JamiiForums Issues an Official Responce to CCM allegations: (Press Release)

Status
Not open for further replies.
Umeua!

With that reason is not surprising ukamsikia mwanasiasa anatoka chama kimoja kwenda kingine! akina prof. Safari na akina Shitambala!.what a shame!

Ideology is what makes you!is what makes party..


What do you mean by Ideology!?

If you are referring what is meant as a Philosophy! or a System! How can that be a political party's policy or strategy behind socio-economic development!? It is impossible! Discuss it!

Isn't that, not a school of thought! A country Constitutional arena! If that is the case then Political Parties have nothing to do but setout policies and strategies on the country's Ideology.
 
Tatizo la ccm sio kujiunga hapa jamvini kwani waliwahi kukatazwa nani?
Wao nadhani bado wana ile kasumba ya kutoshiriki majadiliano kama walivyokatazwa na makamba wakati wa machakato majimboni hapa wanajf wote ni sawa na hauulizwi chama wala dini wala kabila walete hoja hapa na wawe tayari kuzitetea vinginevyo kweli wataona ni cdm kama wanacdm watashinda hoja
 
Eti wamevua gamba. Hivi nani kawadanganya kuwa kuvua gamba kunatoa sumu mwilini? Au nani kawambia mgogod ukitolewa gamba unakua kiazi.? Ama kweli Kikwete hana jipya hajui kavua gamba ila Sumu inamtafuna Kufa lazima afe
 
Hoja inaeleweka barabara, ingawa kuna watu wanajaribu kupindisha kwa kuwa wanaisoma huku wamepindisha shingo zao!

Mimi sioni tofauti ya hao wanolalama Jf ni ya Chadema na wale waliosema Chadema ni hatari kwa Uislamu na kutia chumvi kuwa ni mali ya Wakisto! Nikasubiri kuona Wakistro wote wakiama CCM kuingia Chadema sijaona leo, badala yake nimeona Wakisto wakitoka Chadema kwenda CCM!.

Mhe. Waberoya wasiliana na Msekwa lete list ya watu wa CCM waliowai kuomba registration humu JF wakakataliwa, twende kwa ushahidi sasa, Pia mnaweza kujenga ushahidi wa kitu ambacho Wana-JF wamewai kuisingizia CCM (kuipaka matope) tokea JF imeanza hadi leo 23th April, 2011.

Kama kuna kitu kinaitwa unafki basi kinaweza kuwa hicho cha kusema JF imekuwa kijiwe cha Chadema, nasema huo ni Unafki kwa sababu Zaidi ya asilimia themanini (80%) ya wana-JF hawajuwani! (Wanakutana humu kwenye thread yamkini hata ukikutana na Member mwenzio huwezi kumjua) labda kwa asilimia ishirini (20%) waliojing'amua bayana kama Mbunge wa Nzega, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, mbunge wa Ubungo, Albeto Msando, Mkumbo Kitila, Mhe. Regia, Dr. W Slaa n.k. Albeto, Zito na Dr. Slaa sina uhakika asilimia mia moja (100%) maana wao pia hata picha zao hawakuweka, ila Mbunge wa Nzega, Mkumbo, Mhe. Regia na wengineo wameweka Picha zao.

Kwa mantaki hiyo JF members wanajijua wao kila mmoja katika roho yake na nafsi yake yeye ni Chama gani lakini members wengine hawajui! Lakini pia wanajiunga kila mmoja mwenyewe kwa utashi wake bila kutumwa na Chadema wala CCM, ndio maana kuna wanachama wenye mapenzi na CCM, Chadema, CUF, NCCR Mageuzi nk. Pia kuna wasio na vyama kama mimi binafsi.

Hata hivyo kila mmoja anapaswa kusoma maneno ya Msekwa na kuyachambua kwa mapana kabla ya kujaribu kuona kuna hoja ndani yake, ni vyema waliosahau kuwa JF members sio wote wanashiriki hoja za siasa, mimi nawajua wana JF ambao hata hawajui kama kuna mijadala ya kisiasa inaendelea ndani ya JF, wao kila kukicha wapo ndani ya Jukwaa la Mahusiano na Mapenzi! Nadhani kwa kiwango kikubwa Mkuki unaoichoma CCM utokea jukwaa la Kisiasa au kuna mtu anataka kutwambia hata hoja za mahusiano na Mapenzi pia inaibomoa CCM!

