Japo Bunge Limeridhia, DPW Kuendesha Bandari Zetu, ni Makubaliano Tu, Tukithibisha Kuna Matatizo, Tunarekebisha Mkataba wa HGA, Kazi Nzuri Iendelee!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,504
113,618
Wanabodi,
Kama kawaida yangu, kila nipatapo fursa, huja na makala zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa" kuhusu jambo lolote lenye maslahi makubwa kwa taifa letu liwe ni la kisiasa, kiuchumi au kijamii.

Mada ya leo ni kuhusu makubaliano ya kiserikali, IGA ambapo Bunge letu tukufu, limeridhia kitutusa kwa kura ya gulio ya "ndiyo...!", makubaliano hayo ya IGA kati ya Serikali yetu na kampuni ya DPW ya Mwarabu wa Dubai, kutuendeshea Bandari zetu, naomba kuwapooza moyo na kuwafariji wana maslahi ya kweli ya taifa, kuwa hata baada ya kuridhiwa na yale matutusa ya Bunge letu, ikithibitika pasipo shaka kuwa kuna mambo bado hayajakaa sawa, makubaliano hayo yanarekebishwa kabla ya kuingia mkataba wa HGA na serikali yetu, hivyo Tanzania kufaidika na mwekezaji kufaidika kwa kufikia a win win situation, ili kazi nzuri ya Mama Samia iendelee bila madoadoa!.

Kupitisha kitutusa maana yake ni unapewa lidude, ndani yake kuna mambo ya ajabu yanayokwenda kinyume cha sheria zetu, halafu wewe unalipitisha lidude hilo vile vile lilivyo bila any reservations.

Angalizo la Uzalendo
Watanzania ni watu wa kuridhika kirahisi na sio watu wa kuhoji, hivyo unapotokea mtu kuhoji baadhi ya mambo makubwa kama haya, na kufuatia kuna baadhi ya watu wameupinga mpango huu, hivyo unawekwa kwenye kundi la wapinzani, na ukaonekana sio mzalendo, hivyo naomba nianze kwa declaration ya uzalendo na kusisitiza mimi sio mpinzani wa mpango huu, na bandiko hili limetanguliwa na mabandiko yangu matatu kuusuport mpango huu
1- Hakuna Ubaya Wowote kwa Mtu Yoyote, Taasisi Yoyote, Nchi Yoyote Kusaidiwa Pale Inaposhindwa, Muhimu ni Kuwa Makini Tusipigwe!. Je DPW Tunapigwa?.

2- Wabunge Wetu, Macho ya Watanzania Wote Leo ni Kwenu!. Maslahi ya Taifa Mbele!. Tuwaogope Kama Ukoma Muflis Hawa!, Kama Huwezi, ni Lazima Usaidiwe Tuu!

3- Watanzania tujifunze kukubali kuna vitu hatuwezi, tunaposhindwa tukubali kusaidiwa au tukomae? Baada ya Bandari ni ATCL na SGR au Tusubirie? hivyo nawaomba sana wasomaji wangu, msiwe na wasiwasi kabisa kuhusu uzalendo wangu kwa nchi yangu!.

Kuna watu wana support hatua hiyo kwa hoja za msingi, kuwa DP World ni kampuni kubwa na ina uwezo mkubwa, inaendesha kwa ufanisi mkubwa, Bandari nyingi duniani, hivyo itatusaidia sana kuboresha uendeshaji wa Bandari yetu ya Dar es Salaam, Yes!. Na kuna wanaopinga wakiwaita DP World ni matapeli, kufuatia kesi na migogoro mingi mahali pengi ambapo DP World wana operates, hivyo kitendo cha Bunge letu kuridhia hiyo IGA ya DP World hivyo hivyo ilivyo, licha ya mapungufu na makando kando yake, bila kuifanyia a due diligence report, wala any reservations, kumewafanya wachoke na kudhani, it's over, it's the end of the road kwa suala hili,. naomba kuwapa faraja na kuwatia moyo kuwa it's not the end!, it's not over yet until it's over!.

