Intuition, kwa jina jingine wanaiita inner voice au sixth sense, ipo kiroho zaidi. Unaweza ukawa umekaa zako, unakuta kuna sauti inaakuambia jambo, ambalo wakati mwingine, ukitumia reasoning unaona kama ujinga.
Iliwahi nitokea, ikaja sauti inaniambia, yule jamaa yako atakufa, ikanirejea siku tofauti, reasonung ikaniambia, ni mawazo ya kijinga. Baada ya mwezi mmoja, jamaa akapata ajali mbaya sana na kupata ukemavu, baada ya mwaka na ushee, akapata tukio jingine baya sana la kiafya tofauti na la mwanzo.
Kuna siku nimekaa, nilikuwa nina kibarua ofisi fulani, nikawa natoka niende likizo, kikaja kisauti kinaniambia ondoka na vitu vyako, maana patavunjwa hapa. Reasonung ilikataa maana hakukuwa na mpango wowote, katikati ya likizo, napigiwa simu jengo linavunjwa kwa sababu kadha wa kadha.
Intuition na reasoning havikai chungu kimoja.