🧠 Intuition vs Reasoning: Ipi Inapaswa Kuongoza?

🧠 Intuition vs Reasoning: Ipi Inapaswa Kuongoza?

Ok.
Kwenye "hamna maarifa kwenye mafanikio hapo nimekukataa".
Hakuna ndio, unayeweza kukataa hili sio wewe tu ila hata tukisema tupige kura humu ndani nusu na robo ya member wote wataikataa hii😂😂 ila ndio hivyo, maarifa yako yahawezi kuamua mafanikio yako, unaweza ukawa na maarifa tele kichwani ila ukafa maskini.
 
Intuition na reasoning zinapaswa kuongoza kwa kutegemeana kulingana na hali unayokabiliwa nayo.

Intuition (Hisia) iongoze kwenye dharura, hatari, na maamuzi ya kijamii au mahusiano ambapo maamuzi ya haraka yanahitajika.

Reasoning (Mantiki) iongoze kwenye maamuzi makubwa ya kifedha, biashara, au mambo mapya magumu yanayohitaji takwimu na utafiti.

Tumia intuition kupata wazo au mwelekeo wa kwanza, kisha tumia reasoning kuhakiki kama uamuzi huo unafaa.
 
Hello wana great thinkers 🧠

Blue Monday ✍️

Je, tunapaswa kuamini intuition yetu ya ndani bila kutumia reasoning?

Yaani ile umekaa tu pap... ukapata sauti au msukumo wa ndani unaokuambia usifanye jambo fulani halafu ukaamua kuitii bila kwanza kufikiria kwa kina na kuchambua sababu?

Umewahi kukutwa na hali kama hiyo?

Hebu tuzogoe tunapaswa kuitii kila sauti ya ndani bila kufanya reasoning?

Ni mara ngapi umeipuuza sauti yako ya ndani halafu baadaye ukajikuta kwenye matatizo?

Na ni mara ngapi umeisikiliza intuition yako, ukaacha kutumia reasoning, lakini baadaye ukajikuta kwenye matatizo makubwa zaidi?

Hebu tujiulize pamoja 👇

Kipi kina nguvu zaidi kati ya intuition na reasoning?

Je, hivi vitu viwili vinaweza kufanya kazi kwa wakati mmoja?

Au vinafanya kazi pamoja
Ila hatutambui?

Na kama vinaweza, unawezaje kutumia intuition na reasoning kwa pamoja ili kufanya uamuzi bora zaidi?

Pia mtu mwenye uelewa
Atuambie nini maana ya intuition kwa kina
Na nini maana ya reasoning kwa kina

Maoni yangu kidogo kuhusu mada :

Mimi binafsi ni mara kadhaa nimepuuza sauti ya ndani na kuanza kutumia reasoning pekee ambayo sasa sielewi nakua nashindwa kufanya uchambuzi kwa kina au kwa usahihi na kujikuta nimefanya makosa then baadae nagundua huenda ningetumia vyote the same time lakini inakua too late

So mimi naamini kutumia reasoning ni bora sana bila kupuuza intuition yako

Karibu kwenye Chemsha Bongo



ShesRise_1. 🧠 ✋️

Mkuu nimekukubali, upewe medali zako tuu🎖️🏅🎖️🏅.

Just to ask??? Huwa unatumia haya majani(w**d) joking

You are good at reasoning, seems like you got so much time to observe everything that goes around you & you're surrounding. This is the highest level of intelligence someone have. I real like it and love it.

Back to the topic.

Cha kwanza ni INTUITION maana mambo yote huanza ndani ya mtu. ( Mtu ajionavyo nafsini mwake ndivyo alivyo). Kwa hiyo kwa vyovyote vile mtu anavyoonekana nje bhasi na ndani ndivyo alivyo.
Ikiwa mtu alivyo ndani ni tofauti na nje bhasi REASONING yake haipo vizuri.

Binafsi naweza kusema kwamba INTUITION ndio hunipa sababu ya kuREASON.
 
