In Edward Lowassa, I trust...

Ni Rev huyu wa kila leo au wamekwiba password.Lowassa who??...
 
Rev.Kishoka,

..Lowassa amekuta kila kitu kimetayarishwa kuanzia sera, mpaka fedha za mradi wa elimu.

..waliokaa chini na kutengeneza sera hizo, na zaidi kuweka mipango madhubuti ya kupatikana kwa fedha kwa ajili ya mradi wa elimu, hawapati credit yoyote ile.

..Tanzania kuna Mawaziri Wakuu ambao wametutoa ktk matatizo makubwa, na wamefanya kazi ktk mazingira magumu, kuliko Ngoyai Lowassa.

..tatizo lingine tulilonalo ni kwamba Lowassa amekuwa akinunua waandishi wa habari tangu mwaka 1993/94. kama angekuwa ni mchapakazi wa kweli, and his record speaks for itself, kwanini anunue waandishi wa habari?

..huyu ni mtu hatari sana ambaye uchu wake wa madaraka, na ujasiri wa kuyatafuta madaraka hata kwa mbinu chafu-chafu, unaweza kutufikisha Watanzania mahali pabaya sana.

..hebu fikiria zile kampeni Lowassa na JK za kumuandama Sumaye kwa karibu miaka 9, je Sumaye naye angeamua kutumia mbinu hizohizo kupambana nao nchi hii ingekuwa wapi leo hii?

..Mchungaji unapopendekeza Lowassa arudi madarakani lazima ufikirie gharama zake kwa taifa hili. kwanza kuna gharama ambazo tutapaswa kuingia wakati wa uchaguzi. hapa nakukumbusha kashfa kama za EPA etc. baada ya hapo kuna gharama za uongozi wake ambazo ni kashfa kama za Richmond,Dowans,Buzwagi etc etc.
 
Kaka Rev......Hapana ndugu yangu msimpigie Debe Bwana Ngoyai,Ninaogopa zaidi ninapoona kati ya watanzania karibu 40 millioni hakuna mtu zaidi ya Lowassa.Muungwana Edward keshakaa hapo na tumeona mambo yake.kaondoka kwa kashfa tumjaribu Mwingine...Lowassa Hapana!.Mheshimiwa Mchungaji katika ziara yako ya Tanzania isije ikawa umepitia Monduli?...Maana ni hapa hapa tuliambiwa kuwa Lowassa atasafishwa....Huu utetezi wako kwa Lowassa umenishtua!

Katika watu ambao ninawapendekeza ni:
1. Prof. Mark Mwandosya.
2.Pombe Magufuri.
3.Mohammed Babu.
Pamoja na mambo mengine nimezingatia zaidi utendaji wao kazi....Huo ni mtazamo wangu tu!
 
Kila kitu kina gharama yake, hakiji kirahisi au burebure. Mmemtaja Magufuli, je naye ni muadilifu? Mbona kajijengea majumba mengi na kujitwalia ardhi anavyotaka?

Mnasema Mwandosya, huyu hana shida kwenye uadilifu, lakini hata kujitutumua kuonyesha makali ya uongozi wake ni shida kujua anaelekea wapi!

Sijasema Lowassa ni safi na ndio maana nimesema Watanzania wote tu mafisadi. Nimemzungumzia Lowassa na uchapakazi wake.

Wengine mnadai kanunua magazeti, ni Mwanasiasa gani wa Tanzania ambaye hajanunua wafuasi au waandishi wa habari?

Tatizo tunatafuta Mtakatifu katika mfumo Shetani, na mnatarajia kutazuka Masiha, lakini ili kuanza kubadilisha mfumo shetani, shurti tumpate Shetani mwendawazimu, atuzindue ndani ya mfumowetu huu huu wa kishetani tuliouzoea.

Kama yeye Lowassa ana nguvu za ushawishi mkubwa ndani ya Chama na hata watendaji wa Serikali, hamuoni basi ni rahisi kwa kazi kufanyika?

Hatuwezi kuzuia Ufisadi au Uhujumu bila kubadilisha mfumo mzima na hilo halitatokea usiku wa maanane mmoja au kutarajia tukimteua "mtakatifu" basi nalo Taifa litabadilika.

Katika nafsi zetu za kifisadi na mazingira yetu y kifisadi, tunahitaji atakaye tuchapa bakora kama nyapara au mkoloni ili tuanze kuwajibika na kufanya kazi ndani ya mfumo huu huu wa kifisadi.

Mnaoana leo hata kuhoji kwa nini tunakaa gizani Kikwete anashindwa kutatua tatizo la umeme, mpaka Wafanyabiashara waende kumuomba alisawazishe.

Afadhali na Lowassa alibuni mradi wa mvua alipojua kuna ukme unakuja, meaning he was pro-active.

Lowassa has a political will even though his intentions may be flawed or not at all pleasant to us.

So think about it again, it is only the one who knows the system well and has already been effective who will be useful to jumpstart the Safari ya kusukuma gurudumu la maendeleo.

Isitoshe, Lowassa is looking to redeem himself and prove that he is competent!
 
