Insane coincidence: Futility and Titanic

Mkuu Eiyer kuna habari titanic ilizamishwa kwa sababu ya matajiri watatu waliokwemo ndani ya titanic,ambao ni Benjamin Guggeenhein, Isador Strauss pamoja na John Jacob Astor aliyeaminiwa kuwa tajiri namba moja duniani kwa wakati huo.
Dhana hii naifahamu vizuri sana,lakini kuna maswali kadhaa ambayo yanakosa majibu.....

1;Hii meli ilizamishwa namna gani kwa style hii?
2;Walioizamisha waliizamisha kwa kufuata matukio ya meli ya kwenye hadithi ili iweje?
 
Unaweza kufafanua zaidi mkuu?
Mkuu Eiyer, nitajaribu kuelezea kwa kifupi tu ninavyoelewa, japo mimi sijazama sana kwenye mambo haya. Mara nyingi sana imetokea pale unapowaza kufanya jambo fulani, au unapolifanya, kisha ukaja kushangaa jambo hilo limefanyika sehemu nyingine katika namna ileile uliyoiwaza (au kuifanya) wewe, au ukafikira kitu halafu ukashangaa ulichokifikiria kinatokea baadaye katika namna ileile, na ukabaki kujiambia, “nilijua tu lazima kitokee!’

Hali hii imekuwa ikinitokea sana, mara nyingi naweza kuandika kukielezea kitu (mimi ni mchambuzi) kwa namna ambayo nadhani ni imagination, halafu miaka michache baadaye ikatokea kwa namna ileile nilivyoandika, na mara nyingi watu wanaofuatilia articles zangu huwa wananiuliza kama nilikuwa najua kuhusiana na mambo hayo. Mwanzoni nilidhani ni coincidence tu, lakini nikaanza kufuatilia kujua, inakuwaje niwaze vitu halafu vitokee, zaidi ya mara nne au tano?

Nilichogundua ni kuwa hii inasababishwa na kuwa wewe unayeonekana (au mimi) ni kivuli tu cha mtu halisi aliye ndani yako (mtu wa rohoni) ambaye ana mawasiliano na ulimwengu wa roho na huwa anatenda kazi katika ulimwengu usioonekana (Ulimwengu wa roho), lakini anasababisha matokeo (majibu) ya ulimwengu wa roho yatokee katika ulimwengu wa mwili. Yapo maandiko mengi kwenye Biblia yanayo-prove jambo hili, ila kwa mazingira niliyopo ni ngumu kuonesha.

Wewe sio huo mwili wako, wewe sio hilo jina lako, wewe sio huo mkono wako, wala wewe sio hizo sifa unazopewa, ndiyo maana ukishaaga dunia hawakuiti tena wewe, bali wanasema mwili wa wa marehemu fulani. Ina maana mmiliki halisi wa mwili huo na vyote ulivyonavyo ni yule mtu wa ndani anayetenda kazi kupitia wewe unayeonekana kwa macho ya nyama (huo mwili ulionao).

Ulimwengu wa Roho ni ulimwengu usioonekana kwa jinsi ya mwili, anayeweza kuujua ulimwengu huo ni yule mtu wa "Rohoni", ambaye ni wachache sana wanaweza kujua anafanyaje kazi, na ndiye anaweza kupigana vita katika ulimwengu huo.

Wapo baadhi ya watu wanajua kile kinachoendelea kwenye dunia zote mbili (roho na mwili) na ndiyo tumekuwa tukisikia kila mara kwamba wanai-drive dunia iende vile wanavyotaka, na wengine (kama mimi) tunaona mambo fulani yanatokea tu kama tulivyowaza na kudhani it’s just a coincident. Kumbuka kisa cha Eliya (kwenye Biblia) kuzuia mvua na baada ya miaka mitatu kuomba tena mvua inyeshe.

Ulimwengu wa roho una tawala kuu mbili (Utawala wa Nuru na utawala wa Giza), ili uweze kuweka mabadiliko mahali ambapo "kuna utawala wa ulimwengu wa roho" lazima uanze kuharibu/ kupambana na utawala huo katika ulimwengu wa roho, na ndipo utafanikiwa katika ulimwengu wa mwili.

