Mimi ni extremely introvert, hivyo nitajielezea mimi ili mtu ajue jinsi ya kuishi na sisi:
1. Ninapenda sana sehemu tulivu, isiokuwa na makelele na fujo
2. Nina aibu sana mbele za watu hivyo naweza kukaa kimya muda wote hata kama najua swali au chochote mpaka niulizwe direct
3. Ninapenda sana kukaa ndani peke yangu kwa muda mrefu, naweza hata kumaliza siku tatu sijatoka nje
4. Ninapanga vitu vya baadae sana hata kama ni baada ya mwaka au miaka mingi kuja utekelezaji wake
5. Ni mtu wa mawazo sana asa kufikiria vitu tofauti vinavyo nizunguka na kutaka kuvitolea majibu
6. Nina maumivu ya ndani na uwa ni kazi kumwambia mtu kama ameniudhi au vipi na uwa simuoneshi mtu kukasirika kwangu hvyo ni ngumu mtu uyo kujua kma nimekasirika
7. Sipendi usumbufu wa vitu kuingilia ratiba yangu ambayo nimeipanga
8. Maisha yangu yanaenda kwa ratiba, kwani kila ninachofanya ni tayari nilikipanga kabla.
9. Sipendi mwanamke anayeongea sana kwani nachoka kumsikiliza mapema pia naona ananisumbua pale napo taka utulivu
10. Kuna kipindi uwa sitamani kuongea na mtu yeyote kwa simu wala ana kwa ana bali nataka nikae peke yangu niwaze tu
11. Sipendi kurudia rudia kitu kile kile kwa mtu
12. Uwa sio mpenzi wa sherehe ndo maana hata graduation yangu sikwenda
13. Ni msiri sana, kutoa siri ni mpaka pale nipende mwenyewe na uwa kitu kishapita ndo natolea maelezo
14. Sijawahi kuwa na mapenzi ya dhati kwa mwanamke, hivyo sijadumu kwa mahusiano yoyote, hadi sasa nimebreak mara tatu naona ni usumbufu kuwa kwenye mahusiano.
15. Ni mkimya sana uwa wengi wananiona mpole mno
16. Sipendi kuchat muda mrefu
17. Nimepanga kwenda kujenga polini, sehemu yenye utulivu na vegetation kwani ndo nahisi napata raha uko
18. Sipendi outings kabisa
19. Nina roho ya ukarimu ya kutoa hata kama najua najiumiza
20. Nina huruma uliopitiliza
21. Ninapenda sana kusoma
22. Ni mtu wa kupanga vitu kabla ya kutekeleza, na ninapenda vitu vyangu viwe systematically and not randomly
23. Uwa niko defensive sana kwenye hisia zangu, hvyo kma naona kuna kitu hichi kitanipa au kinaelekea kunipa maumivu uwa napotezea na kuepuka hicho kitu
24. Nikashaamua jambo fulani uwa ni ngumu kubadilisha au kubadilika maana na kuwa nimeshafikiria sana peke yngu na kuamini kuwa niko sahihi.
25. Overthinking ndo ugonjwa wangu kwani kuna muda uwa hadi nakonda kwa kuimagine tu mpaka wengine wanahisi nastress
26. Uwa ni mtu wa kukaa nawaza muda wote, naweza nkawa na watu hapa kumbe mimi mawazo yangu yapo mbali sana.
27. Sina rafiki hapa maeneo ya nyumbani, ni mtu wa ndani au ni moja kwa moja kazini na kurudi ndani
28. Ninaumia sana kama kitu nilichopanga kikafeli au kushindikana kwani ninakuwa nilitumia nguvu nyingi na muda mwingi kukitengenezea plan.
Vipo vingi sana hadi naona sitomaliza, itoshe tu kusema hali hii nilizaliwa nayo na wala sio malezi.
Sent from my iPhone using JamiiForums