Insane coincidence: Futility and Titanic

Insane coincidence: Futility and Titanic

Nilitegemea kusikia kuhusu huu mwisho wake. Sasa naamini kabisa kuwa jambo hilo lilikuwa na uhusiano na ulimwengu wa roho, maana wengi wao huwa na sifa kama za huyo mtu: wanaonekana kuwa ni watu wa kawaida sana, wanaonekana kama wana matatizo ya akili (kwa kuwa wanaishi katika dunia inayoitwa 'beyond imagination'), na hata vifo vyao huwa ni vya kutatanisha, au huambatana na mauzauza fulani...

Nikipata nafasi nitaeleza zaidi kuhusu dunia ya 'beyond imagination' (kwani kwa sasa kuna kazi muhimu naifanya kwanza), kwani wengi waliofanikiwa sana (kama marais, wafanyabiashara wakubwa, watu mashuhuri) walianzia kwenye hii dunia kabla ya kufika hapo walipo...
Mkuu ukileta hizo nondo naomba unitag tafadhali...
 
Daah this story iko impressive sana nimebaki kinywa wazi baada ya kuisom shukrani zako nying mleta mada. Inawezekana ikawa planned kama mchangiaji mmoja alivyosema,
 
Tunasubiri mkuu utupe elimu hii
 
asante kwa kunitag mkuu Eiyer nimejifunza na kutafakari sana namna mambo yanavyoenda hapa duniani hakika kuna master plan anafanya yake kwa namna isiodhanika mapema ila kwakua MUNGU yupo anatufunulia kwa njia nyingi na hata ww ni njia moja wapo.
 
Okay, nimerejea kama nilivyoahidi. Pia nimezingatia angalizo lako.
Maisha ya binadamu huwa yamezungukwa na layers (hatua) nne katika kuhakikisha anapiga hatua kuelekea mafanikio yake, layers ambazo huwa zinamsukuma kufanya mambo (wakati mwingine bila yeye mwenyewe kujua). Layers hizi ndizo huchagiza msukumo wake kuelekea maendeleo au kushindwa kwake.

Layer ya kwanza huitwa “EASY TO DO”; hii ni layer ambayo kila binadamu huiishi, hasa pale anapoona jambo akajisemea “mbona hii hata mimi naweza kufanya!”. Kwa mfano pale anapomwona mkwezi akiangua nazi hudhani kuwa hata yeye anaweza kuwa mkwezi, na kusahahu kuwa kila kazi ina utaalamu wake.

Inapotokea mtu akasikia jambo fulani au akaona jambo fulani limefanyika; mfano hili andiko lako kuhusu Titanic ambalo naamini imekuchukua siku kadhaa kuliandika, mtu mwingine anaweza kudhani ilikuwa ni rahisi tu kwa kuwa hukutunga bali umesoma sehemu na kufanya uchambuzi ama kutafsiri maandiko ambayo tayari yapo, lakini akitaka na yeye afanye kama ulivyofanya wewe ndipo anapogundua kuwa ‘kuna ugumu fulani katika kazi hiyo’, na kwamba hiyo ni kazi inayohitaji utaalamu fulani kuifanya. Hapa ndipo anapoingia kwenye layer ya pili inayoitwa “IT’S DIFFICULT”.

Hii ni layer ambayo kama si mvumilivu, safari yako inaweza kuishia hapa, lakini kwa wanaokomaa hujiambia, “ni ngumu lakini nitajaribu”. Watapambana kwa kila hali na hatimaye kufanikiwa, na wengine hujikuta wakiridhika na kuishia hapo, hasa baada ya mafanikio ya hatua hii. Wanaojaribu kusonga mbele zaidi hukutana na layer ya tatu inayoitwa “IT’S IMPOSSIBLE”.

Hii ni layer ambayo wengi mno tumekwama hapa, kwani binadamu hujikuta kila anachogusa anaona hakiwezekani. Ni katika hatua hii ambapo mambo mengi huwa yanayaonekana hayawezekani kabisa, na anayejaribu kuyafanya anaonekana anasumbuka bure, kwani “haiwezekani”. Ni katika hatua hii mtu anayethubutu na kufanya jambo ambalo wengine walidhani 'haliwezekani' na akafanikia huonekana ni 'genius'.

