Jamani hapa kuna mapenzi kweli?

Jamani hapa kuna mapenzi kweli?

mkuu huyu mtoto ni pisi na nusu na kuna vigezo vyangu (kimuonekano na tabia kidogo) amevikamilisha. Nilikua nataka nijitambulishe kwao ili nisije kumkosa. Lakini amenikatisha tamaa kabisa.
Kijana acha papala na Mapepe tuliza akili acha pupa huyo mwanamke kasha kusoma ila wewe huja msoma bado

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
 
Huyu mwanamke nilikutana nae miezi mitatu iliyopita nikiwa katika harakati zangu za kikazi mkoa flani. Alinivutia muonekano wake na tabia (napenda wanawake wapole). Tukaanza mahusiano baada ya wiki mbili za kufahamiana. Mkoa aliopo anaishi kwa ndugu.

Umri ana miaka 25. Anafanya kazi kiwanda cha wahindi. Hawamlipi vizuri kutokana na maelezo yake na kazi anafanya siku sita za wiki, masaa 12 kwa siku. Hua anapewa siku moja tu ya kupumzika. Kwahyo ili tuwe tunaonana inalazimika mimi ndio niwe nasafiri kila napopata nafasi kwa vile tunaishi mikoa tofauti ni umbali wa masaa matatu kati yetu.

Tatizo binti shida hazimkauki. Binti anaomba sana ela. Kuanzia pesa ya nauli ya kwenda na kurudi kazini. Vocha. Kula. Mahitaji yake yote lazima aombe kubustiwa. Nimepiga hesabu kwa wiki pesa ndogo akiomba ni elfu 80, hua haipungui hapo. Sasa hivi ameomba nimpangie chumba nimnunulie na furniture ili tuwe tunakutana kwa uhuru tofauti na hivi tunavyokutana lodge kila nikija.

Kwahiyo nilimkalisha chini. Mshahara wangu haujui lakini ni zaidi ya mara tisa ya ule anaopokea yeye. Nikampa wazo anipe utaratibu nikajitambulishe kwao wanijue. Then aje tuishi wote huku tukitafta project iwe ya biashara au chochote ambacho ataweza kufanya akiwa huu mkoa niliopo mimi kuliko kuendelea kufanya kazi ambayo haimlipi huku akizidi kuniingizia unnecessary costs. Mipango ya ndoa then iendelee.

Amegoma katakata. Anadai kwa sasa kuishi na mwanaume ni mapema mno. Anataka kua independent awe na chumba chake, afanye kazi zake na maisha mengine. Nimemuambia kama haiwezekani basi kila mtu aendelee na maisha yake kuliko kupotezeana mda. Analia. Analalamika nimemchezea. Eti simpendi na simjali na nimebadilika! Binafsi nimeshindwa kumuelewa!
Mwanamke anakupenda sema ataki kuolewa na kuwa tegemeze kwako ndomana anaogopa kuolewa, ila anataka nae awe na maisha yake kabla ya kuingia kwenye ndoa. ndomana anakuambia ni mapema alafu muda mmekutana bado mapema kumwambia mwanamke maswala ya ndoa.

Usahuri wangu husimuache bado mapema ongea nae vizuri na endelea kumshawishi kumuondolea ofu ya kukuamini zaidi ili iwe rahisi kukubaliana na mawazo yako.

Huyo shida alio nayo ni kwamba hataki kuingia kwenye ndoa alafu amtegemee mwanaume. ongea nae vizuri
 
Kwann mm ndo nifate yako na kwann we usifate yangu wakti wew ndo ulinitongozaaa kuna design ya wanawake hawapendi kuendeshwa kbs yaan bora tuelewana sio kunipelekesha my dear
Tatizo siyo kukataa kuolewa tatizo yeye kutaka kupagiwa chumba na kununuliwa vitu vya ndani, vijana ambao hawaja owa wanashangaa ni jambo gani kwa jamii yetu kijana ambaye hajao kumpangia chumba mpenzi wake na kumnunulia vitu vya ndani na kumpa pesa za matumizi ni maajambo, yani ata mimi kama mzazi niende kwa binti yangu nikute kapanga chumba cha bei kubwa na ana vitu vya gharama na mshahara wake wa mbuzi lazima nitajua ana jiuza ni kahaba tu.huyo binti atafute mume wa mtu ndiyo atafanyiwa hayo anayo yataka kwasababu atakuwa mchepuko wa mume wa mtu, lakini kwa kijana ambaye hajaoa hawezi kukubali kufanywa dodocha.

