Ndugu wanajamvi, habarini za majukumu. Kutokana na wimbi la uhaba wa ajira na hasa ajira za Serikali, baadhi ya vijana wameonekana kukata tamaa juu ya ajira hizi za serikali.
Wengi huwa tunaomba kazi za serikali pale zinapotangazwa na hatujawahi kubahatika kuajiriwa.
Najaribu kufikiria kutuma MAOMBI ya kazi serikalini hata bila kazi kutangazwa.
Mwenye uzoefu wa kupata kazi kwa njia hii tafadhari tujuzane
Hilo nafahamu mkuu, ila kuna baadhi ya taasisi ambazo sijawahi kuona matangazo ya kazi zao utumishi. Ndiyo maana najiuliza kuwa kazi kwenye hzo taasisi zinapatikana kwa namna gani?
Kwa kuongezea kwa mwenye uzi:-
Jobless anaweza tuma maombi ya kufanya kazi kwa kujitolea katika Wizara ambayo inasimamia taaluma aloisomea? Kama ni Yes, utaratibu unakuaje?
Hilo nafahamu mkuu, ila kuna baadhi ya taasisi ambazo sijawahi kuona matangazo ya kazi zao utumishi. Ndiyo maana najiuliza kuwa kazi kwenye hzo taasisi zinapatikana kwa namna gani?