema ukimuona jifanye umekufa maana hali mizoga naye nasikia hakati tamaa kirahisi atakunusanusa kuhakikisha kuwa kweli umekufa sasa uvumilivu wako ndiyo pona pona yako!
😂 😂 😂 😂 Chatu huyo basi ulale flat chini, hivi hujipendi kumbe. Chatu atakupa love bites za kutosha hatari hata kama hana sumu lakini maumivu utapata na hushambulia faster kama nyoka wengine wafanyavyo, ndio maana ukitaka kumkamata unashika mkia ndio um'burute, ukienda mbele yake tu, ana strike miguu au hata mikono, hiyo ndio defense technique yake pamoja na hiyo ya ku kuzunguka na kumeza mzima mzima.
 
Jaquar nae ni balaa mzee anazama kwenye maji anatoka na Caiman mpaka ardhini, Simba kilichofanya awe king of the Jungle ni ule ujasiri katika battle field, lakini kiuharisia hata kwa Tiger simba anateseka sana
Upekee mwngne wa Simba dume ni ile tabia yao yakufukuzwa kwenye familia zao na pale wanapokwenda kujitegemea na kuja kuanzsha territory yake mwenyewe huku akikutana na msukomisuko mingi hadi anapokuja kumiliki territory yake mwenyewe huwa sii mchezo ndio maana simba dume anaogopeka sana,hata fisi makeke yao yote wakimuona simba dume wanapoteana
 
Mi nimekaa Sana pori mpaka nikajijenga kisaikolojia kuwa wanyama wanaogopa binadamu kuliko chochote! Mnyama atamdhuru binadamu kujilinda au Kuna ulazima wa kufanya hivyo!

Mwaka juzi simanjiro tulikua wawili shamba na bro wangu tumepiga camp kwenye territory ya chui jike aliyekua breeding na dume mmoja mpaka wamezaa vitoto viwili

Hatuja wahi sikia mmasai analia mbuzi zimeliwa sisi ilikua tukisha kula usiku mabaki ya ugali na mifupa tunaweka nje ya tent asubuhi hatukuti!
Jike anabeba anapelekea watoto nitatuma picha muona Nina device nyingine
 
Back
Top Bottom