Bishop Hiluka
R I P
- Aug 12, 2011
- 7,150
- 14,724
Nijuavyo mimi (kwa mujibu wa Biblia), Mungu humuonesha mtu amtakaye jambo fulani kwa muda fulani na akiwa na kusudi fulani (ingawa hata shetani huwaonesha watu wake wamwabuduo), na mwingine huoneshwa jambo lingine kwa kusudi fulani. Hata manabii hawakufunulia mambo yote bali kila mmoja alipewa vipande vipande na vipande vilivyobaki akapewa mwingine ili kukamilisha maandiko.Kwahiyo mkuu na jambo hili linaweza kuwa ni kama haya matukio ya ndoto unayoyasema?
Ni kwanini Morgan Roberson hakuwa na maono mengine zaidi ya haya?
Kwa mfano Yeremia alikuwa akifunulia sana kuhusu majanga/ maafa kiasi kwamba walimpachika jina la nabii wa majanga, lakini Isaya akapewa zaidi mafuno kuhusu Masia, Daniel ndiye aliyepewa mafunuo kuhusu kitabu (Dan. 12:4) alichoambiwa akifunge na kukitia muhuri, lakini kikaja kuonekana kwenye maono na Yohana (kwenye Ufunuo)...