Ni katika layer hii ambapo Kyler na timu yake kwenye Manhattan Project walifanikiwa kutengeneza atomic bomb XD, mwaka mmoja tu baada ya profesa mmoja wa sayansi mashuhuri wa Urusi (nimelisahau jina lake) kusema “It’s impossible for a man to capture an atom,” na watu wakaamini hivyo kwa kuwa statement hiyo ilitolewa na profesa aliyebobea kwenye physics. Lakini Kyler na timu yake wakam-prove wrong kwa kutengeneza atomic bomb.

Layer ya mwisho ni “BEYOND IMAGINATION”, ambapo watu wanaoishi kwenye dunia hii mara nyingi huonekana aidha wamechanganyikiwa au wana matatizo ya akili, kwa kuwa hufikiria vitu ambavyo vipo kwenye dunia ya kufikirika. Dunia ambayo wengi hawaioni wala kudhani kwamba ina-exist.

Kwa mfano, mnamo mwaka 1964 wakati Nelson Mandela anahukumiwa kifungo cha maisha jela, kama angetokea mtu akasema kuwa Mandela atakuja kuwa Rais wa Afrika Kusini, angeonekana amechanganyikiwa na anastahili kuwa kwenye wodi ya vichaa. THIS IS BEYOND IMAGINATION.

Lakini Mandela mwenyewe aliishi katika layer hii ndiyo maana alikataa offer ya kutolewa gerezani na kupewa pesa nyingi ili akaishi nje ya Afrika Kusini na kuachana na harakati za uhuru, na wapo waliomuona ama ana matatizo ya akili au amechanganyikiwa.

Mfano mwingine ni; kama miaka kumi na tano tu iliyopita angetokea mtu akasema kuwa dunia (kwa maana ya Marekani) ingekuja kuwa chini ya utawala wa mtu mwenye asili ya Afrika, bila shaka angeonekana amechanganyikiwa, na hata Barack Obama mwenyewe alipoanza harakati za kutaka kuingia ikulu ya Marekani wapo walioona anajisumbua bure, maana wakati huo alikuwa akishindana na wasaniasa waliokuwa wanakubalika sana kama Mama Hiraly Clinton. Wakasahu kuwa Obama mwenyewe aliishi kwenye layer hii akiamini kuwa ndoto zake lazima ziwe kweli…

Hata Jakaya Kikwete alikuwa akiwaambia rafiki zake mara kwa mara kuwa lazima siku moja awe kiongozi wa nchi na kuishi pale magogoni. Alipoianza safari yake mwaka 1995 wapo walioona anamsindikiza Lowassa, lakini baadaye ndoto yake ikatimia. ingawa sidhani kama kuna waliomuona kuwa amechanganyikiwa.

Ndiyo maana huwa nawaogopa sana watu wanaoonekana kama wana matatizo ya akili lakini ukiwatazama kwa makini utagundua si matatizo ya akili in such, bali wanaishi kwenye dunia hii. Kwa mfano atokee msanii mmoja wa Bongo Movies, aoneshe kuwa ana mpango wa kutengeneza movie itakayokuja kutamba kimataifa na kuchukua Tuzo ya Oscar, kila mtu atamuona amechanganyikiwa (au ana matatizo ya akili), lakini kama ataamua kuiishi ndoto yake kwa kufanya kazi kwa bidii, inaweza kutokea na kila mtu akashangaa…
Ok what you are seeking is seeking you
 
asante kwa kunitag mkuu Eiyer nimejifunza na kutafakari sana namna mambo yanavyoenda hapa duniani hakika kuna master plan anafanya yake kwa namna isiodhanika mapema ila kwakua MUNGU yupo anatufunulia kwa njia nyingi na hata ww ni njia moja wapo.
Mkuu tunaishi kwenye maisha fake sana kwakweli....

Siku tukijua hata theluthi tu tutashangaa sana....
 
Daah this story iko impressive sana nimebaki kinywa wazi baada ya kuisom shukrani zako nying mleta mada. Inawezekana ikawa planned kama mchangiaji mmoja alivyosema,
Haina shida mkuu,tutaendelea kuleteana mambo magumu na yasiyosemwa kwa kadiri tutakavyoweza,tuombe uzima tu mkuu....
 
Back
Top Bottom