Asa mkuu utakuaje na reasoning bila kuwa na intuition?

It means lazma uwe na intuition itayo kufanya ufikie reasoning!!

Mfano unaweza kuwa na biashara yako lakini ukawa na wasiwasi kwamba kunakitu hakipo Sawa sindyo ? Hii hali ya kuhisi tayari ni intuition.

Then baada ya kuhisi ndo tutafwatia reasoning je naweza amua nini juu ya hali ninayo kuwa na wasiwasi nayo.

Then utafanya decision baada ya reasoning lakini always intuition comes 1st.

ShesRise_1
Mimi ndio manaa nauliza hivi vitu haviwezi kufanya kazi kwa pamoja?
 
Intuition huwa n mfano wa taa kwenye njia ambayo reasoning anapaswa kupita.

Namaanisha intuition ni anguko ikiwa huwezi kuifanyia crossing kama TAL😁

Why??
Sababu Kuna sauti tatu ndani yako ambazo zote zina sound the same (kwa mtu ambaye hajui mambo hayo)

Kwahyo lazima uwe na reasoning kabla kujafata kichwakichwa..... kwenye hizo sauti ni moja pekee ndio Gold✍️
Zingine mabalaa matupu
Naunga mkono hoja
 
Intuition na reasoning zinapaswa kuongoza kwa kutegemeana kulingana na hali unayokabiliwa nayo.

Intuition (Hisia) iongoze kwenye dharura, hatari, na maamuzi ya kijamii au mahusiano ambapo maamuzi ya haraka yanahitajika.

Reasoning (Mantiki) iongoze kwenye maamuzi makubwa ya kifedha, biashara, au mambo mapya magumu yanayohitaji takwimu na utafiti.

Tumia intuition kupata wazo au mwelekeo wa kwanza, kisha tumia reasoning kuhakiki kama uamuzi huo unafaa.
Shukran sana mkuu
Vipi hivi viwili haviwezi kufanya kazi kwa pamoja?
 
Lakini mleta mada, kuna jambo moja muhimu ambalo tunapaswa kulielewa tunapozungumzia instinct na reasoning.

mara nyingi michakato hii miwili haitokei kwa wakati mmoja, na katika baadhi ya mazingira inaweza kuwa mutually exclusive.


Kwa mfano instinct inaweza kukutahadharisha kwamba kuna hatari na kukuambia kimbia.......


Katika mazingira kama hayo, mara nyingi hakuna muda wa kufanya reasoning ya kina kujiuliza maswali mengi, kuchambua ushahidi, au kutathmini alternatives kwa sababu instinct huja kama mwitikio wa haraka wa kulinda usalama.


kuna mazingira mengine ambapo instinct haizuii reasoning, bali huanzisha reasoning.

Unaweza kupata gut feeling kwamba kuna kitu hakiko sawa, kisha ukaanza kuchunguza sababu, kutafuta ushahidi, na kutumia reasoning kabla ya kufanya uamuzi.....


Kwa hiyo, hatuwezi kuichukulia relationship kati ya instinct na reasoning kwa mtazamo wa single handed approach, kana kwamba kila mara lazima moja itangulie nyingine.

Uhusiano wao unategemea sana circumstances, urgency, mazingira, kiwango cha hatari, na aina ya uamuzi unaofanyika.


Kwa kifupi, instinct inaweza kuwa mwitikio wa haraka unaohitaji action, au inaweza kuwa signal inayokupa sababu ya kuanza reasoning.

Ndiyo maana ni muhimu kuangalia context kabla ya kusema kwamba instinct inapaswa kutangulia reasoning au reasoning inapaswa kutangulia instinct....

Kama Thecoder alivo jaribu kuelezea
Shukran sana mkuu umeeleza vyema sana 👏👏
 
Swali zuri sana mkuu, Natamani nielezee kwa urefu but unfortunately mimi ni mvivu kuandika na kuongea sana.