Hiyo HGA ni makubaliano tuu, MoU na sio mkataba, yaani ni an agreement na sio contract. Kila mkataba ni agreement, lakini sio kila agreement ni contract, yaani mkataba, mfano mzuri ni muungano wa Tanganyika na Zanzibar kuunda Tanzania, ni makubaliano tuu na sio mkataba, mkifika mahali mkashindwa kuelewana, mnagawana tuu fito, kila mtu anasepa kivyake Je, Wajua Kuwa Tanzania Hatuna Mkataba wa Muungano?. Kilichopo ni Makubaliano Tuu ya Muungano?!.

Hivyo kile Bunge letu lilichoridhia, ni agreement tuu, tukiithibitishia serikali yetu, hawa DP World, pamoja na uzuri wao wote, pamoja na uwezo wao mkubwa wa kuendesha Bandari kibao, lakini ni matapeli na wana matatizo lukuki, hivyo serikali yetu iwe makini sana kabla ya kusaini HGA, na utepeli wao, ukiwekwa wazi hadharani peupe, kila mwenye macho aone, tutaisaidia sana serikali yetu, tutamsaidia sana Rais wetu Samia na kulisaidia taifa letu Tanzania tusiingizwe tena mkenge na Mwarabu wa Dubai kama alivyofanywa Chief Mangungo wa Msowero, hivyo serikali yetu, viongozi wetu na Bunge letu kuridhia fasta fasta kwasababu tuu, Mwarabu wa Dubai ni mtu Rahim, mkarimu, amemkirimu Mama yetu kuipaisha bure Tanzania kwenye Expo Dubai, akawakirimu waserikali wetu, kwa trips za Dubai, akawakirimu waheshimiwa wabunge wetu kwa trips za Dubai, na kuwakirimu waandishi wetu wa habari na media zetu kwa trips za Dubai.

Japo Rais wetu, Mama Samia, ana nia njema ya kweli na ya dhati kulisaidia taifa letu, lakini anapokutana na matapeli wa kimataifa wakamuingiza kingi, mkenge, sisi watu wa Mhimili wa Nne, the media, tuna wajibu wa kulisaidia taifa letu kwa kuonyesha madhaifu ya mkataba huu, kuangazia makosa ya kisheria ya hii IGA, na kuzama deep kuibua utepeli wa DPW uko wapi, kisha serikali yetu ikiamua kuendelea na HGA ya Mwarabu wa Dubai licha ya IGA yenye mapungufu, hivyo hivyo ilivyo, sisi watu wa media, tutakuwa na a clear conscious kuwa angalau tumetimiza wajibu wetu, tumeieleza serikali yetu madhaifu yetu na jinsi inavyotaka kuingizwa mkenge na kutapeliwa na DPW, hivyo vipengele vya mkataba wa HGA viboreshwe ili kuzuia tusitapeliwe, na kazi nzuri ya Mama Samia iendelee!.

Kwa vile mimi licha ya kuwa ni mwandishi tuu wa habari wa kujitegemea kwa kujitolea, mimi pia ni mwanasheria na wakili wa kujitegemea, kwa kujitolea kutetea bure haki kwa wasio na uwezo, hivyo ninawaletea makubaliano hayo na kuwachambulia kisheria kwa kuwaonyesha mapungufu makubwa ya kisheria ya hii IGA na jinsi tunavyotaka kutapeliwa mchana kweupe!.
  1. Utapeli wa kwanza mkubwa, ni hakuna mtu yoyote kati yetu aliyefanya a due diligence report ya DP World, tukaletewa, mfano mzuri ni hawa jamaa walipewa kuendesha Bandari 6 za Marekani, Bunge la Congress la Marekani lilawakatalia!. Wenzetu walipiga kura mmoja mmoja kwa majina, sisi Bunge letu limepitisha kitutusa kwa kura za gulio!.
  2. Katiba ndio sheria Mama, hakuna aliye juu ya katiba, Bunge, Serikali na Mahakama ziko chini ya katiba, hivyo kwa mujibu wa katiba yetu na sheria zetu, serikali yetu haiwezi kuingia mkataba wowote wa kimataifa unaokwenda kinyume cha katiba yetu ama sheria zetu. Hii IGA ya DPW na Bandari zetu it's illegal kwasababu inakwenda kinyume cha sheria zetu za rasilimali za taifa.
  3. Baada ya serikali yetu kuingia kwenye an illegal agreement, Bunge letu lilipaswa kuiambia serikali yetu kuhusu illegality hii, hivyo kuipitisha IGA ya DPW na Bandari with reservations kuwa it will come into operations baada ya hiyo illegality kuondolewa!, lakini Bunge letu Tukufu limeridhia makubaliano hayo kitutusa as if mule Bungeni yamejaa matutusa matupu!.
  4. Ile mwaka 2000 mimi nilipoomba kwenda Bungeni, nilisema wazi, nataka kwenda Bungeni kulisaidia Bunge letu, kuisaidia serikali yetu na kuisaidia nchi yetu
    View: https://youtu.be/Qr6j25jFGyI?feature=shared, watu kama sisi tungekupo mule mjengoni, tusingekubali madudu ya ajabu kama haya yapite kitutusa without any reservations!.
  5. Kwa mujibu wa katiba yetu na sheria zetu, an illegal contract ni void ab initio, na sio voidable kusema itarekebishwa!, ni hairekebishiki.
  6. The illegality part ni kile kifungu cha kutatua migogoro nje ya nchi. Sheria yetu ya rasilimali za taifa inasema wazi, mikataba yote ya rasilimali za taifa, itaingiwa kwa sheria za Tanzania na migogoro yote itaamuliwa Tanzania na Mahakama za Tanzania. Hivyo serikali yetu haiwezi kuingia mkataba au makubaliano yoyote ya kimataifa yenye kipengele cha kutatua migogoro nje ya nchi kwa sheria za nchi nyingine yoyote!.
  7. Tulipaswa kwanza tubadili sheria yetu ya rasilimali za taifa kuruhusu migogoro kutatuliwa nje ya nchi ndipo IGA ikasainiwa!.
  8. Tunaelezwa ni DPW ni Governmental Organisation, wakati sii kweli, japo DPW inamilikiwa na serikali ya Dubai, lakini it's a private company!. Serikali yetu haiwezi kuingia an international Treaty na a private company!. Kabla ya kuingia mkataba wowote, lazima kwanza kufanyike kitu kinachoitwa a due diligence process na kutolewa a due diligence report. Hili halikufanyika hivyo serikali yetu kujikuta inaingia mkataba wa kimataifa na parties to contract which has no capacity to contract an international treaty hivyo ku vitiate makubaliano kugeuka void hivyo makubaliano hayo yanakuwa null and void ab initio!. NB. Mtu au kampuni, taasisi yoyote ya Kitaifa au kimataifa, inaweza kuingia mkataba na mtu, kampuni, serikali lakini sio international Treaty, ni international contracts or agreements za non state parties.
  9. Mkataba wa IGA na HGA wa state parties inaingiwa kati ya serikali na serikali za nchi na nchi, hivyo ukisoma documents za makubaliano utaona ni kati ya serikali ya Tanzania na serikali ya UAE, lakini signatories kwa serikali ya Tanzania ni serikali kweli, lakini kwa serikali ya UAE, signatories ni Mwarabu wa Dubai wa DP World na sio serikali ya UAE, wala serikali ya Dubai!, japo kwenye mkataba wameandika serikali ya Dubai, Dubai is not a state, hivyo hapa kunauwezekano tunatapeliwa!. Serikali yetu inaingizwa mkenge kuingia mkataba na a private company disguised as a government of UAE kumbe ni kampuni binafsi!.
    1686460927642.png
