Jaji Mkuu: Mahakama kuhamia rasmi kwenye teknolojia mpya ya Unukuzi na Tafasiri (transcription and translations)

zandrano

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
7,160
7,734
Jaji Mkuu wa Tanzabia Profesa Ibrahim Hamisi Juma ameyasema hayo wakati akiwaapisha Mahakimu na Manaibu wasajili tarehe 11/12/2023, kuwa sasa Majaji na Mahikumu basi kuandika mienendo ya mashauri na hukumu kwa kutumia mkono badala yake itatumika teknolojia ya kisasa itakayo weza kunakli mienendo yote inayo jiri mahakamani.

amesisitiza kuwa vifaa hivyo vitafungwa kwenye mahakama zote za Tanzania na itasaidia kila mwananchi kupata hukumu kwa lugha ya kiswahili au kizungu, ameongeza kwa kusema kuwa mifumo hiyo itakuwa mwarobaini wa lugha ya kizungu kwani sasa lugha ya kizungu inaweza kutafasiriwa kwa kiswahili papo hapo.

Sisi wananchi tumefarijika sana kwa hatua hiyo iliyo fikiwa na mahaka ya kuhama kutoka kwwnye mifumo ya kizamani yaani analojia kwwnda kwenye mifumo ya kidijitali. Hii ni hatua kubwa sana na italeta mageuzi makubwa sana haswa kuharakisha haki za wananchi.

Shime mifumo hiyo sasa ifungwe haraka ili ianze kutumika kote nchini.

Majaji na Mahakimu wanao jifanya wao ni wazungu na sio Watqnzania sasa wabadilike watqmbue kuwa wana wahudumia wananchi ambao ni waswahili sio wazungu. Tuache kujifaragua kwa Kiingereza.

Sasa hatutegemei kuona hukumu za kizungu ambacho hatukielewi, kiswahili ndio lugha yetu ya Taifa.

Pongezi kwa Jaji Mkuu na timu yake yote.





View: https://www.youtube.com/live/X53mFTO8QPQ?si=OxjUOOqb0Jdx8yZJ
 
Back
Top Bottom