Introverts kundi la phlegmatic ni wakimya mno na huwezi kujua kama wamekasirika au wamefurahi . Wanaweza kuwa wananyanyasika bila kusema . Kwa kifupi they are too dull .
Introverts kundi la melancholics siyo waongeaji lakini unaweza kuwatazama usoni ukajua kiwango chake cha furaha au hasira . Mara nyingi ni kundi la watu wanaolenga kwenye ukamilifu ( perfectionists ) , sasa changamoto ni kwamba hakuna mtu asiyekuosea ; nd'o maana wakikosea wao hawawezi kujisamehe na akikosea mwenzie hawezi kusamehe , kwa hiyo ni watu complicated ingawa ukiwaelewa huwa ni wakarimu mno na ni waaminifu na wenye vipaji vikubwa vya akili , utunzi na uvumbuzi .
Naomba kuwasilisha .
Sent using
Jamii Forums mobile app
Mi ni Introvert Sanguine, unaweza kuimagine nafananaje. Vile ninavyoshindwa mkusanyo wa watu ndivyo ninavyoweza kuwa entertainer.
Kitu watu hawajui ni kuwa Siwezi himili physical mkusanyiko kabiiiiisa, digital hivi niko poa kabisa! Hata muwe 100 at per.
Nina marafiki lukuki kimtandao, kila ikitakiwa tuonane mimi nakwepa kabisa
Sijawahi enda disco
Siendi harusi, matamasha haya ya wanawake, sijui kongamano la kidini, kitchen[arty wala sherehe , siwezi tuu!
Naweza kuwa likizo siku 28, na zote nikazimaliza nikiwa ndani!
Ninaandika mno kuliko kuongea.
Napenda watu wakiwa mbali sio wanisogelee!
Nina kajina jina huko mtandaoni, watu huamini mi ni mtu wa watuuuuuuuu vile naaandika sana na kuinteract nao kimaandishi!
Najijua ni Rafiki ninayebore usiponizoea!
Sioni shida kabisa kukaa thearte peke yangu naangalia movie hata mbili mfululizo peke yangu!
na sioni upweke kabiiiisa!
Nyumbani kwangu tunakaa mimi, mume wangu, dada na watoto.
Vile huandika sana, naaminika ni muongeaji sana.
Kitu sicho kabisa, Inasumbua mno!
Shuleni huko nilikuwa nasingiziwa vitu mpk dah!