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
 
Hawa viumbe ni kuishi nao Kwa akili mkuu. Mimi ninae mmoja, wakati namtongoza alikua anaishi na dada yake. Baadae akaniambia anataka kupanga Kwa sababu mdogo wake anakuja na angependa aishi nae. Nikampa Hela ya kupanga ila kushangaza imepita miezi miwili sioni mdogo wake akija. Nimepiga pin kwake anaenda Kwa mwezi mara Moja na kodi analipa mwenyewe. Nimemuachs aendelee kulipa Kodi ya bure mpaka akili yake imkae sawa lakini siwezi kulipa Kodi wakati nyumba ninayo
Kodi ya bure kivipi wakati yeye anaishi.

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
 
Dah na mimi nina wangu mmoja nilikutana nae nikiwa intern na yeye alikua chuo, naye ni mchagga na anaumri huohuo . Mzuri na anamuonekano wa upole.
Alikua kapangishiwa na jamaa mmoja ni anafanya kazi Dodoma. Mimi nilikua nakaa nyumbani kwa hiyo tulikua tunakutana pale alipopangishiwa(nilikua sijui kama kapangishiwa na jamaa yake maana aliniambia wazazi wake ndo wanalipa). Nilikaa naye miezi 2 ndo akaniambia ukweli, akaniambia kuhusu wazazi wake kumpa hela ndogo ya matumizi, akaniambia kuhusu yeye kutembea na wanaume wengi kwa ajili ya kupata hela na akaniambia ananipenda anataka nimuoe na akanitambulisha kwa ndugu zake. kiukweli nilimpenda sana ila nikapunguza malengo yangu kwake maana niliona kama hana uvumilivu na mimi maisha yangu bado najitafuta.
Saivi yupo huko mikoa ya kusini anafanya biashara na anakaa kwa ndugu yake kama by any chance akawa unamzungumzia ni yeye bro kimbia.
 
Hapo hamna machozi ya kweli,
Hayo Ni machozi ya kimkakati baada ya wewe kuonesha msimamo wako halisi.

Huyo mwanamke anakutumia,
Na hayo machozi anajaribu kumanipulate akili yako.

Kiufupi,
Huyo mwanamke Ni mamaJ type
Jinsi ya kuishi nae, njoo nikufundishe mimi
 
Amegoma katakata. Anadai kwa sasa kuishi na mwanaume ni mapema mno. Anataka kua independent awe na chumba chake, afanye kazi zake na maisha mengine.
Mpaka hapo hujaelewa tu? Wala hukuhitaji kuja huku

Keshakuona fala chuma ulete. Just move on. Hiyo 80K ungekuwa unampa mzazi/mlezi wako kila week, baraka zako zingefurika
 
Huyu mwanamke nilikutana nae miezi mitatu iliyopita nikiwa katika harakati zangu za kikazi mkoa flani. Alinivutia muonekano wake na tabia (napenda wanawake wapole). Tukaanza mahusiano baada ya wiki mbili za kufahamiana. Mkoa aliopo anaishi kwa ndugu.

Umri ana miaka 25. Anafanya kazi kiwanda cha wahindi. Hawamlipi vizuri kutokana na maelezo yake na kazi anafanya siku sita za wiki, masaa 12 kwa siku. Hua anapewa siku moja tu ya kupumzika. Kwahyo ili tuwe tunaonana inalazimika mimi ndio niwe nasafiri kila napopata nafasi kwa vile tunaishi mikoa tofauti ni umbali wa masaa matatu kati yetu.

Tatizo binti shida hazimkauki. Binti anaomba sana ela. Kuanzia pesa ya nauli ya kwenda na kurudi kazini. Vocha. Kula. Mahitaji yake yote lazima aombe kubustiwa. Nimepiga hesabu kwa wiki pesa ndogo akiomba ni elfu 80, hua haipungui hapo. Sasa hivi ameomba nimpangie chumba nimnunulie na furniture ili tuwe tunakutana kwa uhuru tofauti na hivi tunavyokutana lodge kila nikija.

Kwahiyo nilimkalisha chini. Mshahara wangu haujui lakini ni zaidi ya mara tisa ya ule anaopokea yeye. Nikampa wazo anipe utaratibu nikajitambulishe kwao wanijue. Then aje tuishi wote huku tukitafta project iwe ya biashara au chochote ambacho ataweza kufanya akiwa huu mkoa niliopo mimi kuliko kuendelea kufanya kazi ambayo haimlipi huku akizidi kuniingizia unnecessary costs. Mipango ya ndoa then iendelee.

Amegoma katakata. Anadai kwa sasa kuishi na mwanaume ni mapema mno. Anataka kua independent awe na chumba chake, afanye kazi zake na maisha mengine. Nimemuambia kama haiwezekani basi kila mtu aendelee na maisha yake kuliko kupotezeana mda. Analia. Analalamika nimemchezea. Eti simpendi na simjali na nimebadilika! Binafsi nimeshindwa kumuelewa!
Single mother mtarajiwa huyo.
 
Back
Top Bottom