Bishanga
JF-Expert Member
- Jun 29, 2008
- 15,323
- 10,050
Ni saa mbili kasoro usiku mko sebuleni na watoto mnasubiri taarifa ya habari TBC mara linarushwa tangazo la biashara ya bidhaa za kinamama za kujisetiri.Tangazo linaanza mara oh inanyonya unyevunyevu,mara inakausha haraka na kaza wa kaza.Hivi mtoto akikuuliza mama/baba hii nini unamjibuje? Wadau mimi nauliza kwa nia njema kabisa hivi ni sahihi kweli matangazo ya aina hii yarushwe primetime?