Nitajibu swali lako kwa ufupi. Kitu kinacho fanya au kitakacho fanya mpango mzima usiharibike ni logic, rules and facts (as My Name) ambavyo vitakuwa tayari vimechakatwa pande zote mbili na kupata decision, solution or conclusion as I said before.
Shukran sana brother 🙏🙏
 
Shukran sana mkuu
Vipi hivi viwili haviwezi kufanya kazi kwa pamoja?
Vinaweza na vinapaswa kufanya kazi kwa pamoja kila wakati. Havipingani, bali vinakamilishana.

Wataalamu wa akili wanaita ushirikiano huu "Akili Jumuishi" (Integrated Mind), na hufanya kazi hivi:

Intuition inaleta wazo (The Spark)

Akili yako ya ndani inakupa mwelekeo au hisia ya haraka kuhusu jambo fulani bila kutumia nguvu.

Reasoning inachambua wazo (The Filter)

Akili yako ya mantiki inaingia kati kukagua kama hisia hiyo ina ukweli, ushahidi, au mantiki.

Mfano halisi:

Unapotaka kumuajiri mtu, intuition inakuambia "Mtu huyu anaonekana mwaminifu na mchapakazi", huku reasoning ikikusaidia kukagua vyeti na kumbukumbu zake za nyuma ili kuthibitisha hisia hiyo.
 
paka sasa hivi sijajua intuition inafanyaje kazi maana ni scientificly imposible kupata feeling ya kitu ambacho kitakuja kutokea then kikatokea kweli

Mimi kwa upande wangu huwa natumia vyote, pale inapohusisha usalama wa afya na uhai wangu huwa nafata intuition zangu bila kufanya reasoning yoyote ila kwenye vitu vingine ndio naweza chagua aidha intuition au reasong
Ooh vizuri sana
Unajua unachokifanya brother
 
Lazima tujue kwamba Intuition sio hisia kuna tofauti kubwa. Kusikiliza Intuition pia sio kila mtu anaweza, kama unaweza kuisikiliza na kuitenganisha na hisia zako hii huwa haidanganyi.
Watu wengi tunapenda reasoning sababu unaweza kuwajibika kwa matokeo yake (yani nafanya hiki kwa sababu hii na natarajia matokeo haya).
Intuition yenyewe haina sababu, haiachi kukwambia jambo, ukiiipuza siku likitokea la tofauti ndo unakumbuka aah lakini kuna kitu kiliniambia nisifanye hii. Na inaua reasons zako zote zilizofanya ufanye hilo jambo.
At the end "Fuata moyo wako, usisahau akili yako"
 
Tufikirie mfano tukiwa tunasafiri katika safari tofauti.

Safari ya kwanza unayo ramani ya sehemu unapokwenda na pia unayo unatumia Dira/compass ambayo inakuongoza.

Safari ya pili unayo ramani lakini hauna Dira inayokuongoza.

Safari ya tatu hauna ramani lakini unayo Dira inayokuongoza.

Safari ya nne hauna ramani wala hauna Dira inayokuongoza.

Katika scenario zote nne kikubwa hapo ni kufika destination ya safari yako bila kujalisha unafikaje

Hapo nimefananisha Dira na uwezo wa kufikiria/reasoning/cognitive function.

Pia nimehusisha ramani na sauti ya ndani/intuition/machale/innner voice.

Kwa muktadha huo vyote vina umuhimu na kutegemeana ila sio lazima vitumike vyote kwa pamoja.

Ingawa ukiwa na Dira na ramani ukitambua jinsi ya kuvitumia vyote unafika safari yako vizuri, salama na kwa muda unaopaswa.

Pia usipokuwa na ramani unaweza ukatumia Dira na ukafika destination yako halikadhalika usipokuwa na Dira unaweza ukafika bila ramani.

Na usipokuwa na vyote Dira wala ramani unaweza na Kuna chance ya kufika destination yako hivyo hivyo ingawa ni kwa mbinde sana.

Moyo /nafsi ndio ramani wakati akili/ubongo/fikra ndio Dira.
Shukran sana mkuu 🙏🙏
 
Back
Top Bottom