Ndiyo maana kila uharibifu (au ubunifu) unapotokea mahali fulani, basi chanzo chake huwa ni "ULIMWENGU WA ROHO"

Nadhani nimejaribu kidogo kujibu swali lako...
 
Asante sana mkuu kwa kutujuza zaidi kuhusu meli ya Titanic

Kwa hiyo walimwua Morgan au?

kuna wakati unaweza kuwaza kitu halafu baada ya muda hata miaka 1 au 2 kinakuja kutokea unajiuliza ilikuwa ni ndoto
Mkuu mm niliota mama yangu kafariki baada ya miaka mitatu tukio likarudia vile vile paka nikajua naota tena kumbe nipo kwenye uhalisia ni kama nilimuadithia kifo chake kitavyo kuwa kwasababu niliota nikamuambia mama nimeota umekufa nikamudithia ndoto yote na siku aliyokufa kweli akuna ata tukio moja lililoenda tofauti na nilicho kiota
 
Mkuu eiyer Mimi niliacha kabisa kupost jamii intelligence, hawa jamaa wanachokifanya ni kero kubwa sana. Mtu unaweka thread inabidi usubiri siku 3 ili ije kuonekana. sijui hua wanaedit nini, yani bado sijaelewa, maana hata wakiachia unakuta thread iko vile vile kama ulivyoipost.

Uongozi wa JF watuletee moderator specific kwajili ya jamii intelligence, awe mtu mwenye akili timamu ambaye anaweza kusoma thread na kufanya editing (kama kutakuwa na umuhimu) na kuachia thread iwe public in less that half an hour.
Mkuu nakuomba tu urudi kuandika nilikuwa napenda story zako unapangilia vizuri aichoshi kusoma
 
Mambo mengi yanayotokea huku duniani yanakuwa yameshakuwa planned miaka kadhaa iliyopita.
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Asante sana mkuu kwa kutujuza zaidi kuhusu meli ya Titanic

Kwa hiyo walimwua Morgan au?

kuna wakati unaweza kuwaza kitu halafu baada ya muda hata miaka 1 au 2 kinakuja kutokea unajiuliza ilikuwa ni ndoto
Heshima Mkuu, Blaki.

Nadhani binadamu mwenye sifa za kinabii ndiye mwenye uwezo wa kutabiri jambo then baada ya muda utabiri wake hujidhihirisha.

Hivi tuite ndoto au maono?.Au yote kwa pamoja?.
 
Dhana hii naifahamu vizuri sana,lakini kuna maswali kadhaa ambayo yanakosa majibu.....

1;Hii meli ilizamishwa namna gani kwa style hii?
2;Walioizamisha waliizamisha kwa kufuata matukio ya meli ya kwenye hadithi ili iweje?
Edward Smith alikuwa ndiye nahodha wa titanic

Edward Smith amekuwa nahodha kwa miaka 26 akiwa na uzoefu wa kutosha na ruti za bahari ya Atlantiki. Amefanya kazi kwa miaka mingi akiwa ndani ya kampuni ya J.P. Morgan. sasa haiingii akilini kwa nahodha kama Edward Smith ashindwe kuelewa baharini kuna iceberg.
 
Mbona kunasehemu nilisoma kwamba huyo jamaaa aliyesimamia hiyo meli Mpaka ikakamilika alipo hojiwa uimara wake ulitoa kufuru akasema kwa kwa jinsi ilivyo imara hata mungu hawezi kuizamisha matokeo yake ndo hayo alileta kufuru huyo majinga
Hata ile ya kwenye hadithi ilikuwa na sifa hizo hizo.....
 
Edward Smith alikuwa ndiye nahodha wa titanic

Edward Smith amekuwa nahodha kwa miaka 26 akiwa na uzoefu wa kutosha na ruti za bahari ya Atlantiki. Amefanya kazi kwa miaka mingi akiwa ndani ya kampuni ya J.P. Morgan. sasa haiingii akilini kwa nahodha kama Edward Smith ashindwe kuelewa baharini kuna iceberg.
Nafahamu kuhusu Cpt Smith....

Ndiyo tujiulize sasa iliwezekanaje jambo hili likatokea?
 
