Je, chatu anaweza kuua jamii ya paka (Simba, Chui, Duma)?

Je, chatu anaweza kuua jamii ya paka (Simba, Chui, Duma)?

Chatu Ni hatari Sana, akikunasa ukaanza kubabaika badala ya kupambana Basi ujue umekwenda na maji.

Pia unashauriwa ukiona anataka kujizungusha mwilini mwako lala chini ili akose namna ya kujiviringisha, roll down then sepa kwa Kasi ya 4G
Ila mwenye njaa kali anakumeza hivyo hivyo bila kujizungusha,anatafuta kichwa chako kilipo anaanza kumeza. Kuna video moja akimmeza mamba bila kupoteza muda wa kujivinlingisha maana na mamba alikuwa anapambana sana kujinasua,mpaka mamba anaishia tumboni alikuwa bado anacheza cheza.
 
Wewe umepata wapi hii kitu, Tiger wanapatikana India, Srilanka, Russia na sehemu fulani za asia tu na ni mkubwa sawa na simba au hata kumzidi simba (Siberian Tiger), ngozi yake inayomichirizi myeusi na madoa ya njano. Jaguar yeye anapatikana Amerika ya kusini hasa katika misitu ya Amazon yeye anafanana sana na Chui wa huku Afrika na madoa ya ngozi yake yanafanana sana na yale ya chui ila yeye ni mkubwa kidogo kuliko chui na mdogo kuliko Simba na hapendi kukwea mitini kama chui ila ni muogeleaji mzuri na chakula chake kikuu ni mamba (Caiman crocodile) na Wanyama wa mitoni kama Capebara nk, Waweza kusema Chui na Jaguar wanafanana mno kimaumbile kuliko Jaguar na Tiger, kwa taarifa na habari zaidi ya hao wanyama Google.
Naongezea pia kuna mwingine anaitwa Blank Panther,yeye ni mwenyeji wa Amerika ya Kaskazini. Ni mweusi na anafanana sana na Simba.
 
Mkuuu hyo uwezo wa kuvuka mto mbele ya mamba naona ni hali ya ujasiri aliokuwa nao simba na mamba wanalitambua hilo.kuwa simba sio muoga na ili kumwa attack huwa shughuli pevu,ninachompendea simba ni ile hali ya ujasiri aliokuwa nao ambao baadhi ya wanyama wengne hawana
Jaquar nae ni balaa mzee anazama kwenye maji anatoka na Caiman mpaka ardhini, Simba kilichofanya awe king of the Jungle ni ule ujasiri katika battle field, lakini kiuharisia hata kwa Tiger simba anateseka sana
 
Mi ndo maana huwa nawapenda sana chui. Ni wanyama wenye akili sana ndo maana ndo wanyama wanaoishi raha msatarehe mwituni. Ni wepesi kupigana kwa akili na kujikamua kwa maadui ambao wanaazidi nguvu kama Simba na fisi.

Halafu chatu wana minofu mikubwa kama sangala. Hapo chui atakuwa anakula tu kama sangala wa kukaangwa.
😋😋😋
 
chatu hutumia kuua kwa kitu inaitwa(coiling)yaan ndani sekunde anakuwa ameshamzunguka mnyama yoyote na kumbana hadi ashindwe kupumua!!nadhani chatu na wanyama kama chui au simba wakikutana wataogopana sababu wote wana technic sawa
Sijawahi ona lakin..kitheory Ni rahisi lakin kuvitendo sio rahisi
 
Dianosor wa ardhini mkubwa kiumbo ni yule mwenye shingo ndefu, So Trex na Spanous ambao ndio Apex Predate Size ya mwili wao ni mkubwa kuliko Tembo ila sio ukubwa wa kuweza kummeza Tembo atamla kwa vipande vipande mpaka aishe Kwanzaa hawana sifa ya kumeza wanamega na kutafuna...
Bora walikufa wakaisha wote maana wangemaliza viumbe wote. Hivi ilikuwaje wakaisha kabisa?
 
Haiwezekani mbegu za kule zikaletwa huku wakazaana na wa huku?
Mhh huko vijiji vipo karibu na wananchi si hatari sana nilipokua naanza kupita chirundu hapo Zimbabwe jamaa walinisihi nisijaribu kutoka nje kuanzia kona ya Kariba mpaka chirundu yenyewe kuna Simba wakali sana na nikipita nilikua nasikia majanga tuu kuwa wapo wazungu wawili wameuawa na kuliwa maana wenzetu wanaambiwa harafu wakifika mbele wanapaki gari na kusogea porini kidogo aah hakuna anaerudi huko ingawaje matangazo yapo mengi hiyo bara bara na pia upande wa Hwange hapo pana Simba hatari sana upande wa Botswana tembo wao ndio wakubwa na wengine wakali ila Simba sio wakali wakati huo huo tembo wa Zimbabwe upande wa Kariba wanapishana tuu na Raia ...
 
Back
Top Bottom