ShesRise_1
JF-Expert Member
- Aug 21, 2025
- 19,317
- 45,589
Kwa nini huwa unachelewa kulala?
Kawaida siku inapoanza kwa kuchomoza kwa jua, watu wengi huanza pilika za kutafuta riziki na kutimiza majukumu yao ya kila siku
Wengine huenda kazini, vibaruani, mashambani, sokoni, huku watoto nao wakielekea shuleni
Kwa kifupi, siku huwa imejaa shughuli nyingi zinazochosha mwili na akili
Usiku kwa kawaida huchukuliwa kama muda wa kupumzika na kurejesha nguvu baada ya uchovu wa mchana, isipokuwa kwa wale wanaofanya kazi za usiku
Hata hivyo, pamoja na uchovu wa kutwa nzima, kuna watu wengi ambao hupata shida ya kulala
Mwili unaweza kuwa umechoka, lakini usingizi usije😢
Moja ya sababu kubwa ni msongo wa mawazo
Hofu kuhusu kesho, changamoto za kiuchumi, madeni, kutokuwa na uhakika wa maisha ya baadaye, matatizo ya kifamilia au kimapenzi vinaweza kuifanya akili ishindwe kutulia
Wengine hukosa usingizi kwa sababu ya maumivu ya ugonjwa au changamoto nyingine za kiafya
Pia kuna suala la matumizi ya simu na mitandao ya kijamii
Watu wengi hujikuta wakitumiq simu kwa saa nyingi usiku bila kutambua kuwa muda wa kulala umeshapita
Wataalamu wanashauri mtu mzima apate angalau saa 7 hadi 8 za usingizi kwa siku, lakini kwa baadhi ya watu hilo limekuwa jambo gumu sqna
Mimi binafsi niliwahi kupitia kipindi cha kukosa usingizi kiasi kwamba nilikesha usiku mzima bila hata kusinzia
Hadi leo sijawahi kurudi kuwa na usingizi mzuri kama nilivyokuwa nao zamani,
Nilikua nalala kiasi naweza kunyanyuliwa na kutolewa njee nisijue saivi mtu akitema mate nasikia 😅
hata nikiacha kutumia simu na kuzima mwanga bado usingizi hauji kwa urahisi
Je, wewe mdau, ni nini hasa hukufanya uchelewe kulala?
Ni mawazo mengi, changamoto za maisha, matumizi ya simu, au kuna sababu nyingine?
Unalala usiku wa manane, alfajiri, au mapema kama inavyoshauriwa? 🤔
ShesRise_1 😴😴