Mkuu Pasco;
This is very useful . . . .
Je unafahamu chochote juu ya Cyber Law ya Tanzania?
SM
Super Man,
Kwanza nakupongeza sana kwa juhudi zako kuhakikisha jf, inapata haki dhidi ya shutuma hizi.
Naunga mkono asilimia 100%, kwenda mahakamani kudai fidia, lengo letu likiwa sio kupata mafao ya tozo, bali kulinda heshima yetu.
Tanzania hatu legistalation yoyote ya cyber law. Sheria zetu zote, zimetokana na sheria za Mwingereza, comon law ambazo walizikopi na kuzipeleka Afrika kusini ilipopata uhuru wake 1912, na baadaye India ikazikopi ilipopata uhuru wake 1948, na Tanzania tocacopy zile sheria za India para-material (neno kwa neno bila kubadili kitu). Wenzetu India, wameshazibadili za kwao na kujumuisha cyber law, sisi bado.
Pamoja na kutokuwa na specific cyber law, tumeshapitisha vifungu kadha wa kadha vyenye kuruhusu prosecution ya cyber crimes kupitia several The Written Laws (Miscellaneous Amendments) na pia kupitia baadhi ya shria mpya tulizoshinikizwa ikiwemo anti-terrosism act.
Wanasheria wamegawanyika sehemu nyingi, wale wenye kushughulikia kesi mbalimbali za madai ya mahakamani, wanaitwa wanasheria waitwa wanasheria wa litigations, na miongoni mwa kesi zinazosumbua mahakamani kuliko kesi nyingine zote, ni kesi za madai ya defamation na libel, zinapoteza muda mrefu na nyingine huishia kutoshinda. Mawakili wa kesi za namna hii nchi za wenzetu, wanatumia mtindo unaitwa 'No Win No Fee', yaani wakili atalipwa tuu baada ya kushinda kesi, ila mgao wake unakuwa ni mkubwa hadi kufikia kugawana nusu kwa nusu (fifty fifty).
Kinachazifanya kesi hizi ziwe sumbufu, ni jinsi ya kuthibitisha umeumizwaje kiuchumi, mfani JF ikidai fidia ya bilioni 100, inatakiwa kuthibitisha kwanza thamani yake, is it woth 100 bilions?, pili kuthibitisha njia za mapato za jf zinatirisha mabilioni hayo, halafu ndipo una prove kuwa matamshi yale yameiangusha jf kimapato hivyo kustahili fidia husika.
Kwa vile lengo letu sio kupata faida ya kuichumi, bado tunaweza kufungua kesi kama ya Mengi na Manji, ambayo Manji anadai Shilingi Moja Tuu (1/=) ili kumthibitishia Mengi, lengo sio mafao bali kulinda heshima.
Gharama za wakili, sio issue sana, mimi naamini kuna mawakili watajitolea kyuibeba hii kesi free of charge. Kwa wenzetu ulaya, ili uweze kujenga jina, mawakili wanaochipukia, hujitolea kubeba complex cases wakishinda ndipo wanapotokea.
Mimi binafsi, sikuwahi kuwa na mpango wa kuwa wakili, lakini jf, ime ni inspire sana, mpaka nimetamani, ningekuwa wakili, ningeibeba hii kesi free of charge, na ninaamini kwa asilimia 100 tungeshinda!.