Mimi Binafsi nimewai kuuliza na kusema kuwa kama ningelikuwa mwanazuoni katika eneo la sayansi ya Siasa, ninge fanya tafiti kubaini iwapo kuna ukweli kuwa chama cha siasa kinakuwa, kinakomaa na baadaye kinazeeka na kuwa kikuukuu na hivyo kuishiwa nguvu kama binadamu anavyoishiwa nguvu za mwili (misuri), nguvu za ubongo (akili na uwezo wa kufikiri) na hata kupoteza uhai (kufa) hata kama kina vijana. Nasema hivyo kwa sababu kama CCM ingelikuwa haielekei kufa basi kila kiongozi wa CCM angelichangia JF iendelee na idumu milele, maana hakuna anayekujenga kama aneyekwambia mapungufu yako mbele ya Jamii! nasema hakuna mahala na wakati unaweza kujirekebisha vyame kama wakati unajua kinagaubaga mapungufu yako, labda kama unataka kufa nayo! mtu akikwambi Mkuu umeshau kufunga flazi ya suruali yako, kwa mtu Mstaarabu unapaswa kumshukuru, hivyo ndivyo CCM inavyopaswa kuwa.

Kama CCM inadhani kuwa members wengi JF ni wanachama wa Chadema na kuwa hoja nyingi za JF ni kuichambua serikali ya CCM, basi wale wanamunga Msekwa mkono wanaweza kujibu maswali yafutayo kama changamoto mpya katika fikra Pevu kama anavyoita Mwnakijiji: -

  • Kama uwanachama wa JF ambao unapatikana kwa hiari unaipa CCM kiwewe, Je? CCM ipo tayari kuona wapinzani wanashinda nafasi nyingi za Ubunge! au CCM inasema nini juu wa wabunge wa Chama kuwemo ndani ya Bunge la muungano!
  • Kama kuna mtu anadhani ianayo sakamwa sana ni serikali ya CCM kwanini CCM hisijaribu kuondoka madarakani ili tuone kama chama kingine chochote kitakacho shika dola kikifanya upuuzi kama wa EPA, Meremeta, Richmond, Dowans nk. havitapigiwa kelele na Wana-JF? nadhani huo utakuwa ushahidi dhahiri kama ikiwa hicho chama kitakuwa Chadema.
  • Kwanini CCM haitaki kukubali makosa yake halisi na kujirekebisha? Wale waliomuelewa vyama Msekwa watwambie iwapo kumziba mdomo anayesema makosa yako kunakufanya uonekane msafi na kufuta hayo makosa uliyofanya ambayo yanasemwa.
  • Je wale wana-JF waliojiunga kwa lengo la kutuchunguza wengine na kubaini tupo wapi na sisi ni wakiana nani hasa, pia ni Chadema? Maana wapo na tunawajua! Kama hawa si Chadema Je JF ni mali ya hao Jamaa? au hapa Msekwa na kundi lake wanataka kutwambia nini?
  • Kwanini Msekwa hakusema JF ni adui wa Rostam Azizi, Edward Lowassa na Jakaya Kikwete? hivi kati ya haya makundi mawili ya hawa jamaa Watatu (LA, EL na JK) na CCM ni kundi lipi lililo lalamikiwa sana na JF kuliko lingine?

CCM ina nafasi nzuri ya kuitumia JF na kujijenga kuliko Chadema, maana Chadema haina Dola, Haikusanya Kodi, Haina mamlaka ya kuchunguza na kupereka mahakamani makosa ya Ufisadi yanayoainishwa ndani ya JF, Siyo JF wala Chadema iliyo mwandikia Kikwete hotuba inayosema hawajui wamiliki wa Dowans!, JF haikumtuma Kikwete kwenda kubembea Cuba, nk.

JF itaendelea kuwepo maana ni Mawazo na Akili za Watanzani, hizo akili na Mawazo yataendelea kuwepo hata kama kunamtu atajaribu kuiziba, anaweza kuleta mafuriko makubwa zaidi na yenye athari kubwa zaidi, hatujui approach itakayo kutumika au ambayo ingetumika iwapo JF hisinge likuwepo, maana njia za kudai uhuru wa kweli zipo nyingi, kama CCM hawataki hii ya mjadala na amani labda wanataka ile ya risasi na vita!

Kama hamtaki tuwachambue basi kaeni pembeni muipishe Chama itakayo kuwa tayari kuchambuliwa na wananchni wake. Maana yanayo ongelewa humu JF kama yangelikuwa yanaongelewa na Barozi CCM ingelikuwa imechukua hatua siku nyingi sana iliwapate kuendelea na ruzuku.
 
Superman na mwenzake Kichuguu walichimba biti la kumburuza Msekwa mahakamani lakini sasa jiiiiii...hatujasikia tena kinachoendelea. Wajanja wa mambo tulijua ilikuwa ni maneno tu.
 
Basi na wenyewe waanzishe mtandao utakao kuwa Anti Jamii Forums na Anti Non Rulling Political Parties.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom