Inawezekana Tanzania haijawa Tayari kwa mashindano makubwa ya kimataifa yanayoihusu timu ya Taifa

Mtemi01

Member
Joined
Dec 23, 2023
Posts
28
Reaction score
56
Nimejaribu kufuatilia mwenendo wa mashindano haya ya CHAN hasa ushiriki wa mashabiki uwanjani, ukweli ni kuwa Tanzania bado sana. Sio tu mashabiki, hata viongozi wenyewe ni kama vile wanajilazimisha tu kujihusisha na CHAN ila wako serious sana na siasa. Inawezekana vipi timu ya Taifa inacheza alafu uwanja ni mtupu? Katika mechi zote tatu za Stars hakuna mechi hata moja tumejaza uwanja. Tutatia aibu sana mashindano ya 2027. Kuna wakati naona bora mashindano ya 2027 yahamishwe tu. Ladha ya soka ni mashabiki, sasa watu wamefanyiwa 2000 kiingilio na hawaendi uwanjani, seriously? Picha hapo chini ni mechi ya Stars ya Jana vs Madagascar
1754803155166.jpg
1754803147446.jpg
 
Mimi nasubiria tu siku ya Mwananchi! 💛💚 Tena nitanunua jezi kwa gharama yoyote ile! Na pia nitalipia kiingilio! Nitasafiri kutoka Mkoani! Nitakuja mjini na kufikia kwenye lodge na wife wangu! Yaani ni full kuunguza pesa!Tutakula! Na tutashangilia pamoja na Wananchi wenzangu!

Hiyo timu ya Taifa Stars ni mali ya CCM, Karia na Samia. Hata watu wasipo jitokeza kwa wingi, ni sawa tu. Na kwa hao wanaojitokeza, ni vizuri mkawapongeza.
 
Uko sahihi👍👍
Mimi pia ni mwananchi, ila kuna jambo huwa linanikera sana....RANGI ya timu.
Sijui ni kwanini Chama Cha Mambuzi kimeshindwa kubuni rangi yao mpaka kiamue kuiba!?
 
Nimejaribu kufuatilia mwenendo wa mashindano haya ya CHAN hasa ushiriki wa mashabiki uwanjani, ukweli ni kuwa Tanzania bado sana. Sio tu mashabiki, hata viongozi wenyewe ni kama vile wanajilazimisha tu kujihusisha na CHAN ila wako serious sana na siasa. Inawezekana vipi timu ya Taifa inacheza alafu uwanja ni mtupu? Katika mechi zote tatu za Stars hakuna mechi hata moja tumejaza uwanja. Tutatia aibu sana mashindano ya 2027. Kuna wakati naona bora mashindano ya 2027 yahamishwe tu. Ladha ya soka ni mashabiki, sasa watu wamefanyiwa 2000 kiingilio na hawaendi uwanjani, seriously? Picha hapo chini ni mechi ya Stars ya Jana vs MadagascarView attachment 3437199View attachment 3437200
Ni vile tu yamekuja wakati ambao siasa zimechachamaa
 
Mimi nasubiria tu siku ya Mwananchi! 💛💚 Tena nitanunua jezi kwa gharama yoyote ile! Na pia nitalipia kiingilio! Nitasafiri kutoka Mkoani! Nitakuja mjini na kufikia kwenye lodge na wife wangu! Yaani ni full kuunguza pesa!Tutakula! Na tutashangilia pamoja na Wananchi wenzangu!

Hiyo timu ya Taifa Stars ni mali ya CCM, Karia na Samia. Hata watu wasipo jitokeza kwa wingi, ni sawa tu. Na kwa hao wanaojitokeza, ni vizuri mkawapongeza.
Watanzania wengi wanapenda Yanga na Simba tu
 
Watanzania Hawana Furaha mitaani
Timu ya Taifa Ni Tia maji Tia maji
Haina Uhakika.
Siasa Kuingizwa kwenye Michezo
Wengi wanakerwa sana Ni Basi tu
Nchi Ipo ipo Kila mmoja Anaona kama Anapoteza Muda wake.
 
Mimi nasubiria tu siku ya Mwananchi! 💛💚 Tena nitanunua jezi kwa gharama yoyote ile! Na pia nitalipia kiingilio! Nitasafiri kutoka Mkoani! Nitakuja mjini na kufikia kwenye lodge na wife wangu! Yaani ni full kuunguza pesa!Tutakula! Na tutashangilia pamoja na Wananchi wenzangu!

Hiyo timu ya Taifa Stars ni mali ya CCM, Karia na Samia. Hata watu wasipo jitokeza kwa wingi, ni sawa tu. Na kwa hao wanaojitokeza, ni vizuri mkawapongeza.

Hakuna mwanayanga anaweza andika ujinga kama huu. Yanga ndo imeleta uhuru kupitia ccm. Huwezi kuwa mwanayanga usiwe ccm. Yanga ni team ya chama na ndo maana hata rangi zinafanana. Kama huelewi dogo.
 
Nimejaribu kufuatilia mwenendo wa mashindano haya ya CHAN hasa ushiriki wa mashabiki uwanjani, ukweli ni kuwa Tanzania bado sana. Sio tu mashabiki, hata viongozi wenyewe ni kama vile wanajilazimisha tu kujihusisha na CHAN ila wako serious sana na siasa. Inawezekana vipi timu ya Taifa inacheza alafu uwanja ni mtupu? Katika mechi zote tatu za Stars hakuna mechi hata moja tumejaza uwanja. Tutatia aibu sana mashindano ya 2027. Kuna wakati naona bora mashindano ya 2027 yahamishwe tu. Ladha ya soka ni mashabiki, sasa watu wamefanyiwa 2000 kiingilio na hawaendi uwanjani, seriously? Picha hapo chini ni mechi ya Stars ya Jana vs MadagascarView attachment 3437199View attachment 3437200
Tuanze na wewe. Je umeenda uwanjani. Usitake watu waende wakati wewe huendi na unashusha lawama. Kushiriki michezo iwe jukumu letu sisi sote. Lakini pia TFF waongeze ubunifu kuvutia watu waende. Serikali uone umuhimu wa kuweka huru siku ambazo taifa stars inacheza watu wafike uwanjani
 
CCM wako kwenye state of denial. Hawataki kukubaliana na ukweli kuwa nyakati zimebadilika na wao wabadilike. Badala ya kuangalia wao walipokosea na mchango wao katika hali hii, wameona bora wawatishie wananchi kuwa mashindano haya yahamishiwe Kenya kisa hawaonyeshi kuyaunga mkono.

Niliwahi kusema na kuahidi ufunguzi wa AFCON au fainali utafanyika Arusha kisa jina la uwanja. Naona tumeanza kuandaliwa kisaikolojia. Niliwaambia machawa wameshaanza kuandaliwa kupush hiyo agenda na naona mnajionea wenyewe sasa jinsi wanavyoanza kujitokeza mmoja mmoja. Watakuja kusema uwanja ni mkubwa sana hautajaa, ni bora utumike wa Arusha kwa sababu ni mdogo na mpya.
 
Ukweli ni kuwa CHAN hayajawahi kuwa mashindano makubwa kihivyo. Ni sisi tu kwa sababu ya mzuka wa kutowahi kuandaa mashindano yoyote makubwa na pia uchu wa baadhi ya watu wanaotaka kuyatumia kisiasa. Ila ni mashindano madogo sana. Hauwezi kuyalinganisha na AFCON.
 
Mambo makubwa huanza na mambo madogo..dharau na dhihaka hufanya mambo mengi madogo ya msingi yatupite..si CHAN tu hata AFCON itakuwa kama ilivyo hakuna jipya.

Michezo ni hamasa na starehe si udogo wa michezo.

Tumeshajikatia tamaa na mambo mengi sana ya hovyo yanachanganywa ndani ya furaha na starehe hata iwe ndogo.
 
Pamoja na hoja nyingi pia kumbukeni Tanzania ni nchi masikini na watu wake kwa ujumla ni masikini sana.

Wachache sana wanaweza kufuliliza kuingia uwanjani toka siku ya ufunguzi hadi fainali. Wengi wetu ni hand-to-mouth.
 
Tumeshajikatia tamaa na mambo mengi sana ya hovyo yanachanganywa ndani ya furaha na starehe hata iwe ndogo.
Kenya wametoka kifungoni si muda mrefu, lazima watakuwa na mzuka tofauti na sisi ambao mashindano ya kimataifa yamekuwa mengi na yanafanyika kila siku nchini.

Pia uchumi wetu ni mdogo, hatutaki kukubali na tupo out of touch kwa kutofahamu hilo. Hiyo 2,000/= mnayoona ni ndogo sana ni kubwa kwa waendaji viwanjani ukijumuisha na nauli.

Lakini kubwa zaidi ambalo hatutaki kukubali ni hali ya kisiasa nchini na michezo kuingizwa kinyemela au waziwazi katika siasa. Kwa kuwa watu hawana jinsi ya kuonyesha kupinga hayo wanaamua kususa.
 
Back
Top Bottom