Jamani TBC hii ni sawa kweli? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jamani TBC hii ni sawa kweli?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Bishanga, Sep 23, 2011.

 1. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #1
  Sep 23, 2011
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  Ni saa mbili kasoro usiku mko sebuleni na watoto mnasubiri taarifa ya habari TBC mara linarushwa tangazo la biashara ya bidhaa za kinamama za kujisetiri.Tangazo linaanza mara oh inanyonya unyevunyevu,mara inakausha haraka na kaza wa kaza.Hivi mtoto akikuuliza mama/baba hii nini unamjibuje? Wadau mimi nauliza kwa nia njema kabisa hivi ni sahihi kweli matangazo ya aina hii yarushwe primetime?
   
 2. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #2
  Sep 23, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Mkuu never ever do that again
  Kukaa na watoto wako sijui na mke wako na wageni sebuleni mnaangalia Tv kwa pamoja hasa hizi tv za wabongo ambazo kwao tangazo lolote linatolewa hata kama linaviolate the rules
  tafuta hata kiTV chako cha inc 14 ukiweke rum uangalie na mkeo
  utakuja umbuka siku moja wanaweka tamthilia zao hizi wanaonyesha jamaa wanavuana nguo wanapanda kitandani kwa mahaba na uko na mama mkwe wako mnaangalia au na mtoto wako mdadisi anakuuliza mbele ya mama mkwe eti dady wale wanafanya nini
  Sijui utakimbilia wapi au utajiuma uma na kuipotezea
  Ila hapo ujue aibu tayari
   
 3. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #3
  Sep 23, 2011
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  we acha tu Mkuu.
   
 4. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #4
  Sep 23, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,971
  Likes Received: 2,967
  Trophy Points: 280
  Utandawazi huo.
   
 5. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #5
  Sep 23, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180


  Rocky ila once in a while kaa kando jifanye unasoma gazeti observe
  wanaoa channels wanachagua na kutafuta... na pia maongezi yao
  dhidi ya vipindi... inakupa saana picha level ya mwanao ya kufikiri iko
  vipi na mambo gani likely anajua....
   
 6. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #6
  Sep 23, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280

  Nakubaliana na wewe si kwamba uabandon sebule yako kabisa
  Ila sometime unakaa nao kwa muda mfupi uangalie ni nini anachoangalia na ni vipindi gani anapenda
  na mtizamo wake kwenye vipindi vya tv ukoje na nini anachojifunza humo
  Ni kwa muda mfupi ili usije kuumbuka maana mwanangu wa kiume akiona tounge kiss ananiambia dady ile mbaya
   
 7. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #7
  Sep 23, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180

  ........lolz.... Nimekupata... tuko pamoja!
   
 8. N

  Nehondo JF-Expert Member

  #8
  Sep 23, 2011
  Joined: Aug 14, 2011
  Messages: 311
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  unachosema ni sawa ila pia ni wajibu wa wazazi kuwalinda watoto na TV. ikiwezekana watoto wawe wanaangalia vipindi vya watoto tu
   
 9. Tausi.

  Tausi. Senior Member

  #9
  Sep 23, 2011
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 125
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kaka unavyosema ni kweli lakini sasa hata kama sebuleni amemwacha mama mkwe na watoto inamaanisha taarifa ya habari hawataangalia, au ndio wataweka cd tu kila kukicha, na unakuta miongoni mwa watoto wako yupo mmoja anapenda sana kuangalia taarifa ya habari ili ajue yaliyojiri duniani, kusemakweli mkuu hivi vyombo vya habari havijari hilo, na hili ni hatari kwa taifa zima, matangazo kama hayo wangekuwa wanayaweka usiku wa manane. Au mwasemaje waungwana.
   
 10. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #10
  Sep 23, 2011
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  yaani mimi nachoka kabisa,i hope watu wa TCRA wanaingia humu mmu.
   
 11. s.fm

  s.fm JF-Expert Member

  #11
  Sep 23, 2011
  Joined: Jul 8, 2009
  Messages: 669
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Lakini mkuu hii si kwa TBC peke yake...inatokea kwa almost TV zetu zote iwe za bongo na hata za nje pia! na hizi movie zetu za kibongo ambazo pengine watoto na wanawake ndio hupendelea sana, siku hizi mambo hayo ndio nje nje! kwakweli bora kuwa na ka-Tv kako chumbani...maana waweza umbuka ati..oohooo!
   
 12. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #12
  Sep 23, 2011
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  yaani Asha malezi ya kileo kwenye utandawazi kaaaazi kweli kweli.
   
 13. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #13
  Sep 23, 2011
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  kama walivyosema wakuu hapo juu ndo umekaa na ma mkwe,lol!
   
 14. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #14
  Sep 23, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Nakubaliana na wewe na nakubaliana na mawazo yako
  Tatizo nu kuwa hatujui tume ya mawasiliano inafanya nini au TCRA huwa hawaangalii vipindi vinavyorushwa na hizi tv
  Maana kuna tamthilia ambazo zinaonyeshwa kwenye tv hizi zina mabo ya wazi ya mapenzi ila zinaonyeshwa mchana kweupe na sio hata kwa wale may be wenye cable wala dstv au star times ni hizi station za kawaida kama tbc au star tv au channel ten
  Ila zinaachwa zikiwa na the same episode za mapenzi
  Ni ngumu sana kucontrol haya mambo haswa wakati wewe unapambana kutafuta maisha mfanyakazi wako wa ndani yeye yuko kwenye tv na watoto wako wanaangalia tamthilia au movie za kinigeria ambazo nyingi zina masuala ya mapenzi
   
 15. ChaterMaster

  ChaterMaster JF-Expert Member

  #15
  Sep 23, 2011
  Joined: Aug 17, 2009
  Messages: 1,290
  Likes Received: 409
  Trophy Points: 180
  unajua shida ni kwamba sisi weusi tumeletewa mambo ya utandawazi haraka haraka bila kujipanga ndio maana lazima yatutokee mdomoni kama sio puani, wenzetu weupe kwao vitu kama hivi sio ishu kabisaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!!!!!!!!!!!!!!
  Wakiamua hata uwanjani kweupeeeeeeeeeeeeee wanafanya lolote kama vile wapo chumbani.
   
 16. s.fm

  s.fm JF-Expert Member

  #16
  Sep 23, 2011
  Joined: Jul 8, 2009
  Messages: 669
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Ndio watu wa TCRA wanaweza kutusaidia kiasi katika hili...lakini wakati mwingine lazima tuangalie uhalisia wa kitu kuliko kuhangaika kutafuta mchawi ni nani! utandawazi ndio ushaingia hivyo na ni vigumu sana kupingana nao...sasa tatizo jingine ni huku kwenye familia zetu tunashindwa ku-control discipline kwa watoto, ndio tunaweza kusema labda tamthilia fulani zianze kuoneshwa saa tano, cha ajabu huo muda unakuta watoto hata lile wazo la kwenda kulala hawana na wazazi wanaangalia tu! TV zingine huweka parental control (mwongozo wa familia) kwa mfano 13, 16 au 18 lakini huwa tunaona lile kama pambo vile...! kazi ipo
   
 17. Makindi N

  Makindi N JF-Expert Member

  #17
  Sep 23, 2011
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 1,068
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Kwakweli condom na pad adverts in peak hours blitz embarrasses....... Na watoto wa siku hz walivyo wadadisi na wasiotaka kupitwa na kitu, maswali wanayoyafurumusha wakati mwingine naona yanawazidi umri...... Inapelekea hata taarifa ya uangalie chumbani..... Kazi kweli kweli......
   
 18. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #18
  Sep 23, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180

  Kitu ambacho wazazi tunakosea ni ile hali ya kufikiri kua tukiwaachia watoto wawe
  modern moja kwa moja ndo usasa... haya mambo ya media haya inabidi kua makini saana.
   
 19. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #19
  Sep 23, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Kweli inabidi kuwa makini sana na kuwa karibu nao kila wakati kujua hata ule muda ambao hukuw anyumbani ni nini walichhokiona kwenye media
  naamini huwezi kupingana na ukweli ila inabidi kuwa makini na kila linaloendelea kwa mtoto
   
 20. Likwanda

  Likwanda JF-Expert Member

  #20
  Sep 23, 2011
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 3,854
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Dah, huwa nakerekwa sana pale Shaa anaposema "ninapokuwa katika siku zangu", kwanza huwa naona kinyaa, pili wakati mwingine ndio hivyo tupo sebuleni tunaangalia taarifa ya habari yaani siangalii habari ya 2usiku Kupitia TBC kama kunamchanganyiko wa kifamilia.
   
Loading...