JamiiForums Issues an Official Responce to CCM allegations: (Press Release)

JamiiForums Issues an Official Responce to CCM allegations: (Press Release)

Status
Not open for further replies.
A retainer is a fee paid to an attorney or other professional in advance, for services.

:an amount of money that you pay to someone (such as a lawyer) to make sure that you will have that person's services when you need them.

Hapa chini maelezo zaidi.

Kwa hiyo retainer, kwa maneno yangu mwenyewe ni security deposit unayompa wakili na ambayo kwa uzoefu wangu mimi ni non-refundable. Umeelewa sasa?

Ni shule tosha, thanks, kwa vile mimi sio wakili, labda tumuone Msando, tumlipe hiyo retainer ili tumretail kama jf lawyer kwenye hili.
 
Ni shule tosha, thanks, kwa vile mimi sio wakili, labda tumuone Msando, tumlipe hiyo retainer ili tumretail kama jf lawyer kwenye hili.

Msando kama mwanachama wa JF huoni kama hiyo ita compromise baadhi ya mambo?
 
Mtandao wa Kijamii wa Jamii Forums, umekanusha madai yaliyotolewa na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Pius Msekwa, kuwa umeanzishwa na vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na kwamba unatumiwa na chama hicho katika harakati zake za kisiasa hapa nchini.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jamii Forums, unafanya kazi kwa kujitegemea na kwamba haumilikiwi na chama chochote cha kisiasa wala kufadhiliwa na Chadema kama alivyodai Msekwa.

Taarifa hiyo ilisema Msekwa alitoa madai hayo wiki iliyopita wakati akitambulisha Sekretarieti mpya ya CCM mjini Dodoma ambapo alitumia muda wake kushutumu mtandao huo.

Mtandao huo ulisema kwa sasa una wanachama 40,000 waliojiandikisha na kwamba unafanya kazi kama chanzo huru cha habari bila kutumiwa na mtu wala chama chochote cha siasa.

Shutuma hizo za Msekwa zilitolewa Aprili 14, mwaka huu mjini Dodoma ambapo pia mwanasiasa huyo alisema mtandao huo ulichangia kukikosesha kura CCM katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.

Taarifa hiyo iliongeza kwamba shutuma zinazotolewa dhidi yao kwamba unatumika kuivuruga CCM na serikali yake sio za kweli na kwamba zinalenga kuukwamisha mtandao huo katika harakati zake za kuielimisha jamii na kuipasha habari.

Mtandao huo ulisema CCM inauandama kutokana na wao kuwa mstari wa mbele katika kupiga vita vitendo vya rushwa ambavyo hivi karibuni vimekichafua chama hicho na serikali yake.

Shutuma hizo zimewasababishia usumbufu kutoka kwa wanachama wao walioenea kona zote za nchi na nje ya nchi na kwamba hatua hiyo ya CCM ni ishara kuwa kimeanza kuuogopa mtandao huo.

CHANZO: NIPASHE
 
Kama CCM walikuwa na akili timamu basi wangetoa shukrani za ki-pekee kabisa kwa JamiiForums na hata ikibidi kuwawezesha kwa hali na mali (JF) ili izidi kuimarika.
Wameanza kuwezesha JF, promo ya Mzee Msekwa ni sehemu ya ruzuku ya CCM. Wengi wanaweweseka JF ni dude gani hadi msekwa aingie Kiwewe.Wanatafuta njia,wakaribishwe!
Na Wangekuwa wanasoma maoni mbalimbali yanayotelewa humu with open mind wasingekuwa hata na haja ya kuingia gharama ya kumlipa yule 'consultant'
.
Ni maoni hayo ndiyo wanayafanyia kazi kwa mtindo wa kujivua gamba. Walichotaka ni kupata maelezo ya Consultant aliyevaa njano na kijani, lakini yote waliyoyapitia ni matokeo ya mijadala.
Nchi nyingine wanaingia gharama kubwa kujua nini maoni ya wanachi kuhusu sera na utekelezaji wake, kukubalika kwa viongozi wake na hasa maoni ya wananchi mara pale wanapokumbwa na kashfa kubwa kubwa. EPA, Kagoda etc zimejadiliwa sana humu Jamvini na hasa kipindi cha kabla ya uchaguzi. Wangeweza kujua kabisa nini maoni ya watu (hata kama sio scientic research) but you can detect public mood kwa kusoma humu JF. Walipuuza sasa yamewakuta ya kuwakuta wanaona tatizo ni JF na wala soi uzembe wao kutofautilia public mood
Kuvuja kwa pakacha. Ni wagumu hawa kuelewa hata Mungu atakapotangaza hakuna kufa tena, bado watahitaji kujadili ndani ya CC na NEC
Watu wenye akili timamu kama Dr. Slaa, Mnyika Regia Mtama na wengine wengi wamo humu kwa sababu wanaelewa nini maana ya kiongozi wa umma kutenda kwa kuzingatia maoni ya hao unaowangoza.
Hao uliowataja wanajua kitu kinaitwa Public relationship(PR). CCM wanajua PR ni kuzusha habari TBC, Uhuru na Radio Uhuru
Mzee Msekwa angeweza kukutaka (kwa hoja) na Mzee Mwenzie Mtei. CCM wanaona JF ni adui! upofu gani huu?
Mzee Mtei anakwenda na wakati,msikivu na makini ndio maana aliwaacha miongo miwili iliyopita. Mzee Msekwa bado anatafakari jinsi alivyosimamia kamati ya kuunganisha TANU na ASP hata kama nusu ya 'audience' ilikuwa haijazaliwa.
Ni Mheshimiwa mmoja tu kutoka CCM nimeshamwona humu kwa jina la Hamis Kingwangalla, labda wapo wengine kwa ID tofauti
Wapo wengi, lakini hawajitokezi kwasababu ya nidhamu ya woga. Wanaogopa kuitwa mbele ya CC au NEC, kwao bora liende.
Lakini hawa wakina Nape, January na kiongozi wao Mukama wangeia humu tena ikiwezekana kwa ID zao kama walivyofanya Dr. Slaa, Myinka Regia Mtama, Zitto na hata mwenzao Kingwangwalla na kueleza hoja zao, maudhi na hata hizo shutuma zao za JF kutumiwa na CDM
Wataingia tu hata kwa ID fake maana mzee Msekwa kawatonya wapi kisima cha maji kilipo, wengi tu wameshajiunga kimya kimya.
Kubeba watanzania waliopigika kimaisha kwenye fusso na kuwapigia muziki wa taarab kisha propaganda hakuwezi hata siku moja kusaidia kutengeneza sera wala kujua uhalisia wa namna/kiasi gani sera na utekelezaji wake unakubalika kwa umma
Ndiyo maana wananchi wameanza kutoa adhabu kali kupitia sanduku la kura, maandamano, makongamano n.k Huwezi kumfunza mbwa mzee mbinu mpya.
Waje humu ndani watoe hoja ili zijibiwe na great thinkers wanaoweza kutoa critical analysis na sii kutupigia kelele with their un-answered style mara TBC mara Manzese kwa Bakhressa.
Wanakaribishwa jamvini.
 
Huwezi kuweka constraints (vikwazo) kwa mawazo ya mwanadamu kuhusu suala lo lote. Kwa ni fursa nzuri kuruhu uwezekano wa fikra zote zijitokeze ili uziweke kwenye mizani. Sikubaliani na wewe kwa hoja yako. Kwa saikolojia ya ualimu kazi kubwa ni kuibua fikra za mwanafunzi kwa sababu akiweza kuzitoa kwa uhuru ataweza kukabiliana na mitihani ya darasani na ya dunia.

CCM walishaamua kufikiri, kuamua na kutenda watakavyo badala ya kila mtanzania wala siyo kwa naba ya mtanzania

Kwa mantiki hiyo Hoja zote zinaheshimika. Hatuhitaji kukubaliana au kutokubaliana bali mitazamo na fikara tofauti mwishowe azimio litapatikana. Tazama Star TV Jumamosi nitafanya kipindi cha Jicho letu katika habari ITEM Hii nitaiweka mawazo na michango yenu ni itasaidia kupambanua ukweli.
 
Kumbe na wao wanabrowse JF, sasa tumeng'amua CCM wote wanakurupuka kujenga hoja zisizo na msingi.

Ukimwambia Msekwa athibitishe kauli yake hana lolote, kazi kuongea hovyo utadhani yupo msalani.

Tatizo CCM wakishaona kuna jamii iko against their will wanaanza kuropoka eti wanashabikia CHADEMA, mimi nadhani kujivua gamba haitoshi, hawa jamaa inatakiwa wachunwe ngozi kabisa.
 
I feel sorry for MKJJ and his crew

Malalamiko ya kuwa JF ni kijiwe cha chadema yamesemwa sana humu ndani, ila tatizo waliosema hawakuwa akina Msekwa!

Leo mnashtuka when things is too late.

What I ahve learned is that is easy to point fingers to others, sijaona action hii ya MKJJ na timu yake na tabia za CCM na ku-act when is too late. is this not what the famous statement of NN intercept kuwa miafrika ndivyo tulivyo?

Since May 2010 kumetokea tremendeous change in JF hakuna hoja bali matusi tu na viroja, yet you want Msekwa to say otherwise??

mpaka mnawaza mawakili, sijui nani nani! what a joke?

Tatizo lipo, tulibadilishe, MKJJ once again live by your standard double standard always suck.

This is too late action, malalamiko yaliishakuwepo humu, ila kasema Msekwa....
 
Ni wazi kuwa hujasoma alichosema Msekwa na pili hujaweza kupima uzito wa kile kilichosemwa na kiongozi wa juu wa chama na taarifa yao. Ni jambo moja kudai kuwa JF inatumiwa sana na Chadema au wanachama wake wengi ni mashabiki wa Chadema au kusema kuwa sauti za vyama vingine haisikilizwi vya kutosha. Huo ni mjadala peke yake na hayo ndiyo yanasemwa.

Utaona kuwa Msekwa hajasema JF ni "kijiwe cha Chadema" kwani angesema hivyo angefanana na walialia wengine wa JamiiForums. Yaani kwa vile mashabiki wa mtandao huo wanaonekana kuwa ni wengi kuliko wa vyama vingine basi ndio kimekuwa "kijiwe cha Chadema". Well mngependa watu wafanye nini? Tulinganishe maoni kwa kuhakikisha yakitolewa maoni ya 50 yanayounga mkono CHadema basi maoni 50 yanayoipinga nayo yatolewe? Mngependa wanachama wachujwe ili ionekane kuna uwiano? Hivi au mashabiki wa Chadema ambao hawana sauti kwenye vyombo vya habari vya Tanzania waende wapi? Sote tuliona jinsi Vyombo vya serikali vya habari vinayoibeba serikali ya CCM bila hata haya na bila kujali ni lini vyombo hivyo vilifungua kwa usawa habari za vyama pinzani? Tena baya zaidi nikuwa vyombo hivyo vya habari vinalipiwa na walipa kodi wa Tanzania! Sasa ukiita "vijiwe" basi nihivyo vyombo vyenu vya habari TBC, DAily News n.k ndivyo kweli vimekwua vijiwe vya CCM.

Halafu huko kudai kuwa ati JF "hakuna hoja bali matusi tu" ni kutia chumvi kusiko kwa lazima. Hivi wewe ulipoandika mambo ya Dr. Slaa ulikuwa unaandika matusi na viroja? Umewahi kusoma nikiandika matusi mimi? Kweli unaweza ukasema vinavyoandikwa na watu wengi ni matusi na viroja? Au ndio mbinu ile ile ya kujaribu kuidiscredit JF?

Kurudi kwa Msekwa labda usome hasa alichokisema na labda.. and I mean labda utaelewa tofauti ya alichosema yeye na chama chake na kile ambacho watu hulalamika wakisubiri kubebwa au kupewa upendeleo waliozoea kama chama tawala. Ukishindwa kuona tofauti hiyo nitafurahi kukuonesha.

And no! sina crew.. its just me, myself and I.. and I LOVE JF!
 
kufikiwa kwa madai haya ni ishara kuna watu wanaoiona jf kwa mtazamo huo! Wanaweza wasiwe sahihi lakini itambulike kuwa wapo! Inawezekana wanashawishika kuwa na mantiki hiyo kutokana na pengine colour tone ama mwelekeo na density ya michango dhidi yao, hii ikawa fallacy kuihukumu jf. Bado haiondoi jukumu la jf kwa vitendo na kauli kuwashawishi wanaoamini hivyo kuwa jf haina predatory psychological aggression dhidi yao au wanataka waiambukize gamba?
 
I feel sorry for MKJJ and his crew

Malalamiko ya kuwa JF ni kijiwe cha chadema yamesemwa sana humu ndani, ila tatizo waliosema hawakuwa akina Msekwa!

Leo mnashtuka when things is too late.

What I ahve learned is that is easy to point fingers to others, sijaona action hii ya MKJJ na timu yake na tabia za CCM na ku-act when is too late. is this not what the famous statement of NN intercept kuwa miafrika ndivyo tulivyo?

Since May 2010 kumetokea tremendeous change in JF hakuna hoja bali matusi tu na viroja, yet you want Msekwa to say otherwise??

mpaka mnawaza mawakili, sijui nani nani! what a joke?

Tatizo lipo, tulibadilishe, MKJJ once again live by your standard double standard always suck.

This is too late action, malalamiko yaliishakuwepo humu, ila kasema Msekwa....

Dude!!.......wat happn' t' ya dude!.......me na believe dis........dis ain't ya at all
 
Si mngekaa kimya tu wakabwabwaja hadi mwisho? JF ipo na itawndelea kuwepo, siku-join JF kwa ajili ya CDM na kuipinga CCM, i joined JF kwa sababu niliona ni place ambayo I can express my feelings na ikawafikia wengi zaidi kwa haraka zaidi! CCM waache kujishuku na kama wanaona ni wao basi wajue wana tatizo! wajichunguze!
 
Ni wazi kuwa hujasoma alichosema Msekwa na pili hujaweza kupima uzito wa kile kilichosemwa na kiongozi wa juu wa chama na taarifa yao. Ni jambo moja kudai kuwa JF inatumiwa sana na Chadema au wanachama wake wengi ni mashabiki wa Chadema au kusema kuwa sauti za vyama vingine haisikilizwi vya kutosha. Huo ni mjadala peke yake na hayo ndiyo yanasemwa.

Utaona kuwa Msekwa hajasema JF ni "kijiwe cha Chadema" kwani angesema hivyo angefanana na walialia wengine wa JamiiForums. Yaani kwa vile mashabiki wa mtandao huo wanaonekana kuwa ni wengi kuliko wa vyama vingine basi ndio kimekuwa "kijiwe cha Chadema". Well mngependa watu wafanye nini? Tulinganishe maoni kwa kuhakikisha yakitolewa maoni ya 50 yanayounga mkono CHadema basi maoni 50 yanayoipinga nayo yatolewe? Mngependa wanachama wachujwe ili ionekane kuna uwiano? Hivi au mashabiki wa Chadema ambao hawana sauti kwenye vyombo vya habari vya Tanzania waende wapi? Sote tuliona jinsi Vyombo vya serikali vya habari vinayoibeba serikali ya CCM bila hata haya na bila kujali ni lini vyombo hivyo vilifungua kwa usawa habari za vyama pinzani? Tena baya zaidi nikuwa vyombo hivyo vya habari vinalipiwa na walipa kodi wa Tanzania! Sasa ukiita "vijiwe" basi nihivyo vyombo vyenu vya habari TBC, DAily News n.k ndivyo kweli vimekwua vijiwe vya CCM.

Halafu huko kudai kuwa ati JF "hakuna hoja bali matusi tu" ni kutia chumvi kusiko kwa lazima. Hivi wewe ulipoandika mambo ya Dr. Slaa ulikuwa unaandika matusi na viroja? Umewahi kusoma nikiandika matusi mimi? Kweli unaweza ukasema vinavyoandikwa na watu wengi ni matusi na viroja? Au ndio mbinu ile ile ya kujaribu kuidiscredit JF?

Kurudi kwa Msekwa labda usome hasa alichokisema na labda.. and I mean labda utaelewa tofauti ya alichosema yeye na chama chake na kile ambacho watu hulalamika wakisubiri kubebwa au kupewa upendeleo waliozoea kama chama tawala. Ukishindwa kuona tofauti hiyo nitafurahi kukuonesha.

And no! sina crew.. its just me, myself and I.. and I LOVE JF!

Nilifikiri umepumzika ijumaa kuu! kumbe upo? tuendelee mkuu

we all love JF! LOL!
 
Ku focus kwenye nani anayesema, badala ya nini kinasemwa, ni umasikini wa fikra.

Hata kama JF ni ya CHADEMA (which is not necessarily the case), tuambieni kinachosemwa kina mantiki au hakina?

Mgharibi ni kawaida kabisa kujua kwamba NY Times is a liberal leaning paper while Wall St Journal is a Conservative paper, hii haileti ugomvi, kinachotakiwa kuleta ugomvi ni nini kimesemwa, sio nani kasema.

Moja ya sababu za kushindwa kuendelea Afrika ni ukweli kwamba hatuna ideologies, siasa zetu zinafuata personalities. Na kama huna ideologies, huwezi kuwa na middle class iliyo meaningful politically, and the vicious circle contines, huna a politically meaningful middle class thereofore no ideology on and on and on.

Ndiyo maana kila siku ukija hapa utasikia Zitto hivi, Makamba hivi, ukiwauliza watu ideology ya CHADEMA ni nini? Policy ya mambo ya nje ni nini? Wanasemaje kuhusu mazingira, kazi, maji etc?

Wwatu kiiimya.
 
Niwakumbushe chama cha magamba kwamba maoni yatolewayo kwenye jukwaa ni ya watanzania wazalendo, watu waliochoka na maovu, yanayofanywa na wenye madaraka. Hivyo wana jf ni ya wanachama wa vyama vyote vya siasa na wale wasio na vyama. Kusema jf ni ya chadema ni kukosa hoja.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom