Jaji Mkuu apata dawa mlundikano mashauri, ashauri majaji wapangiwe idadi ya kesi za kumaliza kwa mwaka

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,314
5,478
JAJI Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahimu Juma, amesema kuna haja ya kuweka utaratibu wa kila Jaji wa Mahakama ya Rufani kumaliza idadi fulani ya mashauri kwa mwaka ili kuondoa mlundikano wa mashauri mahakamani.

Alitoa kauli hiyo jana wakati wa mkutano wa nusu mwaka wa Majaji wa Mahakama ya Rufani uliofanyika mjini hapa, akibainisha kuwa mahakama haijaweka kiwango, bali unatumika utaratibu wao wa muda mrefu tangu mwaka 1979, yaani miaka 43 iliyopita.

Alisema, utaratibu huo hufanyika kila kinapoketi kikao cha Mahakama ya Rufani kinapaswa kumaliza mashauri yote yanayopangwa katika kikao husika isipokuwa kama kuna sababu zisizozuilika za kutokumaliza shauri husika ambapo pia hawakufikia malengo.

Alisema takwimu zinaonyesha kuwa Mahakama ya Rufani ina mashauri ya muda mrefu 611 na mashauri 42 yanayosubiri kusomwa hukumu yaliyozidi siku 90.

Alisema vigezo vya kupunguza mlundikano wa mashauri mahakamani vinalenga kushusha mlundikano hadi asilimia 0.05 ambapo tayari wamefanikiwa kushusha kwa asilimia 0.15 na kwamba lengo kuu ni shauri liwe mahakamani ndani ya siku 350.

Alisema wako vizuri katika kutekeleza hilo, sasa shauri linadumu mahakamani kwa wastani wa siku 338.

Jaji wa Mahakama ya Rufani, Augustine Mwaliga, alisema kikao hicho kimefanyika mwaka huu baada ya kutokufanyika kwa miaka miwili mfululizo iliyosababishwa na janga la UVIKO-19.

Source: Nipashe
 
Tatizo sio uharakishaji wa kesi au mashauri...

Je sheria zinatfsiriwa sahihi?
Majaji na mahakimu wana uwezo wa kutafsiri sheria?

Majaji na Mahakimu wako huru kufanya maamuzi kwa kuzingatia sheria?

Je mahakama ni chombo huru?
 
Hizi ngonjera haziwezi isha leo Wala kesho matendo yanayo fanyika mahakamani na matendo ya majaji niya kihayawani kabisa,hakuna mtu mwenye akili timamu anaye ziamini mahakama na majaji.

Hata mazuzu siku hizi wasio tambua sheria wakisia hukumu za mahakama zinazo fanywa na majaji Wana baki midomo wazi.
 
Kuna nchi zingine mpk jumamosi,jumapili mahakama znafanya kazi

Ova
 
Back
Top Bottom