Je, chatu anaweza kuua jamii ya paka (Simba, Chui, Duma)?

Je, chatu anaweza kuua jamii ya paka (Simba, Chui, Duma)?

Kuandika rahisi mkuu. Ila ikiwa ndo tukio mubashara panic tu inaweza mrahisishia bwana chatu kukumeza maana unaweza baki unabweka tu bwiii, bwiiii, bwiiii hata hajajiviringisha bado.
Kwanza nasikia chatu anatisha usoni na ana macho makali! Kwahiyo ikitokea ukabahatika kujitupa chini kabla hajakuviriga nasikia hakati tamaa kirahisi atakutambaa mwili mzima akifika usoni anakutazama kama mtu!

Sasa ukiweza vumilia ndiyo pona yako maana ana nguvu na ni mzito sasa imagine anakutambaa! Ni kama simba vile wanasema ukimuona jifanye umekufa maana hali mizoga naye nasikia hakati tamaa kirahisi atakunusanusa kuhakikisha kuwa kweli umekufa sasa uvumilivu wako ndiyo pona pona yako!
 
Wote hao kwa kiswahili ni chui ila lugha ya kiingereza ndiyo imewatofautisha leopard ni chui mwenye madoa (chui madoa) ila tiger ni chui mweye mistari (chui milia)! Tanzania sidhani kama tuna tigers ila leopards tunao ndiyo maana watu wengi hudhani leopard tu ndiyo chui!
Kweli mkuu!
 
Haya mambo aliwezaga Samson tu aise
Alafu sielewi kitu kimoja sawa Samson alikuwa na Nguvu ila rule of the jungle sio suala la kuwa na nguvu tu pia meno na makucha...je Samson angekamatwa shingoni asinguwawa na simba.
 
Ili utumie hiko kiwembe inabidi uwe na mambo yafuatayo
1)Chatu aelewe hitajio lako aache kubana mikono
2)Aache kubana mifuko yako endapo umeweka mfukoni
3)Aache kubana shingo na mapafu ili upate punzi na ufahamu wa kuwaza kiwembe
4)lazima ongee na chatu kwanza kwamba chatu akwambie kesho nakukamata so beba kiwembe
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Wewe umepata wapi hii kitu, Tiger wanapatikana India, Srilanka, Russia na sehemu fulani za asia tu na ni mkubwa sawa na simba au hata kumzidi simba (Siberian Tiger), ngozi yake inayomichirizi myeusi na madoa ya njano. Jaguar yeye anapatikana Amerika ya kusini hasa katika misitu ya Amazon yeye anafanana sana na Chui wa huku Afrika na madoa ya ngozi yake yanafanana sana na yale ya chui ila yeye ni mkubwa kidogo kuliko chui na mdogo kuliko Simba na hapendi kukwea mitini kama chui ila ni muogeleaji mzuri na chakula chake kikuu ni mamba (Caiman crocodile) na Wanyama wa mitoni kama Capebara nk, Waweza kusema Chui na Jaguar wanafanana mno kimaumbile kuliko Jaguar na Tiger, kwa taarifa na habari zaidi ya hao wanyama Google.
Mkuu na kuna wale wengne ni jamii hiihii ya paka lakin wao ni weusi sana huwa wanaitwaje ?
 
Jaguar mweusi uyo
JAGUAR SIO MWEUSI....
Hana tofaoti sana na LEOPARD ila anapatika kwenye misitu ya amazon tuu duniani...wakati leopard anapatikana karibia kila bara hasa Africa ndo wapo wengi wa mfano...
wale unaoona wanawinda kwenye maji hao ni jaguars nadhani mazingira ya misitu ya amazoni imechangia kwenye hiyo tabia
jaguar.jpg
jaguar-v-leopard.jpg
jvle.jpg
3.jpg
 
Kuna clip hii niliwahi kuiangalia kitambo sana, ila kiukweli Tiger ni most aggressive, licha ya kuwa Tiger alikuwa ni mdogo kiumri kwa Lion.
*Lion alikiona cha moto
*Lion alijeruhiwa sana
*Lion alikimbia pambano.

*Tiger kwa vile alikuwa ni mdogo hivyo alikuwa anaishiwa nguvu.

 
Simba wanavuka mto wenye mamba wengi na watata kama huko Zimbabwe mbuga yao moja imezungukwa na maji duma linabaki likiunguruma tuu kuwakinga watoto wakivushwa na jike Simba wanakula bangi sio kuvuta Mkuu... Kruger's game hapo Simba wanaweza kukaa barabarani masaa mengi hata hawajali wanatoka muda wanaotaka wao taratibu...
Mkuuu hyo uwezo wa kuvuka mto mbele ya mamba naona ni hali ya ujasiri aliokuwa nao simba na mamba wanalitambua hilo.kuwa simba sio muoga na ili kumwa attack huwa shughuli pevu,ninachompendea simba ni ile hali ya ujasiri aliokuwa nao ambao baadhi ya wanyama wengne hawana
 
Unachanganya Chui(Leopard) na Duma(Cheetah).

Cheetah ndio mwenye tabia hizo kwasababu katika wanyama walanyama cheetah ndio mdhaifu anazinguliwa hadi na fisi ila sio

Leopard huyo ni Badass anaroho mbaya fisi mwenyewe anamuheshimu hana haja ya kukutisha ukimbie yeye anakuvaa mzimamzima
Kweli mkuu sifa nyingne ya huyo chui (Leopard) hana rafiki na pia hataki urafikii na hafugiki hata kidgo ni atari sana ukikutana nae andika umeumia 😁
 
Back
Top Bottom