mkaruka ataja rinu
JF-Expert Member
- Aug 27, 2016
- 3,309
- 2,218
Nilitegemea Serikali kutoa tamko la maana kumbe wakatoa tamko la kitoto kabisa. Serikali iache kuzikandamiza Hospitali kwa kigezo cha huduma, wanatakiwa kutafuta ufumbuzi wa suala hilo maana NHIF imepigwa na wao wenyewe halafu leo wanataka kubebesha mzigo Hospitali.Zipo baadhi ya hospitali binafsi ambazo ziliwahi kubebwa sana na Serikali na hatimaye zikapata faida kubwa na kujiimarisha.
Zipo baadhi ya hospitali zilianza kama hospitali za kujitolea yaani Charitable hospitals lakini leo zinaingia kwenye mkumbo wa kishabiki.
NHIF amehusika kukuza hospitali nyingi za binafsi kwa reimbursement ya mafedha mengi leo hii zinagomea wateja. Hata kama NHIF ina changamoto zake lakini sio kwa extent ya kugomea wateja wake...yaani wa kina sisi.
Sio kwamba hatuoni mnavyolazimisha na mlivyotengeneza genge la kuwapiga watanzania kwa kuexagerrate price za tiba mfano oxygen.
Hongera waziri tukiwaachia watatuletea ombwe kama ilivyo huko USA yaani mwalimu au hata daktari atashindwa kumudu gharama za matibabu.
AFYA SIO BIASHARA....NI HUDUMA.
KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!!