Rev. Kishoka
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 4,526
- 1,552
- Thread starter
- #141
Rev ; Sio kweli na si haki. Chagua kula Keki au kuiweka, na wala hakuna mrengo wa kati juu ya hili. Tupe msimamo wako tushike yepi uliotamka Awali au Leo?
Jujuman,
Msimamo wangu utakusaidiaje wewe kutumia haki yako ya kumchagua yule unayemdhani ni bora?
Je Mchungaji kusema Lowassa atatufaa, basi nawe bila kujipima na kufikiria unaunga tela na kuafikiana nami? Je kufanya kwako hilo la kuunga tela si ndilo tunalolipigia kelele kuwa wale 80% walitekwa kwa tabasamu na kuunga tela?
NImesema, na narudia tena bila kujing'ata ulimi kuwa nilichokisema awali kuhusu Lowassa kitabakia kama nilivyokitamka na nilichokisema leo nacho nakisimamia vile vile.
Sasa sababu zangu za kumnadi Lowassa, nimezitaja. Uamuzi ni wako kukubaliana nami au kutokubaliana nami.