JamiiForums kushiriki mjadala wa “ICT for Promoting Digital Security and Data Privacy”, leo Novemba 8, 2023

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,814
11,991
Ikiwa ni Siku ya pili (Nov 8) ya Tamasha la Jinsia kutoka TGNP, JamiiForums inashiriki kwenye Mjadala kuhusu 'Ushirikishwaji wa Wanawake na Wasichana katika Usalama wa Kidijitali na Faragha ya Taarifa'

Mjadala huu utaangazia namna ya kuongeza Ushiriki wa Wanawake kwenye Nyenzo za Kidijitali kutokana na Takwimu nyingi za Kimataifa kuonesha changamoto zinazoendelea kuzuia Wanawake kushiriki kwa usawa katika Sekta ya Teknolojia

Hali ya Kutofikia Teknolojia kutaendelea kuyatenga makundi ambayo tayari yako nyuma, ikiwa ni pamoja na Wanawake na Wasichana wa Vijijini jambo linalowanyima Haki ya Kupata Taarifa na Uhuru wa Kujieleza.

20231108_121403.jpg
 
Back
Top Bottom