Jamani hapa kuna mapenzi kweli?

Jamani hapa kuna mapenzi kweli?

Hapo hamna machozi ya kweli,
Hayo Ni machozi ya kimkakati baada ya wewe kuonesha msimamo wako halisi.

Huyo mwanamke anakutumia,
Na hayo machozi anajaribu kumanipulate akili yako.

Kiufupi,
Huyo mwanamke Ni mamaJ type
Jinsi ya kuishi nae, njoo nikufundishe mimi
mamaJ type! Nimeshampiga chini aisee. Nimeblock kila kitu najua hili nalo litapita tu
 
Dah na mimi nina wangu mmoja nilikutana nae nikiwa intern na yeye alikua chuo, naye ni mchagga na anaumri huohuo . Mzuri na anamuonekano wa upole.
Alikua kapangishiwa na jamaa mmoja ni anafanya kazi Dodoma. Mimi nilikua nakaa nyumbani kwa hiyo tulikua tunakutana pale alipopangishiwa(nilikua sijui kama kapangishiwa na jamaa yake maana aliniambia wazazi wake ndo wanalipa). Nilikaa naye miezi 2 ndo akaniambia ukweli, akaniambia kuhusu wazazi wake kumpa hela ndogo ya matumizi, akaniambia kuhusu yeye kutembea na wanaume wengi kwa ajili ya kupata hela na akaniambia ananipenda anataka nimuoe na akanitambulisha kwa ndugu zake. kiukweli nilimpenda sana ila nikapunguza malengo yangu kwake maana niliona kama hana uvumilivu na mimi maisha yangu bado najitafuta.
Saivi yupo huko mikoa ya kusini anafanya biashara na anakaa kwa ndugu yake kama by any chance akawa unamzungumzia ni yeye bro kimbia.
Huyu hayupo mikoa ya kusini
 
Miezi mi3 unataka umpangie chumba kwanza unaishi nae mbali huwenda ndani ya hiyo miez mi3 umekutana nae Mara 5 tu na umeshalipa nauli elfu 80 kwa wiki 12 bado kuna hela zingine nyingi tu umepigwa ila kwa aibu huwezi kuzisema.
Utaliwa sana hela we endelea kusema nimetaka kumuacha analia, kulia kwenyewe tukikuuliza umemuona kwa macho yako akilia? Utatujibu alikutumia Emoji
 
Inaonekana upendi msaada maana utoi majibu sahihi...!! Jibu nimekuuliza hapo juu nikufungulie hyo code.
 
Huyu mwanamke nilikutana nae miezi mitatu iliyopita nikiwa katika harakati zangu za kikazi mkoa flani. Alinivutia muonekano wake na tabia (napenda wanawake wapole). Tukaanza mahusiano baada ya wiki mbili za kufahamiana. Mkoa aliopo anaishi kwa ndugu.

Umri ana miaka 25. Anafanya kazi kiwanda cha wahindi. Hawamlipi vizuri kutokana na maelezo yake na kazi anafanya siku sita za wiki, masaa 12 kwa siku. Hua anapewa siku moja tu ya kupumzika. Kwahyo ili tuwe tunaonana inalazimika mimi ndio niwe nasafiri kila napopata nafasi kwa vile tunaishi mikoa tofauti ni umbali wa masaa matatu kati yetu.

Tatizo binti shida hazimkauki. Binti anaomba sana ela. Kuanzia pesa ya nauli ya kwenda na kurudi kazini. Vocha. Kula. Mahitaji yake yote lazima aombe kubustiwa. Nimepiga hesabu kwa wiki pesa ndogo akiomba ni elfu 80, hua haipungui hapo. Sasa hivi ameomba nimpangie chumba nimnunulie na furniture ili tuwe tunakutana kwa uhuru tofauti na hivi tunavyokutana lodge kila nikija.

Kwahiyo nilimkalisha chini. Mshahara wangu haujui lakini ni zaidi ya mara tisa ya ule anaopokea yeye. Nikampa wazo anipe utaratibu nikajitambulishe kwao wanijue. Then aje tuishi wote huku tukitafta project iwe ya biashara au chochote ambacho ataweza kufanya akiwa huu mkoa niliopo mimi kuliko kuendelea kufanya kazi ambayo haimlipi huku akizidi kuniingizia unnecessary costs. Mipango ya ndoa then iendelee.

Amegoma katakata. Anadai kwa sasa kuishi na mwanaume ni mapema mno. Anataka kua independent awe na chumba chake, afanye kazi zake na maisha mengine. Nimemuambia kama haiwezekani basi kila mtu aendelee na maisha yake kuliko kupotezeana mda. Analia. Analalamika nimemchezea. Eti simpendi na simjali na nimebadilika! Binafsi nimeshindwa kumuelewa!
Huyo anahitaji backup yako tu kutumiza mahitaji yake akifanikiwa atakutupa kama used condom😅
 
Vijana mnaendekeza sana mapenzi kuliko kazi nyie ndio mnafanya wengine tuonekane wapuuzi yaani mwanamke mpaka anakuona zoba.
 
Mkuu hapo ni mkoani,arusha?? Ulizia vzuri huyo dada ajawai kuishi na mtu before na je? Ajazalishwa
Sorry hajawahi kuzalishwa. Alikua na boyfriend huko chuoni ambae aliishi nae kigetto getto ila jamaa ameshaoa. Hili nina uhakika nalo.
 
Baada ya mikausho mikali naona ameamua kua mpole. Habari za kupangiwa chumba hana tena!
Screenshot_20221230-082208_2.jpg
 
Back
Top Bottom