Hapana jamani twende mbele turudi nyuma,
Nimechunguza maudhui ya hili gazeti nimegundua yanawakilisha kundi lililo ndani ya chama ambalo limeathirika na ujio wa Mwenyekiti mpya.
Kundi ambalo lilikuwa linanufaika na udhaifu wa serikali iliyopita, mirija imekatwa sasa wanaanza chokochoko kwa mgongo wa wananchi kuwa hawana imani na rais kumbe wao ndio hawana imani na Magufuli kama atalinda maslahi yao. Tuseme Hapana.
Haiwezekani Magufuli kaza uzi, ukiona mtu anapiga kelele gizani juwa jiwe limempata.
Ni kweli maisha yanakuwa magumu tutaumia kwa kipindi kifupi lakini binafsi bado nauona mwanga huko mbeleni.
Wananchi tuweni na akili za uchambuzi, wale waliofanya maisha yetu yawe duni kwa kujitajirisha wao na watoto wao ndio hao hao wanataka kutumia hali ngumu iliyopo kufifisha jitihada za rais.
Inakuwaje hali ngumu yetu waione leo kwani awamu iliyopita tulikuwa na hali nzuri?
Kwa hili niko na rais, he is doing a wonderful job ambayo haikuwahi kuonekana awamu iliyopita, ni wavivu, wazembe, wezi, waliozoea madili tu ndio watakaomwona hafai.