JamiiForums Issues an Official Responce to CCM allegations: (Press Release)

JamiiForums Issues an Official Responce to CCM allegations: (Press Release)

Status
Not open for further replies.
Sasa Kama wanalalamika Jf ni ya Chadema,si na wao waanzishe mtandao wao wa ccm?,au waje huku kutetea hoja sio kupiga blablaa tu mtaani huko.Kwanza nna wasiwasi na Msekwa kwa uzee wake huwa ni msahaulifu na ulimwengu umemyacha nyuma mfano ktk kongamano la kuunda katiba mpya ambalo liliwahi kurushwa na ITV na Msekwa alikua mgeni rasmi,alishindwa kujibu maswali aliyoulizwa na waandishi,wananchi kwa asilimia 75%.
 
Karafuu ni zao linalotokana na mkarafuu, ingawa karafuu hazimo katika kundi la vyakula wala vinywaji, lakini ni kiungo muhimu sana. Karafuu zina matumizi kadha, wakati fulani zinatumika kwenye utengenezaji wa sigara, upishi, utengenezaji wa aina fulani ya dawa ya meno, na pia mafuta yake hutumika kwa kuchua misuli.

Kutokana na kitabu cha historia, mikarafuu ilianza kupandwa kwenye visiwa vya Shelisheli, Mauritius na sehemu nyinginezo. Miche ya mkarafuu ililetwa Zanzibar kutoka Mauritius mwaka 1818, miti hii imestawi zaidi Visiwani Unguja na Pemba ambavyo vinatoa asilimia 80 ya karafuu zinazohitajika duniani. Na uchumi wa visiwa vya Zanzibar unategemea sana zao la karafuu.

Meneja masoko wa shirika la biashara la taifa la Zanzibar ZSTC Bwana Suleiman Juma Jongo alisimulia kwa undani kidogo kuhusu historia ya kilimo cha karafuu na hali ya upandaji wa mikarafuu visiwani Zanzibar. Alisema kuwa:

"Historia ya upandaji wa karafuu visiwani imeanza zamani sana. Miche ya mikarafuu kuja kwake hapa imetokana na visiwa vya Indonesia, mashariki ya mbali, ilifika huko Madagasca na shelisheli katika karne ya 19, na ndiyo ikakuja hapa kwetu Zanzibar na kupandwa wakati wafalme wa Oman walipotawala hapa. Kimbunga kiliwahi kutokea na na kiling'oa mikarafuu mingi. Kwa hivyo kukawa na juhudi mpya ya wafalme wa wakati ule ya kupanda mikarafuu mipya. Lilikuwa si kitu hiari, bali lilikuwa lakini ni jambo la lazima, watu wapande mikarafuu kwa sababu kitu hicho kinasaidia uchumi."

"Kabla ya mapinduzi, mashamba ya mikarafuu yalikuwa ni ya watu binafsi, lakini baada ya mapinduzi, serikali ilitaifisha ardhi na kuigawakwa wananchi. Kila mwananchi alipata eka tatu za kumwezesha kulima, kupata chakula chake, na kupata mahitaji yake ili ajiendeleze na familia yake. Na hiyo imeendelea mpaka leo, kwa hiyo sasa suala la karafuu linamilikiwa na wananchi wenyewe. Idadi kubwa ya mashamba yalikuwepo ni ya wananchi wenyewe. Ingawa kuna maeneo ya serikali, maeneo yanayomilikiwa na serikali ambayo yana karafuu na serikali inawakodisha watu ambao wanataka kukodi, kuchuma na kuuza, mashamba hayo yapo Zanzibar na Pemba."

Bwana Jongo aliongeza kuwa:

"Sasa utaratibu wa upandaji wa zao la karafuu bado unashughulikiwa na wizara ya kilimo, wizara ya kilimo ndiyo yenye idara maalum ya kuendeleza mazao haya ya biashara. Sasa wizara ya kilimo ndiyo inashughulika kuwa na vitalu vya miche ya karafuu."

"Kwa kuwa ZSTC ndiyo inayoshughulikia zao la karafuu, serikali kupitia wizara ya biashara ya ZSTC inachangia maendeleo ya zao la karafuu. Inawalipa vibarua wanaoshughulikia kuendeleza upandaji wa mikarafuu mipya katika sehemu mbalimbali ambazo mikarafuu imekufa, ZSTC inanunua zana za kutengeneza miche na kupanda miche mpaka kuisambaza kwa wananchi."

Bibi Mosesev Hatibu amefanya kazi katika taasisi ya utafiti wa kilimo ya Zanzibar Unguja, anaelezea kwa undani jinsi ya kuotesha miche ya karafuu na jinsi ya kutunza shamba la mikarafuu. Alisema kuwa:

"Kwanza unatayarisha eneo lako, unapiga tuta kisha unaweka mbolea, halafu unachukua majani makavu yaliyotokea katika mikarafuu. Unapiga mistari unaweka zile mbegu za mikarafuu ambayo ni matende. Ukisha panda unafunika majani makavu ya mkarafuu, unamwagilia maji halafu unaweka kivuli, unapalilia kila baada ya wiki. Baada ya mwezi mmoja, matende tayari yashaanza kuchipua, unaiacha miche yako vile mpaka itimie miezi miwili. Baada ya miezi miwili, unaenda kung'oa unachukua kimoja kimoja pamoja na kile kitende chake kile ambacho ni mchele mkarafuu uliochipua, unauchukua na kuuweka kwenye mifuko, na mifuko hiyo inakuwa imewekwa udongo ambao umechanganya na mbolea, halafu unachukua "humus" ambayo ni takataka zenye mbolea, una mchanganyiko huu unaweka kwenye mifuko."

"Unapandikiza miche yako, miche yako unaitunza inakaa kwa muda wa miezi mitatu mpaka minne. Miche yako imeshakuwa tayari, imeshakuwa mikubwa ina majani sita mpaka manane unaiacha kwa miezi sita, baada ya miezi sita miche yako inakuwa tayari kwa kupelekwa shambani. Katika msimu wa mvua wa masika au vuli, unakwenda kupiga mashimo unapanda, sasa katika kupanda shambani mikarafuu mimi nashauri wakulima wapande na mazao mengine kwa ili shamba la mikarafuu liwe safi, wapande mihogo au migomba ili kupata kivuli na shamba liwe safi sio wapande mikarafuu mitupu."

Idhaa ya Kiswahili 2004-11-30
 
Binafsi sioni tatizo wao kujiingiza humu rather naona ni njia sahihi kupata maoni mbadal ya wananchi wenye uchungu na nchi yao, otherwise kama tunapoteza muda, naunga mkono wao kutembelea JF hata kama kwa ID za kufoji its ok
 
Jamani wanJF ni muda mrefu sasa CUF haijasikika
Je JF inawatendea haki? kwani kila siku na habari za chadema na ccm?

Kuna mtu ana habari kama hiki chama bado kipo?

kama bado kipo nashauri JF itendee haki kwa vyama vyote
kwani JF ni nani wee mat@ko?
 
Kama CCM walikuwa na akili timamu basi wangetoa shukrani za ki-pekee kabisa kwa JamiiForums na hata ikibidi kuwawezesha kwa hali na mali (JF) ili izidi kuimarika. Na Wangekuwa wanasoma maoni mbalimbali yanayotelewa humu with open mind wasingekuwa hata na haja ya kuingia gharama ya kumlipa yule 'consultant'. Nchi nyingine wanaingia gharama kubwa kujua nini maoni ya wanachi kuhusu sera na utekelezaji wake, kukubalika kwa viongozi wake na hasa maoni ya wananchi mara pale wanapokumbwa na kashfa kubwa kubwa. EPA, Kagoda etc zimejadiliwa sana humu Jamvini na hasa kipindi cha kabla ya uchaguzi. Wangeweza kujua kabisa nini maoni ya watu (hata kama sio scientic research) but you can detect public mood kwa kusoma humu JF. Walipuuza sasa yamewakuta ya kuwakuta wanaona tatizo ni JF na wala soi uzembe wao kutofautilia public mood.

Kwangu mimi naona kama JF ingekuwa ni one of the sources ya kupata maoni ya wananchi almost instantly for FREE na kuyafanyia kazi mambo fulani fulani. Watu wenye akili timamu kama Dr. Slaa, Mnyika Regia Mtama na wengine wengi wamo humu kwa sababu wanaelewa nini maana ya kiongozi wa ummakutenda kwa kuzingatia maoni ya hao unaowangoza. Mzee Msekwa angeweza kukutaka (kwa hoja) na Mzee Mwenzie Mtei. CCM wanaona JF ni adui! upofu gani huu?.

