JamiiForums Usiku wa manane

JamiiForums Usiku wa manane

Maisha Wakati mwingine Huleta "Surprise" Zisizo na Sherehe...

Kuna kipindi maisha yanakuletea dhoruba usiyoitarajia. Huna namna ya kuiepuka, inabidi tu ukubali matokeo na uishi nayo.
Moja ya dhoruba hizo ni ndoa kuvunjika. Hili siyo jambo la kusherehekea hata kidogo. Ni huzuni kubwa kwa sababu familia inasambaratika.

Hapo ndipo utakuta ama mama anabaki na watoto na baba anasepa, au baba anabaki nao na mama anachukua hamsini zake. Ingawa, ukweli wa mitaani unaonesha mara nyingi ni akina baba ndio wanaonaga nanga kwanza na kuacha jahazi likiyumba.

"World Cup" ya Fitina: Vita ya Wakubwa, Sumu kwa Watoto

Sasa, hapa ndipo ujinga unapoanzia: ndoa nyingi zikivunjika kwa maumivu na hasira, wazazi wanaanza kulipiza visasi. Na silaha yao kubwa inakuwa ni nani? Watoto!
Hapo sasa mzazi mmoja anaanza kuwalisha watoto sumu ya maneno ili wamchukie yule mzazi mwingine ambaye hawaishi naye.

Inapigwa fitina ya kiwango cha World Cup! Lengo likiwa moja tu: kuhakikisha watoto wanamuona mzazi wao mwingine kama adui namba moja.

Ebo! Wazazi wa namna hii acheni ushamba na ujinga.
Ugomvi wenu usiwahusu watoto kabisa—it’s none of their business! Kama mmeshindwana na mmeamua kupigana mwereka wa maisha, pambaneni na hali zenu nyinyi wenyewe, lakini waacheni watoto pembeni.

Swali la Kizushi: Ukifa Kesho Itakuwaje?

Fikiria hili kiutu uzima:

Leo hii unawajaza watoto chuki na sumu kali kama ya Black Mamba—sumu ambayo kupona kwake ni bahati nasibu. Je, kesho ukifa wewe, unategemea hawa watoto wataishi vipi duniani? Utakuwa umewatengenezea ulemavu wa kihisia ambao utawatesa maisha yao yote.
Maslahi ya Watoto Kwanza!

Hata kama mapenzi yenu yamekufa, bado nyinyi ni wazazi. Watoto wanastahili:
Upendo usio na masharti kutoka pande zote mbili.

Huruma na malezi ya baba na mama, hata kama mnaishi mitaa tofauti.
Amani ya akili ili wakue vizuri na kuwa watu bora kesho.

Kwenye mgogoro wenu, wekeni mbele mustakabali wa hawa vijana wetu. Kupasuka kwa ndoa kusimaanishe na maisha ya watoto yameharibika.

Tubadilike ndugu zangu! Chuki isituhofishe tukasahau ubinadamu wetu.

Alamsiki!
 
Sawa homie 😊
 
Back
Top Bottom