  10. Mkataba Kati ya serikali ya Tanzania na Dubai ni batili kwenye sheria za kimataifa. Maana Dubai sio nchi, a sovereign state kama ilivyo Tanzania, Dubai hapa inajitambulisha kama a State Party, Dubai is not a state hivyo haiwezi kuwa a state party, it has no the capacity to transact as an international state IGA, haiwezi kuingia mikataba ya kimataifa na nchi na nchi!, inaweza kuingia mkataba wa kimataifa wa nchi na kampuni au kampuni na taasisi kama ilivyoingia na mamlaka ya Bandari, taasisi kwa taasisi, kama ilivyofanya hapa
    1686461228426.png
    ambapo DP World iliingia mkataba na Mamlaka ya Bandari TPA, mkataba ambao Rais Samia aliushuhudia ukisainiwa kule Dubai during Expo Dubai.
  11. Sasa kampuni hii ya DP World iliyoingia mkataba na mamlaka ya Bandari, sasa inajigeuza nchi, sovereign state of Dubai!, imeingia mkataba wa kimataifa wa state party na serikali yetu!, huku ni kututapeli!. Dubai is not a sovereign state, it's not a nation na nchi isiyo na sovereignty!. DP World is not a state, it's a private company!, hapa imejigeuza ni nchi!. Huu sio utapeli?.
    1686466691966.png
  12. Mikataba ya kimataifa ya state parties, inaingiwa kati ya nchi na nchi, hapa nchi inayotambuliwa ni Falme ya Kiarabu, UAE, ndio inayotambulika kwenye sheria za kimataifa as a state, na sio Dubai ambayo ni sehemu ya UAE, sio state, hivyo hapa kuna utapeli!. Due diligence ingefanyika, hili lingeonekana!.
  13. Status ya Dubai kwe UAE ni sawa na status ya Zanzibar ndani ya JMT, Zanzibar has no capacity to transact an international treaty kwasababu Zanzibar sio sovereign state, haina sovereignty. Dubai pia sio sovereign, hivyo mikataba yote ya kimataifa ya Zanzibar, inaingiwa na JMT kwaniaba ya Zanzibar, IGA na HGA inapaswa kuingiwa kati ya Tanzania na UAE na sio Tanzania na Dubai!.
  14. DPW ni kampuni kama inavyoonyesha hapa
    1686466821809.png
  15. Wanasheria wanapoamua kufanya magumashi ya kisheria, wanakuzuga kwa maneno ya kweli kwenye mkataba, mfano hapa Dubai inatambulishwa kama nchi,
    1686466895812.png
    lakini mkataba wetu hii iliyoandikwa kama nchi, sio nchi kweli bali ni kampuni ya DPW!.
  16. Kwa vile kwa upande wetu ni serikali yetu, ili kuonyesha IGA ni kati ya serikali mbili, hapa wameitaja kampuni ya kiserikali ili kuiserikalisha kampuni binafsi ya DPW kuwa ni serikali
    1686466969407.png
  17. Hivyo mikataba ya HGA utaokuja kuingiwa na serikali yetu, sio mkataba wa kimataifa wa kiserikali kati ya serikali yetu na serikali ya UAE, lakini hakuna chochote cha UAE bali kampuni binafsi ya DPW iliyoserikalishwa na kujifanya ni serikali!.
    1686467041823.png
    1686467116175.png
  18. Kwa vile mikataba ya kimataifa inahusisha state parties, HGA inayokwenda kuingiwa ni HGA kati ya nchi ya Tanzania ambayo ni state na kuingia na DPW iliyo ji stetisha kama a state ambapo huu pia sio utapeli?.
    1686467223681.png
  19. Kwa Tanzania mamlaka yote ya nchi, mtu yoyote ili asaini mkataba wa kimataifa wa kuiingiza nchi, anapaswa apewe the Power of Attorney na Rais wa JMT. Hii hapa chini ni POA ya Rais Samia kumpa mamlaka Prof. Mbarawa kuingia huo mkataba kwa niaba ya Tanzania,
    1686466333664.png
    POA hii kisheria ni defective, kwasababu japo imesainiwa na Rais Samia, lakini haina muhuri wa rais, au muhuri wa serikali, hizi documents za kisheria ikisemwa POA must be signed and stamped by the official seal, lazima iwe hivyo, not otherwise!, kama walivyofanya hawa counter parts hapa chini.
    1686466491072.png
  20. Ili serikali yetu iingie kwenye mkataba wa kihalali wa kimataifa na taasisi ambayo sio nchi, kulitakiwa kuwepo POA toka UAE kuipa mamlaka Dubai kuingia mkataba wa kimataifa kwa niaba ya UAE, then ndipo Emirate wa Dubai angeweza kuwapa POA DPW kujigeuza ni nchi.
  21. Hapa Prof. Mbarawa almanusura angekosea kusaini
    1686466226745.png
  22. Hakuna ubaya wowote kwa kampuni yoyote kuingia mkataba na serikali under PPP, lakini hili la kampuni binafsi iliyo serikalishwa kuingia an International treaty na serikali yetu, halikakaa vizuri!.
  23. Jambo jingine, kuna kipengele cha kuizuia nchi isiendeleze Bandari nyingine, hivyo kuiweka mashakani Bandari ya Bagamoyo, hili halikubaliki hata kidogo!.

Hitimisho
Kwa vile Rais Samia ana nia njema ya dhati kuisaidia nchi yetu, wasaidizi wa rais na sisi Watanzania wengine wote tuna wajibu wa kumsaidia rais wetu na kulisaidia taifa letu na huu ndio uzalendo wa kweli.

Paskali.
 
Attachments

  • 1686460858169.png
    1686460858169.png
    15.4 KB · Views: 16
1. Hakuna la maana ikiwa maridhiano mikataba haitowekwa wazi na iwe na kikomo.
2. Maridhiano na mikataba iandikwe kwa kiswahili ili namimi huku ibologelo nisome na kuelewa.
3. Mikataba na marishiano iundiwe tume huru itakayo ipitia kabla ya kuipitisha "kwa maslahi ya taifa.
4. Dp World ichunguzwe kwa tuhuma za kufukuzwa nchi zingine ili tufanye marekebisho isio ya kinyonyaji.
 
Tatizo hayo unayoita makubaliano inaonekana yameshaanza kutekelezwa since October 2022, kwa maana nyingine hapo ni kwamba, bunge la CCM jana limeridhia makubaliano ambayo tayari yalishaanza kutekelezwa, hapo ukitazama kwa makini utaona kabisa bunge halikuwa na ujanja wa kupinga kitu ambacho kimesharidhiwa na serikali ya mwenyekiti wao Samia.

Hapa kwa ufupi niseme kwamba, bunge limetumika kuhalalisha uhuni uliofanywa na serikali, nalo kwa kutokujitambua, likabariki uhuni huo, hivyo hapo ni kama serikali inafurahi imempata mjinga mwingine wa kufa nae, huku Spika Tulia akiwa ndie kiongozi wa hao wajinga.

Nachotaka hayo makubaliano/mkataba yavunjwe, naona kabisa kuna vitu vingi ambavyo havina haki kwetu ajabu tumeweka saini kwenye yale makubaliano, na inapoonekana Mbarawa mzanzibari, na Samia mzanzibari wote wamehusika, ndio inaumiza moyo zaidi, hawa wawili wana nia mbaya na wabara, ukweli usemwe tu.
 
Hivi wewe kazi yako katika kitengo ni KUWA SPIN DOCTOR?

Hebu acha kujaribu kutuliza Hasira zetu. Unazidi kutuumiza!
Hawa waandishi wa magazeti wameahidiwa fedha iwapo watapigia Debe mkataba wa kuuza nchi!
These mercenaries are now busy spinning to facilitate the sale of our country kama Mangungo wa Mvomelo alivyouza kwa shanga enzi hizo za utumwa!
 
Makubaliano yalikuwa kwenye memorandum of understanding, vyote vinavyofata baada ya hapo ni mkataba halali na sio makubaliano. Ila yote kwa yote na cha msingi zaidi ni vipengele vilivyopo ndani ya mkataba, je ni rafiki kwa kila mmoja au ni kwa upande mmojawapo???

Na je vipi ukomo wake??, Na je mmoja akitaka kujitoa je??? Na kadhalika na kadhalika na hapo ndipo wengi tunapopatwa na mashaka.
 
Wanabodi,
Bunge letu tukufu, limeridhia makubaliano ya IGA kati ya Serikali ya UAE na Tanzania, kampuni ya DP World ya Mwarabu wa Dubai, kutuendeshea Bandari zetu.

Kuna watu wana support hatua hiyo kwa hoja za msingi, kuwa DP World ni kampuni kubwa na ina uwezo mkubwa hivyo itatusaidia sana. Na kuna wanaopinga wakiwaita DP World ni matapeli, hivyo kitendo cha Bunge letu kuridhia hiyo IGA, kumewafanya wachoke na kudhani, it's the end of the road. Naomba kuwapa faraja kuwa it's not the end!.

Hiyo HGA ni makubaliano tuu na sio mkataba, yaani ni an agreement na sio contract. Kila mkataba ni agreement, lakini sio kila agreement ni mkataba, mfano mzuri ni muungano wa Tanganyika na Zanzibar kuunda Tanzania, ni makubaliano tuu na sio mkataba, mkifika mahali mkashindwa kuelewana, mnagawana tuu fito, kila mtu anasepa kivyake Je, Wajua Kuwa Tanzania Hatuna Mkataba wa Muungano?. Kilichopo ni Makubaliano Tuu ya Muungano?!.