Ni Mheshimiwa mmoja tu kutoka CCM nimeshamwona humu kwa jina la Hamis Kingwangalla, labda wapo wengine kwa ID tofauti. Lakini hawa wakina Nape, January na kiongozi wao Mukama wangeia humu tena ikiwezekana kwa ID zao kama walivyofanya Dr. Slaa, Myinka Regia Mtama, Zitto na hata mwenzao Kingwangwalla na kueleza hoja zao, maudhi na hata hizo shutuma zao za JF kutumiwa na CDM. Kubeba watanzania waliopigika kimaisha kwenye fusso na kuwapigia muziki wa taarab kisha propaganda hakuwezi hata siku moja kusaidia kutengeneza sera wala kujua uhalisia wa namna/kiasi gani sera na utekelezaji wake unakubalika kwa umma. Waje humu ndani watoe hoja ili zijibiwe na great thinkers wanaoweza kutoa critical analysis na sii kutupigia kelele with their un-answered style mara TBC mara Manzese kwa Bakhressa. Chicken!
 
Kama CCM walikuwa na akili timamu basi wangetoa shukrani za ki-pekee kabisa kwa JamiiForums na hata ikibidi kuwawezesha kwa hali na mali (JF) ili izidi kuimarika. Na Wangekuwa wanasoma maoni mbalimbali yanayotelewa humu with open mind wasingekuwa hata na haja ya kuingia gharama ya kumlipa yule 'consultant'. Nchi nyingine wanaingia gharama kubwa kujua nini maoni ya wanachi kuhusu sera na utekelezaji wake, kukubalika kwa viongozi wake na hasa maoni ya wananchi mara pale wanapokumbwa na kashfa kubwa kubwa. EPA, Kagoda etc zimejadiliwa sana humu Jamvini na hasa kipindi cha kabla ya uchaguzi. Wangeweza kujua kabisa nini maoni ya watu (hata kama sio scientic research) but you can detect public mood kwa kusoma humu JF. Walipuuza sasa yamewakuta ya kuwakuta wanaona tatizo ni JF na wala soi uzembe wao kutofautilia public mood.

Kwangu mimi naona kama JF ingekuwa ni one of the sources ya kupata maoni ya wananchi almost instantly for FREE na kuyafanyia kazi mambo fulani fulani. Watu wenye akili timamu kama Dr. Slaa, Mnyika Regia Mtama na wengine wengi wamo humu kwa sababu wanaelewa nini maana ya kiongozi wa umma kutenda kwa kuzingatia maoni ya hao unaowangoza. Mzee Msekwa angeweza kukutaka (kwa hoja) na Mzee Mwenzie Mtei. CCM wanaona JF ni adui! upofu gani huu?.

Ni Mheshimiwa mmoja tu kutoka CCM nimeshamwona humu kwa jina la Hamis Kingwangalla, labda wapo wengine kwa ID tofauti. Lakini hawa wakina Nape, January na kiongozi wao Mukama wangeia humu tena ikiwezekana kwa ID zao kama walivyofanya Dr. Slaa, Myinka Regia Mtama, Zitto na hata mwenzao Kingwangwalla na kueleza hoja zao, maudhi na hata hizo shutuma zao za JF kutumiwa na CDM.

Kubeba watanzania waliopigika kimaisha kwenye fusso na kuwapigia muziki wa taarab kisha propaganda hakuwezi hata siku moja kusaidia kutengeneza sera wala kujua uhalisia wa namna/kiasi gani sera na utekelezaji wake unakubalika kwa umma. Waje humu ndani watoe hoja ili zijibiwe na great thinkers wanaoweza kutoa critical analysis na sii kutupigia kelele with their un-answered style mara TBC mara Manzese kwa Bakhressa. Chicken!
 
Msekwa amepitwa na wakati. Mimi siko chadema lakini, I AM PROUD MEMBER wa jamii forums. Hapa ni sehemu ya watu wanaotaka maendeleo katika taifa lao. Wao akina Msekwa hawawezi kukabiliana na "criticism" ya uongozi wao. Wamejifanya ni miungu ya dunia. Jamiiforums Oyeeeee.
 
