JamiiForums Usiku wa manane

JamiiForums Usiku wa manane

Anatulia kidogo unaanza kupata usingizi, come back yake! Ya mwanzo ikasome
Aisee binafsi nikilala na mtu kama huyo kulala kwangu ni mtihani usingizi hauji,ila dawa ni kumshtua akigeuka kidogo inakuwa fresh walau kwa muda fulani
 

"Connection" Isikufanye Ukajiona Mungu Mtu: Somo la Heshima Kazini



Kufahamiana na bosi mkubwa au kuwa karibu na tajiri asiyeugusa udongo, kusikufanye ukaanza kuwatishia bastola walio chini yake. Hii ni siri ya kijinga sana ambayo watu wengi inawaponza.

Binafsi namfahamu jamaa mmoja ambaye, kwa kuwa tu ana uwezo wa kumfikia tajiri kirahisi na kupiga naye stori mbili tatu, basi amejiona amemaliza maisha. Hiyo connection ameigeuza kuwa fimbo ya kuwachapia na kuwadharau viongozi wake wa karibu wa kazi.

Imefikia hatua anajiona yuko juu ya sheria:
Msimamo wake umekuwa: "Hawa wataniambia nini mimi? Who are they?"

Nidhamu sifuri: Kwa mujibu wa watu wake wa karibu, hata kuripoti kazini na kufuata taratibu za kawaida kama wafanyakazi wengine kwake ni msamiati mgeni. Haoni sababu ya kujishusha.

Lakini Swali la Msingi la Kujiuliza: Je, Kesho Iko Wapi?

Maisha hayajawahi kuwa mstari mnyooka. Fikiria kwa makini kuhusu kesho yako kupitia milango hii miwili:

Siku ambayo Tajiri hatokuwepo: Leo tajiri yuko hai na ana nguvu, je, kesho asipokuwepo utauweka wapi uso wako?

Hao uliowadharau jana ndio watakaoshika hatamu.

Nguvu ya "Umoja" wa Chini: Hawa viongozi wa chini unaowapuuza wakiamua kujipanga, wakatengeneza faili lako vizuri na kuliwasilisha kwa tajiri kwa hoja zisizopingika—hadi tajiri mwenyewe aamue kukumwaga—utakimbilia wapi?


Ukweli Mchungu..

Haijalishi una uwezo wa kumfikia nani au una ushawishi gani kwa watu wa ngazi za juu. Hekima, unyenyekevu, na busara bado ni nguzo kuu za utu wako.

Jenga mahusiano mazuri na ya karibu na wale unaoishi nao au kufanya nao kazi kila siku. Maisha yana surprises nyingi sana ambazo huwezi kuzitawala, na kesho yako huijui. Yule unayemkanyaga leo akishuka ngazi, ndiye anayeweza kuwa mtu pekee wa kukushika mkono kesho ukiteleza.
Tupunguze kiburi cha msimu.

Alamsiki!
 
Nimefungua uzi huu kutokana na kuwa na janga la kukata usingizi usiku. Kama na wewe ni mmojawapo naomba tuungane pamoja hapa kwa kuandika ulipo na unafanya nini kwa wakati huo baada ya kukosa usingizi.

Muda wa jukwaa ni kuanzia saa 6 usiku mpaka 11 asubuhi. Mimi hapa leo tangu nimeamka nimeamua KUFANYA IBADA Tuuuu!
Mitungi tu
 
1583.gif

Au asiyesikia la mkuu huenda ni kiziwi wanamsingizia
00:35AM 17-07-2026
 
Back
Top Bottom