Hivyo kile Bunge letu lilichoridhia, ni agreement tuu, tukiithibitishia serikali yetu, hawa DP World, pamoja na uzuri wao wote, pamoja na uwezo wao mkubwa wa kuendesha Bandari kibao, lakini ni matapeli na wana matatizo lukuki, hivyo serikali yetu iwe makini sana kabla ya kusaini HGA, na utepeli wao, ukiwekwa wazi peupe, tutaisaidia sana serikali yetu na kulisaidia taifa letu tusiingizwe mkenge na Mwarabu wa Dubai kwasababu tuu ni mtu mkarimu, amemkirimu Mama yetu kuipaisha bure Tanzania kwenye expo Dubai, akawakirimu waserikali wetu, kwa trips za Dubai, akawakirimu waheshimiwa wabunge wetu kwa trips za Dubai, na kuwakirimu media na waandishi wa habari wetu kwa trips za Dubai.

Japo Rais wetu, Mama Samia, ana nia ya kweli na ya dhati kulisaidia taifa letu, lakini anapokutana na matapeli wa kimataifa wakamuingiza mkenge, sisi watu wa Mhimili wa Nne, the media, tuna wajibu wa kulisaidia taifa letu kwa kuonyesha utepeli uko wapi, kisha serikali yetu ikiamua kuendelea na HGA ya Mwarabu wa Dubai, sisi watu wa media, tutakuwa na a clear conscious kuwa tumetimiza wajibu wetu, tumeieleza serikali yetu inavyotaka kuingizwa mkenge.

Kwa vile mimi licha ya kuwa ni mwandishi tuu wa habari wa kujitegemea kwa kujitolea, mimi pia ni mwanasheria na wakili wa kujitegemea, kwa kujitolea kutetea haki bure, hivyo nitawaletea makubaliano hayo na kuwachambulia kuwaonyesha jinsi tunavyotaka kutapeliwa mchana kweupe.

Utapeli wa kwanza mkubwa, ni hakuna mtu yoyote kati yetu aliyefanya a due diligence report ya DP World, tunaelezwa ni Governmental Organisation, wakati sii kweli, it's a private company!.

Mkataba wa IGA na HGA inaingiwa kati ya serikali na serikali, hivyo ukisoma documents za makubaliano utaona ni kati ya serikali ya Tanzania na serikali ya UAE, lakini signatories kwa serikali ya Tanzania ni serikali kweli, lakini kwa serikali ya UAE, signatories ni Mwarabu wa Dubai wa DP World na sio serikali ya UAE hivyo hapa tunatapeliwa!, serikali yetu inaingizwa mkenge kuingia mkataba na a private company disguised as a government of UAE kumbe ni kampuni binafsi!.

Jambo la pili, kuna kipengele cha kuizuia nchi isiendeleze Bandari nyingine, hivyo kuiweka mashakani Bandari ya Bagamoyo, hili halikubaliki hata kidogo!.

Kwavile saa hizi ni usiku mkubwa, Joni Mtembezi ananisisitiza nitembee tembee nae hivyo nitamalizia kesho.

Paskali.
Nasubiri ufafanuzi wako wa Ibara zenye utata, ikizingatiwa kuwa IGA ndio utakuwa Mkataba mama (referal agreement) wakati wa kuandaa HGAs.

Je, wewe umefanikiwa kuona na kusoma MoU kati ya TPA na DP World, kwa maana "boss" wa TPA ameitetea sana DPW?
 
CCM na matakataka yake yote ni ya kuifukuzilia mbali, ili tupate manufaa ya nchi yetu ni lazima CCM ing'olewe tu, uzuri wa bahati kwa kuiingiza nchi katika mikataba/makubaliano hayo na Kampuni ya kitapeli ya kimataifa yenyewe imejipalia makaa ya moto--- hakuna kuremba tena CCM must go as its fellow freedom fighter sister parties.
 
Wanabodi,
Bunge letu tukufu, limeridhia makubaliano ya IGA kati ya Serikali ya UAE na Tanzania, kampuni ya DP World ya Mwarabu wa Dubai, kutuendeshea Bandari zetu.