Nimesikitika sana Serikali ilivyomtosa MHANDO pale TBC kisa eti katoa ruhusa midahalo ya wazi kuendehwa live! Mimi kwa maoni yangu bwana Mhando aliisaidia sana CCM (Chama Cha Magamba) kujitetea mbele ya wananchi lakini wao wakawazuia wagombea wao kujieleza mbele ya waajiriwa wao ambao ni wanachi. Hii ilikuwa dharau kubwa kwa wananchi kunyimwa haki ya msingi ya kuwahoji wagombea wao. Hata tunapoomba kazi kwenye ofisi yoyote ile lazima uhojiwe ni kwa nini umependa kufanya nao kazi na kipi kipya utawafanyia na wewe kweupata nafasi ya kujua utafaidikia vipi kwenye kazi hiyo. Aibu hii ilizidi pale ambapo Rais naye alipogoma kushiriki mdahalo na wagombea wenzake. Hili nalo wananchi tulikukmbuke kuwa alitudharau sote watanzania. Si wote tuliopata nafasi ya kuhudhuria mikutano ya kampeni hivyo kwa kushiriki mdahalo angetuwezesha kumsikia na pengine kumhoji juu matarajio yetu kwake. Nadhani hawa CCM hawajajua maana ya nguvu ya umma/jamii nawaomba waangalie na wajifunze kilichotokea Misri, Algeria........ Nawaomba wana-Magamba wajitafakari juu ya nguvu ya umma wa Watanzania wasidhani wako kwenye kisiwa ambacho hakiwezi kufikiwa na hayo yaliyotokea kwa wenzetu........
 
Utaweza kweli kuyathibitisha hayo? That's just frivolous.

Mkuu hii inawezekana. They can perform trend analysis of visitors before the announcement and after!! Make a cross analysis by having a sample when things were calm!!

This is possible mkuu....
 
I dont believe such statement being given by such a matured person like P msekwa ...

... why give Power to JF so easely..!!
 
hawa majuha yasibabaishe watu..kwani kwa tafsiri yao mtu yeyote anayetaka ukweli ni ANT Chama Cha Magamba...I say to hell with what ever they think, now they r out of ideas they what to start what wont be finished.,,,TUWAKARIBISHENI..
 
Mkuu hii inawezekana. They can perform trend analysis of visitors before the announcement and after!! Make a cross analysis by having a sample when things were calm!!

This is possible mkuu....

I doubt it. This is not a winnable case. I am waiting to be proved wrong.
 
Mwanakijiji / Maxence / Wanasheria wanachama wa JF / Wana JF

Je; Inawezekana kuiburuza CCM mahakamani na kudai Damages / Fidia kwa habari za:

1. Uongo
2. Kuivunjia Heshima na Hadhi JF
3. Kuwasababishia wanachama usumbufu, kuwapa wasiwasi na kuwaumiza kisaikolojia?

We dare to talk openly and we can also dare to DO openly.

JF should not take any "Bullshit" from CCM nor any Party nor the Government. We are simply a social network.

Why dont we give them a lesson? Tunaogopa nini au tunamwogopa nani?

Mkuu nakubaliana na hoja yako, ila kwa Tanzania hatuna mahakama huru tuna tawi la serikali linalofanya kazi kwa maelekezo ya watawala. Rejea kesi ya mtikila dhidi ya mgombea huru, rejea kesi zote za uchaguzi, ingekuwa ni nchi zenye kujali sheria kufuata na kuacha sheria iwe huru saa hizi tungeisha pata hukumu zote za wabunge walioiba kura na tungekuwa tumeisha chagua wabunge wanaowakilisha wananchi.

CCM ingekuwa imepoteza wabunge zaidi ya 50 waliotangazwa wameshinda so far. Ila kuwa serikali ya CCM, mahakama ya CCM, na bunge la CCM usitarajie kupata haki yako kwa kumshitaki CCM
 
hahaha, kama kikosi kazi cha CCM ndio kilimshauri Msekwa kuwa JF ni adui na vijana wa Chadema, no wonder hata taarifa za kiinterejensia za polisi hufanya madudu, maana kizaliwacho na nyoka ni nyoka! shame mtu kama msekwa na chama kama CCM pamoja na wasomi waliomo ndani ya chama hicho wanaweza kukimbili very weak urgement na ku point finger kwa JF! no wonder then Pinda na JK hawajui chanzo cha umaskini wa nchi hii, si ndio wataalam wao wa utafiti huwapa taarifa dhaifu kama hizi!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom