Innaa lillahi wainnaa ilayhi raaji uun waislamu tumefikia hatua hii ?!!!

Status
Not open for further replies.
huo ni unafiki mkubwa. Nchi hii chanzo kikubwa cha mapato ni pombe na sigara. Hiyo hela wafanyakazi hulipwa mishahara, kujenga shule, hospitali, barabara, bandarikununua vyombo vya kusafiria, nk. Kati ya hizo umewahi kugoma kutumia kwa vile vimetokana na pombe/sigara. Kt nyumba za ibada harambee/michango/sadaka hutolewa bila kuuliza pesa umepataje, fisadi,mwizi,kahaba, shoga, muuza madawa ya kulevya wote hotoa na zinapokelewa. Ni vema kutafakari kwa kina sio kwa ajili ya ramadhani tu.
 
Huu ni msiba. Ipo siku tutawapa hawa makafiri mimbari watoe hut'ba ili tupate pesa.

Juzi tumemuita Lowasa na kumvisha kilemba, leo tunapokea misaada.

Huu ni msiba.

Uacheni Umma wa Allah ufaidi. Sio kila mtu mwenye uwezo wa kula kashata na kahawa. Wengine hawana kabisa hata uwezo wa kununua kahawa ya sh 100...
cc: Mwana Mtoka Pabaya, Masanilo
 
Last edited by a moderator:
mlaumu baba ako na mama ako kukuzalia ktk janga la kidunia,mlaumu na shekh wako kwa kukukazia uwongo,eti unajiita mzee,kwani unadhani mimi kijana?kagongane huko ulale.

wewe kweli unapita mipaka! kama kweli wewe si kijana!! basi ni hasara ilioje kuwa na mzee kama wewe ktk jamii ya watanzania. mungu asaidie vizazi vijavyo visiwe na tabia kama hizi, loooh! uzee busara baba! sio matusi na kashfa!! au nyie ndo wale wazee macheki bob! kuupenda ujana usio na manufaa?!
 
Nilikua sitaki kuchangia
lakini maneno yako yamenigusa. Mkuu hebu punguza chuki dhidi ya uislam,
jaribu kuwa mstaarabu kama Mkuu Mkerekweta. Unajua mnapokua katika
jamii ambayo kuna mchanganyiko wa itikadi tofauti ni lazima uvumilivu
uwepo la sivyo hamuwezi kuishi kwa amani. Lazima tuelewe kwamba wote
sisi binadamu tumeanzia kwa adamu{kama jina lilivyo BIN ADAMU} Yaani
Kama unaitwa Salehe Omari basi wewe ni Salehe Bin Omari. Bilashaka Great
Thinkers mmenipata. Tofauti zetu za kiimani zimesababishwa na
wasambazaji wa maandiko ya Mungu. Nafasi ya kujadiliana na kujenga hoja
juu ya uamuzi wa mtu kuwa muislam au mkristo itumiwe katika misingi ile
ile ya amani na utulivu tena bila kutukanana maana sote ni Ndugu(kama
nilivyofafanua hapo juu). Mtoa hoja analo la kusema kwa mujibu wa
mafundisho ya dini yake aliyoyapata. Kama kwa upande mwingine amekukera
basi toa comments zako katika namna ambayo yoyote atakayesoma
ulichoandika,bila kujali dini yake hawezi kuchefuliwa na
ulichokiandika.

wala siwachukii ndugu zetu watukufu waislaam,mbona nakaa nao sana tu kwenye kula kitimoto na bia?sema tu mtoa maada inabidi apewe maneno makali ili asirudie tena kutuandikia porojo,si umeona hata wewe ulikuwa hutaki kuchangia?tena ilitakiwa huyu kijana atandikwe viboko hadharani ili akome kuwaona wenzake matahira kwa kupokea msaada huo
 
msumari upi unaeweza kunipiga ewe mkamua kinyec maiti, tafadhali niache nipate wasaa wa kui-train akili yangu kufikiri mambo ya maana zaidi/

ha ha ha ha! angalia baba, ukikaa vibaya ntakukamua hata wewe! manake hilo jina linaweza kukusaliti! nikuache kwani mimi na wewe tumefunga ndoa lini?! mbona unataka kuniletea shida na mama watoto wangu tena??? alllla!
 
ha ha ha ha! angalia baba,
ukikaa vibaya ntakukamua hata wewe! manake hilo jina linaweza
kukusaliti! nikuache kwani mimi na wewe tumefunga ndoa lini?! mbona
unataka kuniletea shida na mama watoto wangu tena??? alllla!

anakuhatarishia ndoa yako huyu aisee,balaa gani tena hili.?
 
wewe na huyo mwenzako aliyejipa jina la kiislamu Abdulhalim nidhamu zenu ni ndogo sana, na nilikuwa najiuliza ni nini sababu!? lkn umeshanipa jibu!! ULAJI WA KITIMOTO!, hiyo ndio sababu ya kutokwa povu la kashfa dhidi ya waungwana! mkuu kiti moto kinarusha akili! nakuapia vile!! ohooo! shauri yako! wee endelea kula tu. sasa hivi utaanza kuimba brbrani!
Huo usilamu ulinipa wewe, tafadhali don't draw me into your stupidity/
 
ha ha ha ha! angalia baba, ukikaa vibaya ntakukamua hata wewe! manake hilo jina linaweza kukusaliti! nikuache kwani mimi na wewe tumefunga ndoa lini?! mbona unataka kuniletea shida na mama watoto wangu tena??? alllla!
Ndo maana nimeomba uniache, maana sidhani kama mtu mwene fikra za kukamua kinyesi maiti tunaeza tukajadili jambo lolote la maana. Tafadhali endelea kujadiliana na watu mnaolingana mafikara./
 
hayo uliyoyaandika hapo juu ni dhahiri umekurupuka kama alivyokurupuka muislam mwenzio,nyie ndugu zetu jaribuni kutumia akili na sio kukubali kudanganywa tu na mashekh wenu,eti ni dini pekee inayomfundisha binadamu jinsi ya kuoga,kula,kulala nk.!UMESHIRIKISHA UBONGO KWELI?

Area 254, acha ubishi nina uhakika kuwa unafahamu fika kuwa kabla ya uislam watu walikuwa hawalali, hawaogi, hawali, hawalei watoto, hawaishi na jirani,hawahifadhi pesa, hawalimi, n.k.
 



KIWANDA CHA POMBE CHATOA MSAADA PEMBA KWA AJILI YA RAMADHANI..

PICHANI: Mkurugenzi wa Kampuni ya (KUTENGENEZA POMBE YA KONYAGI) Tanzania Distilleries Limited (TDL) David Mgwassa (kushoto),

akiwakabidhi msaada wa vyakula na mafuta ya kupikia vyote vikiwa na thamani ya sh.milioni 9, wabunge wa Zanzibar, Ahmed Ngwali (kulia), wa

Jimbo la Ziwani na Khalifa Suleiman wa Jimbo la Kagando kwa ajili ya kuwasaidia wajane na yatima waliofiwa na wategemezi wao katika ajali ya meli

ya Mv Spice na Skagit zilizotekea visiwani humo. Makabidhiano hayo yalifanyika Dar es Salaam juzi.

Mgwasa, alisema,”Kampuni yetu inatoa msaada hasa kwa ajili ya Mwezi huu Mtukufu wa Ramadhani ili watoto hawa yatima wakapate futari.

Alisema msaada uliotolewa umelenga kuwasaidia yatima walioko Pemba kwanza. Mbunge wa Gando, Khalifa alisema “...Na pia wananchi wasitizame

nani ametoa msaada ila ini amesaidia ili tu kuwasaidia hawa wenye uhitaji,” alisema Khalifa. (via HabariLeo)

chanzo. Habarileo


Kama ningelikuwa ndio mimi mpokezi wa huo Msaada ;Wallah nisingelipokea kamwe Msaada wa haramu huo.

SURAT AL MAIDA Sura 5:90-91-92

90. Enyi mlio amini! Bila ya shaka ulevi, na kamari, na kuabudu masanamu, na kupiga ramli, ni uchafu
katika kazi ya Shet'ani. Basi jiepusheni navyo, ili mpate kufanikiwa.



91. Hakika Shet'ani anataka kutia kati yenu uadui na chuki kwa ulevi na kamari, na akuzuieni kumkumbuka Mwenyezi Mungu na kusali. Basi je, mmeacha

92. Na mt'iini Mwenyezi Mungu, na mt'iini Mtume, na tahadharini. Na ikiwa mtageuka basi jueni ya kuwa juu ya Mtume wetu ni kufikisha ujumbe tu ulio wazi.

Pesa inayotokana na Pombe na Kamari ni Pesa ya Haramu haifai kwa Muislam kuitumia kwa kulia futari ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Asalaama aleikhum...Sasa tunapotaka mahakama ya Kadhi ianzishwe na serikali lazima ighalimie, Sasa hizo hela zitatenganishwaje na zile za Vinywaji vya kilevi au kodi ya vitimoto????!!!! Hapo ndipo tunapoonekana ndumakuwili kaka
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom