Tumekuwa tukisikia kauli mbalimbali za viongozi wa CCM na serikali wakiwemo mawaziri kuwa uchaguzi ule wa 2020 chini ya Magufuli haukuwa wa kidemokrasia wala haki.
Tunashukuru kwa taarifa. Swala ina maana kuanzia viongozi wote waliochaguliwa uchaguzi ule hawakuingia kihalali kuanzia juu,wabunge hadi Serikali za Mitaa.
Kuzitendea haki nafsi zao na watanzania kwa nini viongozi wote wako madarakani toka hiyo 2020 hawajiuzulu wote kuanzia juu, bunge hadi serikali za mitaa ili uitishwe uchaguzi mpya huru na haki na wa kidemokrasia ili kuwatendea haki watanzania wasiendekee kuongozwa na viongozi waliopita kupitia mfumo usio wa haki na kidemokrasia mara tu baada ya kugundua kuwa wameingizwa kinyume xha haki na demokrasia?
Kwa nini bado wamekalia viti wanawakebehi watanzania kuwa ndiyo uchaguzi haukuwa huru na haki na haukuwa wa kidemokrasia lakini sisi tupo kwenye viti tunaendelea kula pizza na raha za vyeo vya kuingia bila haki wala Demokrasia.
Walitakiwa wajiuzulu wote .Sio lazima kuwa uchaguzi ungesubiriwa 2025.
Soma:
- Januari Makamba adai uchaguzi wa 2020 ulitugawa, watu walifungwa, walinyang'anywa pesa, na waliharibiwa biashara zao