Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,408
- 33,285
KIWANDA CHA POMBE CHATOA MSAADA PEMBA KWA AJILI YA RAMADHANI..
PICHANI: Mkurugenzi wa Kampuni ya (KUTENGENEZA POMBE YA KONYAGI) Tanzania Distilleries Limited (TDL) David Mgwassa (kushoto),
akiwakabidhi msaada wa vyakula na mafuta ya kupikia vyote vikiwa na thamani ya sh.milioni 9, wabunge wa Zanzibar, Ahmed Ngwali (kulia), wa
Jimbo la Ziwani na Khalifa Suleiman wa Jimbo la Kagando kwa ajili ya kuwasaidia wajane na yatima waliofiwa na wategemezi wao katika ajali ya meli
ya Mv Spice na Skagit zilizotekea visiwani humo. Makabidhiano hayo yalifanyika Dar es Salaam juzi.
Mgwasa, alisema,"Kampuni yetu inatoa msaada hasa kwa ajili ya Mwezi huu Mtukufu wa Ramadhani ili watoto hawa yatima wakapate futari.
Alisema msaada uliotolewa umelenga kuwasaidia yatima walioko Pemba kwanza. Mbunge wa Gando, Khalifa alisema "...Na pia wananchi wasitizame
nani ametoa msaada ila ini amesaidia ili tu kuwasaidia hawa wenye uhitaji," alisema Khalifa. (via HabariLeo)
chanzo. Habarileo
Kama ningelikuwa ndio mimi mpokezi wa huo Msaada ;Wallah nisingelipokea kamwe Msaada wa haramu huo.
SURAT AL MAIDA Sura 5:90-91-92
90. Enyi mlio amini! Bila ya shaka ulevi, na kamari, na kuabudu masanamu, na kupiga ramli, ni uchafu
katika kazi ya Shet'ani. Basi jiepusheni navyo, ili mpate kufanikiwa.
91. Hakika Shet'ani anataka kutia kati yenu uadui na chuki kwa ulevi na kamari, na akuzuieni kumkumbuka Mwenyezi Mungu na kusali. Basi je, mmeacha
92. Na mt'iini Mwenyezi Mungu, na mt'iini Mtume, na tahadharini. Na ikiwa mtageuka basi jueni ya kuwa juu ya Mtume wetu ni kufikisha ujumbe tu ulio wazi.
Pesa inayotokana na Pombe na Kamari ni Pesa ya Haramu haifai kwa Muislam kuitumia kwa kulia futari ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.