Jaji M.C. Othman Jaji Mkuu mpya wa Tanzania

Conflict of interest ipo wazi kabisa..Haiwezekani nafasi ya boss wa TISS na CJ kuchukuliwa na ndugu, ukitilia maanani maovu mengi yaliyofanywa hapa nchini huku TISS ikikaa kimya, hivyo kuondoa imani.
 
Hivi hapa hakuna conflict of Interests... AU NI MIMI TU, NA MAWAZO YANGU YA KIZAMANI.......??????


Hiyo conflict of interest unaona wewe lakini tukisema kwamba UTEUZI WOWOTE WA CCM NI SHARTI KUFWATE MKONDO FULANI na kwamba BILA VIJI-CONNECTIONS FULANI tunduni haujapita wengini wakawa wanadhani ni utani hapa.

Ni wachache mno wanaotazamwa kwa elimu, ufanisi wa kazi na uzalendo wake. Tukisema Dr Malecela kuna Katapila nyuma kama godfather hamsikii. Sasa ya Othman Chande wa TISS kutumia nafasi yake ya sasa kumpigia chapuo mtoto walioachiana ziwa wewe unaona shida gan??? Hata Jaji Makame majuzi alipofanya vizuri kwenye uchaguzi wetu mkuu tayari dogo lake Prof Makame yuko ndani ya ulingo Dodoma anakula good-time kwa 'Hundi ya Wazi' aliouandika kaka kule Tume ya Uchaguzi 2010.

Kwa kifupi, hapa ni Mega-Corruption Syndication, Nepotism, Favouritism and Bird-Feathering kwa kwenda mbele. Kaka JK kanyaga twende!!! Hapa hata gunia la mkaa linaweza kuteuliwa. Wala sitoshangaa Mzee Jangara akiteuliwa Balozi wetu kule Umoja wa Mataifa; kama ni kiingereza atajisomeaga huko huko kazini.

Hivi ndivyo mambo yanavyokwenda baba. Lile swali la rais wa zamani wa Marekani juu ya mtu kujiuliza ataifanyia nini taifa lake; hapa kwetu swali hilo ni kwamba MTU UMEWAHI KUKIFANYIA CCM AU NDUGU YAKO YUPI AMBAYE AMEWAHI KUIFANYIA NINI CCM na wala kuifanyia nini taifa na maslahi yake.

Bwanae, kwenye KATIBA MPYA HUKO rais apunguziwe kwa sana madaraka ya kupindukia kiasi hiki. There is too much President in our everyday lives. Nafasi hizi zote zitangazwe, mashirika makubwa na ya kuaminiko kwenye mambo ya ajira yashirikishwe kama mashirika matatu hivi kila kimoja kikifanya kazi yake kwa peke yake lakini kwa kipidi kimoja.

Mashirika haya yachuje majina kiutaalam bila kuingiliwa, kisha kila muombaji nafasi apewe mi-alama au marks kabla ya kupelekwa majina yaliochujwa (kama 6 hivi kwa nafasi husika) kupelekwa bungeni nako wakabakishwa watatu na kupewa alama mle upya na mwisho rais kupata mtu pale kwa nafasi husika.

Process itakapokua very transparent and most rigorous then accountability to the general publi and not merely the president will be most assured than is the case to-date.

Hivi hawa ni wale watoto wa yule Chande wa kwenye historia kuwemo kwenye Baraza la Mawaziri sio??? Ukweli ni kwamba maendeleo ya nchi hutegemea sana ufanisi wa taasisi zake.

Nako pia ufanisi huo ni lazima utokane na kiwango cha ubora katika kupatikana watendaji hawa. Sasa, tofauti na hapo ni makida makida tu twende kasi!!!
 
Hivi conflicts of interests ni kwa CJ kuwa muislamu au kuwa na ndugu TISS jiachieni tu?
 
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116539
E-mail: press@ikulu.go.tz
Website: www.mawasilianoikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425




PRESIDENT’S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.



TAARIFA KWA VYOMBO VHABA

Rais Jakaya Mrisho Kikwete, amemteua Jaji Mohamed Chande Othman kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania, kuanzia tarehe 28 DIsemba, 2010.

Jaji Othman anachukua nafasi ya Jaji Augustino Ramadhani anayestaafu kwa mujibu wa sheria tarehe 27 DIsemba, 2010.

Kwa sasa Jaji Othman ni Jaji wa Mahakama ya Rufaa na pia ni mtaalamu binafsi juu ya hali ya Haki za Binadamu huko Kusini mwa Sudan, hadi mwezi Agosti 2011.
Jaji Othman alizaliwa tarehe 1 Januari, 1952, ana shahada ya kwanza ya Sheria (LLB) ya Chuo Kikuu cha Dar-Es-Salaam na Shahada ya Uzamili (MA) kutoka katika Chuo Kikuu cha Webster, Geneva-Uswisi.

Amewahi kuwa Makamu wa Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Rwanda huko Arusha na amewahi kushika nafasi sawa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali huko Timor Mashariki.

Jaji Othman pia, amewahi kufanya kazi ndani na nje ya nchi katika Mashirika mbalimbali ya Kitaifa na Kimataifa kama vile Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDP) na Shirika la Msalaba Mwekundu.

Jaji Othman ataapishwa kesho tarehe 27 Disemba, 2010 katika viwanja vya Ikulu saa 4:00 asubuhi.

Imetolewa na Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi
Ikulu
Dar es Salaam
26 Disemba, 2010


kikwete ndiyo anachochea udini angalia sasa raisi makamu wake waziri wa ulinzi,mambo ya ndani,waziri wa fedha watu wote wa dini moja aoni aibu
 
Hata kama jamaa angekuwa qualified na ana busara kama Solomon (Suleimani)....... ilo la kwamba Boss wa TISS ni ndugu yake....., Linam disqualify kabisa.....
 
Sijakataa kwamba ni ndugu. lakini undugu wao hauhusiani na kazi watakazofanya. na wala hakuna ushahidi uliowekwa hapa kwamba eti Othmani wa TISS ndiye aliyechagiza kuteuliwa kwa huyu Ndg yake New CJ. kama unao ushahidi weka hapa

CRAP Majibu yako kijana!!!!

Uteuzi wa taasisi ya maamuzi na kutoa haki ndani ya taifa inapoanza kwa guu la kutiliwa mashaka, harufu ya udini, ushawishi kindugu toka TISS na kwa kuzingatia kiwango cha unyenyekevu kwa CCM, basi ujue zoezi zima limepoteza imani kwa wananchi sawa sawa taasisi za Jeshi la Polisi, TISS, NEC, na Ikulu zilivyowatoka watu rohoni na kutokuaminika tena!!!!!!!!!
 
Imefikia wakati imekua ni ngumu sana kwa nchi yetu kufanyika uteuzi wowote wa kiongozi bila kingizwa ktk context ya kidini. Lakin saa nyingine watu hutumia kigezo cha elimu au ukabila. Ni afadhali kukawa ni vigezo vinavyoeleweka vya mtu kupata mtu kupata cheo kama vile elimu na uzoefu wa ktk kazi, ambapo ktk hili nafikiri sifa hizo zipo.

Hoja nyingi zilizotolewa hazionyeshi ujengaji madhubuti wa hoja kua nini hasa tatizo. Kuna wale wanaodai kua huyu bwana ana uhusiano na Ndugu Othman again wanashindwa kutetea hoja yao ok kama mtu akiwa na uhusiano na kiongozi wa serikala lakin akawa na sifa za kutosha kwa kazi fulani hafai kuchaguliwa?

Wakati umefika wa kuacha ushabiki na kuyaangalia mambo kwa kina zaidi
 
kikwete ndiyo anachochea udini angalia sasa raisi makamu wake waziri wa ulinzi,mambo ya ndani,waziri wa fedha watu wote wa dini moja aoni aibu

hata festiledi ni dini moja na rais, walalamikaji bwana.
 
Mdogo wa Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa Jaji Mohamed Othman Chande ameteuliwa kuwa Jaji Mkuu.

Sijui naye ni mchakachuaji?
 
Kuna wale wanaodai kua huyu bwana ana uhusiano na Ndugu Othman again wanashindwa kutetea hoja yao ok kama mtu akiwa na uhusiano na kiongozi wa serikala lakin akawa na sifa za kutosha kwa kazi fulani hafai kuchaguliwa?
A conflict of interest (COI) occurs when an individual or organization is involved in multiple interests, one of which could possibly corrupt the motivation for an act in the other.

We huoni kwamba Boss wa TISS na JAJI mkuu ni sensitive positions ambazo kuwepo kwa mtu na kaka yake kuna raise the eyebrows
 
Ulitaka mteuliwa awe Jaji PETER JOHN JOSEPH?maana kina Othman hawajasoma

Whether awe John au Othmani lakini jamani si atafanya kazi kwa mujibu wa taratibu na kanuni? Hata we unayefurahia kwamba ameteuliwa wa dini yako kwani atakusaidia nini? we utabaki na shida/raha zako na wala hatahudumia watu wa dini fulani bali watanzania wote. Kwani sheria inasema watanzania wote ni sawa mbele ya sheria.
 
kikwete ndiyo anachochea udini angalia sasa raisi makamu wake waziri wa ulinzi,mambo ya ndani,waziri wa fedha watu wote wa dini moja aoni aibu

Mna mawaziri wangapi wakristo serikalini, who are the majority serikalini. Acheni kulia lia kusiko kuwa na maana Tatizo la baadhi ya watu ukungu wa chuki dhidi ya uislamu huwaziba hata kufikiri. Hawafikirii pengine huyo jaji Chande pengine ndio the most qualified. Kuhusu conflict of interest Uwezo Tunao amesema Tanzania imetawaliwa na Favouritism, nepotism na takataka kibao sasa kama TISS amemteua mdogo wake kuwa tungelianza kwanza kujiuliza mbona wengine wanateua ndugu zao, wake zao, bibi zao humu maofisini hatukemei?

Ah malalamiko mengine jamani tuwe wakweli badala kulia lia tu. Tumjadili Chande kwa merits and qualification badala kutengeneza a smear campaign against him.
 
Back
Top Bottom