Mkuu Eiyer, nitajaribu kuelezea kwa kifupi tu ninavyoelewa, japo mimi sijazama sana kwenye mambo haya. Mara nyingi sana imetokea pale unapowaza kufanya jambo fulani, au unapolifanya, kisha ukaja kushangaa jambo hilo limefanyika sehemu nyingine katika namna ileile uliyoiwaza (au kuifanya) wewe, au ukafikira kitu halafu ukashangaa ulichokifikiria kinatokea baadaye katika namna ileile, na ukabaki kujiambia, “nilijua tu lazima kitokee!’
Nimesoma maelezo yako mkuu....

Hiki unachokisema hapa huwa kinatokea kwa namna ile ile au kunakuwa na tofauti kadhaa?
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Mkuu mm niliota mama yangu kafariki baada ya miaka mitatu tukio likarudia vile vile paka nikajua naota tena kumbe nipo kwenye uhalisia ni kama nilimuadithia kifo chake kitavyo kuwa kwasababu niliota nikamuambia mama nimeota umekufa nikamudithia ndoto yote na siku aliyokufa kweli akuna ata tukio moja lililoenda tofauti na nilicho kiota
Mwaka huu niliota ndoto nipo katikati ya Kundi la Polisi wenye vyeo vya juu (CP, DCP SACP, ACP) katika Jeshi la Polisi wakiniskiliza tukiwa tunapiga stori (mimi sio Polisi) tukiwa maeneo ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, nilipoamka asubuhi nikajiuliza sana juu ya ndoto hii na sikupata majibu. Nikaamua kupuuzia, lakini wiki iliyofuata nikawa katika mazingira yaleyale Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (katika ulimwengu wa mwili na sio ndoto tena) nikiwa nimezungukwa na Polisi walewale niliowaona ndotoni tukipiga stori, hii ilikuwa wakati tukisubiri kuuaga mwili wa mpwa wangu Peter Kubezya (yule OCCID aliyeuawa Kibiti ambaye mwili wake uliagwa Muhimbili kabla hajasafirishwa kwenda kuzikwa Ushirombo). Wakati nikiongea na askari hao ikanijia picha ileile niliyoiona kwenye ndoto...
 
Tudokezee kidogo kuhusu titanic 2
Hii ni meli inayotengenezwa baada ya ile ya kwanza kuzama....

Inatengenezwa ili ije ifanye safari kitoka kule kule Southampton kuelekea New York....

Meli hii inatengenezwa Australia na kampuni ya CSC Jinling,Nanjing....

Meli hii itagharimu dola mil 500...

Meli hii ni mali ya kampuni ya Blue Star line....

Itakuwa na urefu wa futi 883 na kampuni itakayomiliki meli hii iko chini ya billionea Clive Palmer ambaye ni mwenyekiti wa kampuni.......
 
Hilo ni tukio la uhalifu wa kupangwa(Consipiracy). Matukio kama haya fatilia ni watu gani mashuhuri au maarufu waliokuwepo kwenye hiyo meli. Kuna maelezo kulikuwa na matajiri wakubwa duniani. Unaweza ukafatilia zaidi ukawasoma hao matajiri kuhusu wao unaweza ukang'amua kitu. Hiyo ilipangwa, ilipangwa vipi sijui. Tunaweza kuhadithiwa ni barafu limegonga kumbe ni shambulizi limefanyika makusudi kisha wakasema ni barafu limegonga. Kila kitu kinawezekana.

Kuhusu kufanana na kitabu, inawezekana wao ndio wamefanya makusudi ili ifanane, kuanzia vipimo na uwezo wa meli mpaka wapi tukio la kuzama litokee n.k Eiyer
 
Nimesoma maelezo yako mkuu....

Hiki unachokisema hapa huwa kinatokea kwa namna ile ile au kunakuwa na tofauti kadhaa?
Kwangu mimi (sijui kwa wengine) huwa kinatokea kwa namna ileile, ni zaidi ya mara tatu au nne. Kwa mfano kuna wakati nimewahi kuota ndoto niko katika mji wa kigeni, nikawa napita kwenye mitaa kadhaa ambapo kulikuwa na mabango na baadaye nikaingia kwenye jengo fulani la ghorofa tatu, linalopakana na jengo lingine linalolindwa na wanajeshi, likiwa na bendera.

Miaka minne baadaye nikasafiri kwenda Bujumbura, nikajikuta nikipita mitaa ileile na kuona mabango yaleyale niliyoyaona ndotoni, cha ajabu ni kwamba hata jengo nililoingia lilikuwa ni hoteli inayoitwa 'New Agena Hotel' ambayo ipo eneo linaloitwa Sororezo, ipo jirani na jumba analoishi rais mstaafu wa Burundi, Pierre Buyoya, ikiwa inalindwa na askari walewale niliowaona kwenye ndoto...
 
Mwaka huu niliota ndoto nipo katikati ya Kundi la Polisi wenye vyeo vya juu (CP, DCP SACP, ACP) katika Jeshi la Polisi wakiniskiliza tukiwa tunapiga stori (mimi sio Polisi) tukiwa maeneo ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, nilipoamka asubuhi nikajiuliza sana juu ya ndoto hii na sikupata majibu. Nikaamua kupuuzia, lakini wiki iliyofuata nikawa katika mazingira yaleyale Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (katika ulimwengu wa mwili na sio ndoto tena) nikiwa nimezungukwa na Polisi walewale niliowaona ndotoni tukipiga stori, hii ilikuwa wakati tukisubiri kuuaga mwili wa mpwa wangu Peter Kubezya (yule OCCID aliyeuawa Kibiti ambaye mwili wake uliagwa Muhimbili kabla hajasafirishwa kwenda kuzikwa Ushirombo). Wakati nikiongea na askari hao ikanijia picha ileile niliyoiona kwenye ndoto...
Kwahiyo mkuu na jambo hili linaweza kuwa ni kama haya matukio ya ndoto unayoyasema?

Ni kwanini Morgan Roberson hakuwa na maono mengine zaidi ya haya?
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Hilo ni tukio la uhalifu wa kupangwa(Consipiracy). Matukio kama haya fatilia ni watu gani mashuhuri au maarufu waliokuwepo kwenye hiyo meli. Kuna maelezo kulikuwa na matajiri wakubwa duniani. Unaweza ukafatilia zaidi ukawasoma hao matajiri kuhusu wao unaweza ukang'amua kitu. Hiyo ilipangwa, ilipangwa vipi sijui. Tunaweza kuhadithiwa ni barafu limegonga kumbe ni shambulizi limefanyika makusudi kisha wakasema ni barafu limegonga. Kila kitu kinawezekana.

Kuhusu kufanana na kitabu, inawezekana wao ndio wamefanya makusudi ili ifanane, kuanzia vipimo na uwezo wa meli mpaka wapi tukio la kuzama litokee n.k Eiyer
Inawezekana kabisa tukio hili lilipangwa...

Sasa mkuu wamefananisha na kitabu ili iweje?
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Kwangu mimi (sijui kwa wengine) huwa kinatokea kwa namna ileile, ni zaidi ya mara tatu au nne. Kwa mfano kuna wakati nimewahi kuota ndoto niko katika mji wa kigeni, nikawa napita kwenye mitaa kadhaa ambapo kulikuwa na mabango na baadaye nikaingia kwenye jengo fulani la ghorofa tatu, linalopakana na jengo lingine linalolindwa na wanajeshi, likiwa na bendera.

Miaka minne baadaye nikasafiri kwenda Bujumbura, nikajikuta nikipita mitaa ileile na kuona mabango yaleyale niliyoyaona ndotoni, cha ajabu ni kwamba hata jengo nililoingia lilikuwa ni hoteli inayoitwa 'New Agena Hotel' ambayo ipo eneo linaloitwa Sororezo, ipo jirani na jumba analoishi rais mstaafu wa Burundi, Pierre Buyoya, ikiwa inalindwa na askari walewale niliowaona kwenye ndoto...
Nimekusoma mkuu...

Ninavyojua masuala haya anayekuwa na "maono" haya hawi na maono mara moja tu bali hata zaidi,nashangaa huyu ni tukio hili hili tu.....
 
Back
Top Bottom