Kuna watu wana support hatua hiyo kwa hoja za msingi, kuwa DP World ni kampuni kubwa na ina uwezo mkubwa hivyo itatusaidia sana. Na kuna wanaopinga wakiwaita DP World ni matapeli, hivyo kitendo cha Bunge letu kuridhia hiyo IGA, kumewafanya wachoke na kudhani, it's the end of the road. Naomba kuwapa faraja kuwa it's not the end!.

Hiyo HGA ni makubaliano tuu na sio mkataba, yaani ni an agreement na sio contract. Kila mkataba ni agreement, lakini sio kila agreement ni mkataba, mfano mzuri ni muungano wa Tanganyika na Zanzibar kuunda Tanzania, ni makubaliano tuu na sio mkataba, mkifika mahali mkashindwa kuelewana, mnagawana tuu fito, kila mtu anasepa kivyake Je, Wajua Kuwa Tanzania Hatuna Mkataba wa Muungano?. Kilichopo ni Makubaliano Tuu ya Muungano?!.

Hivyo kile Bunge letu lilichoridhia, ni agreement tuu, tukiithibitishia serikali yetu, hawa DP World, pamoja na uzuri wao wote, pamoja na uwezo wao mkubwa wa kuendesha Bandari kibao, lakini ni matapeli na wana matatizo lukuki, hivyo serikali yetu iwe makini sana kabla ya kusaini HGA, na utepeli wao, ukiwekwa wazi peupe, tutaisaidia sana serikali yetu na kulisaidia taifa letu tusiingizwe mkenge na Mwarabu wa Dubai kwasababu tuu ni mtu mkarimu, amemkirimu Mama yetu kuipaisha bure Tanzania kwenye expo Dubai, akawakirimu waserikali wetu, kwa trips za Dubai, akawakirimu waheshimiwa wabunge wetu kwa trips za Dubai, na kuwakirimu media na waandishi wa habari wetu kwa trips za Dubai.

Japo Rais wetu, Mama Samia, ana nia ya kweli na ya dhati kulisaidia taifa letu, lakini anapokutana na matapeli wa kimataifa wakamuingiza mkenge, sisi watu wa Mhimili wa Nne, the media, tuna wajibu wa kulisaidia taifa letu kwa kuonyesha utepeli uko wapi, kisha serikali yetu ikiamua kuendelea na HGA ya Mwarabu wa Dubai, sisi watu wa media, tutakuwa na a clear conscious kuwa tumetimiza wajibu wetu, tumeieleza serikali yetu inavyotaka kuingizwa mkenge.

Kwa vile mimi licha ya kuwa ni mwandishi tuu wa habari wa kujitegemea kwa kujitolea, mimi pia ni mwanasheria na wakili wa kujitegemea, kwa kujitolea kutetea haki bure, hivyo nitawaletea makubaliano hayo na kuwachambulia kuwaonyesha jinsi tunavyotaka kutapeliwa mchana kweupe.

Utapeli wa kwanza mkubwa, ni hakuna mtu yoyote kati yetu aliyefanya a due diligence report ya DP World, tunaelezwa ni Governmental Organisation, wakati sii kweli, it's a private company!.

Mkataba wa IGA na HGA inaingiwa kati ya serikali na serikali, hivyo ukisoma documents za makubaliano utaona ni kati ya serikali ya Tanzania na serikali ya UAE, lakini signatories kwa serikali ya Tanzania ni serikali kweli, lakini kwa serikali ya UAE, signatories ni Mwarabu wa Dubai wa DP World na sio serikali ya UAE hivyo hapa tunatapeliwa!, serikali yetu inaingizwa mkenge kuingia mkataba na a private company disguised as a government of UAE kumbe ni kampuni binafsi!.

Jambo la pili, kuna kipengele cha kuizuia nchi isiendeleze Bandari nyingine, hivyo kuiweka mashakani Bandari ya Bagamoyo, hili halikubaliki hata kidogo!.

Kwavile saa hizi ni usiku mkubwa, Joni Mtembezi ananisisitiza nitembee tembee nae hivyo nitamalizia kesho.

Paskali.
Nadhani utakuwa unaota wewe.
Hiyo ndio imekwisha.
Hakuna tena cha kugeuza mambo.
Liwe jua au mvua hakuna kipya.
Watanganyika mmeshapigwa, tena mmepigwa kavu kavu, mchana kweupeee.

CCM Oyeeeee!
 
Back
Top Bottom