January Makamba anatakiwa aitwe na kuhojiwa na chama chake kuhusiani na kauli zake zinazohusu uchaguzi wa 2020

Mr Dudumizi

JF-Expert Member
Sep 9, 2020
6,860
12,293
Habari zenu wanaJF wenzangu,

Huyu mtu baada ya kushindwa kuiongoza wizara aliyopewa bure kutokana umaarufu wa baba yake huko chamani, na pia kushindwa kuisimamia vyema wizara ya mambo ya nje aliyohamishiwa, sasa kaamua kuja na mkakati wa kumchafua hayati Magufuli kwa lengo la kutrend katika mitandao ya kijamii, akifikiri kuwa style hiyo ya kumchafua hayati Magufuli itamsaidia kutoboa katika kinyang'anyiro cha uchaguzi cha mwaka 2025.

Mimi nafikiri huyu mtu hafai kuendelea kuwa chamani wala wizarani, maana ni mnafiki, mpenda majungu na muendekeza siasa za majitaka zilizopitwa na wakati.

Raisi Samia akiendelea kumfuga huyo mtanga katika chama na baraza lake la mawaziri basi ajue kwamba kuna siku na yeye atakuja kusemwa kama anavyosemwa mwenzake alietangulia mbele ya haki.

Soma:
- Januari Makamba adai uchaguzi wa 2020 ulitugawa, watu walifungwa, walinyang'anywa pesa, na waliharibiwa biashara zao
 
Kwani uongo.
Kwa ambao hamkuwepo na msio na kumbukumbu, uchaguzi wa 2020 haukua wa haki.
Alivyosema January Ni ukweli mtupu.
Lakini pia January hajashindwa kuendesha wizara na Wala hakupata uwaziri kwa sababu ya jina la mzee wake.
Tatu, jifunze kuwa na adabu unapowasema waheshimiwa Kama Makamba senior.
 
Habari zenu wanaJF wenzangu,

Huyu mtu baada ya kushindwa kuiongoza wizara aliyopewa bure kutokana umaarufu wa baba yake huko chamani, na pia kushindwa kuisimamia vyema wizara ya mambo ya nje aliyohamishiwa, sasa kaamua kuja na mkakati wa kumchafua hayati Magufuli kwa lengo la kutrend katika mitandao ya kijamii, akifikiri kuwa style hiyo ya kumchafua hayati Magufuli itamsaidia kutoboa katika kinyang'anyiro cha uchaguzi cha mwaka 2025.

Mimi nafikiri huyu mtu hafai kuendelea kuwa chamani wala wizarani, maana ni mnafiki, mpenda majungu na muendekeza siasa za majitaka zilizopitwa na wakati. Raisi Samia akiendelea kumfuga huyo mtanga katika chama na baraza lake la mawaziri basi ajue kwamba kuna siku na yeye atakuja kusemwa kama anavyosemwa mwenzake alietangulia mbele ya haki.
Kuna uongo kwenye maneno yake?
 
Alivyosema January Ni ukweli mtupu.
Weka ushahidi sio utuletee maneno matupu.
Lakini pia January hajashindwa kuendesha wizara na Wala hakupata uwaziri kwa sababu ya jina la mzee wake.
Bila baba yake huyo jamaa yenu asingekuwepo hapo alipo leo, na pia niambie kitu gani cha maana alikifanya pale wizarani?
Tatu, jifunze kuwa na adabu unapowasema waheshimiwa Kama Makamba senior.
Yani atuharibie nchi alafu tusimseme, yeye amekuwa nani nchi hata. Hata raisi anasemwa, sembuse yeye mnafki.
 
Back
Top Bottom