OOOOOOPSSSSSSSSS let me take a braek,honestly kikwete hanivutii kwa utendaji wake,na msaidizi wake pinda analalama kwenye mikutano ya wazi kama raia asiyekuwa na power,eti haya magari ni gharama sana huku wakiagiza mengine mapya,hiyo ni myopia ya viongozi wetu
 
Yes, I have said it. Ili tuendelee, tunamhitaji Edward Ngoyayi Lowassa!

Ni mchapakazi, mfuatiliaji na mkali asiye na masikhara na walioko chini yake si kuwa wanamheshimu tuu, wanaogopa kushukiwa na zali kutokana na ukali na ufuatiliaji wake.

Kila kazi aliyopewa, kaifanya kwa bidii na kwa ufanisi. Kuna tofauti kubwa sana za kiutendaji kati yake na wenzake walioshika nafasi za uongozi ambazo alizishikilia.

Naamini kwa dhati kuwa ili Tanzania iweze kuamka na kurudi katika mstari ulionyooka wa kujituma, kufanya kazi kwa bidii na maarifa bora na la zaidi kwa nidhamu ili tuendelee vyema na safari yetu ya kujijenga kiuchumi na kijamii ili kuleta maendeleo ya kweli, basi hakuna mwingine zaidi ya Lowassa!

Kama unaye wa kwako, tupe jina na umnadi, wangu miye ni Lowassa!

Rafiki,
Hiyo timu ya mafisadi a.k.a. wafilisi nchi na wewe imekununua? Lol! Pole sana. Kwa mtaji huu hatutafika mbali maana Wa-tanzania tutazidi kusalitiana sisi kwa sisi, kisa mmoja wetu ananufaika na mafisadi na anakuja kuuza sera zao hapa. May GOD forbid.
 
Kaka Rev......Hapana ndugu yangu msimpigie Debe Bwana Ngoyai,Ninaogopa zaidi ninapoona kati ya watanzania karibu 40 millioni hakuna mtu zaidi ya Lowassa.Muungwana Edward keshakaa hapo na tumeona mambo yake.kaondoka kwa kashfa tumjaribu Mwingine...Lowassa Hapana!.Mheshimiwa Mchungaji katika ziara yako ya Tanzania isije ikawa umepitia Monduli?...Maana ni hapa hapa tuliambiwa kuwa Lowassa atasafishwa....Huu utetezi wako kwa Lowassa umenishtua!

Katika watu ambao ninawapendekeza ni:
1. Prof. Mark Mwandosya.
2.Pombe Magufuri.
3.Mohammed Babu.
Pamoja na mambo mengine nimezingatia zaidi utendaji wao kazi....Huo ni mtazamo wangu tu!
Kwa kuwa hao wawili wa mwanzo wamekaa saana kwenye hii system yetu mbovu mbovu na wana harufu ya ufisadi wa TTCL na Nyumba za Serikali, basi nitaenda kwa Babu lakini naomba utupe hizo sifa zake za utendaji aka uadilifu
 
Ni kweli alikuwa busy na serious sana katika kuleta maendeleo ya tumbo na mifuko yake. Tatizo ni pale anapotaka kuchukua kila kitu kutoka kwa wananchi!!
 
Labda niseme hivi nieleweke.

Tatizo la Tanzania si Ufisadi, bali ni sisi watu wenyewe, tu wavivu, magoigoi na tumeridhika mno na mambo ya ajabu ajabu ambayo Serikali imelala kabisa.

Sasa jiulize kama Dar Es Salaam juzi walidiriki kukaa masaa karibu 14 bila umeme na Serikali nzima na Wananchi wanaona ni jambo la kawaida, hamuoni kuwa tunahitaji mtu fyatu ambaye akihoji ni nini kilichotokea, basi watu wataanza kubadilika?

For now Lowassa stands to be the only ideal choice we have, maana nilichokiona Tanzania hatuhitaji tena eti mtaalamu kama Ndulu au Shivji.

NIlijiuliza kwa nini Watanzania hawana mwamko wa kufanya kazi au kujitutumua? nikajiuliza kwa nini Watanzania wameridhika na shida na dhiki? Naendelea kujiuliza kwa nini Watanzania wanaendelea kunyanyaswa na Serikali na Majuha wachache wanaotaka kujifanyia mambo wanavyotaka (shida ya umeme, maji, takataka na foleni za magari)? Nikajiuliza kwa nini Watanzania hawafuati sheria au kanuni ilhali sheria na kanuni zipo na nyingi? nikajiuliza kwa nini watunga Sheria na enforcers wa sheria si makini katika kuhakikisha Sheria na kanuni zinafuatwa?

Sasa kwa kipmo hicho na wala si mambo ya Uhujumu au Ufisadi, utagundua kuwa Tatizo la Tanzania ni mfumo mbovu wa uongozi na jamii ambao unahitaji mtu fyatu na mkali ili tunyooke.

Give Lowassa 10 years and trust me we will see a big difference na ndipo sasa tuanze kutafuta watu softisofti kama Membe au sijui ni majina gani!

Mnaodai kuwa tutaendelea kuliwa, ni lini tuliacha kuliwa? Tangu enzi za Nyerere tunahujumiwa na hatujabadilika mpaka leo hii.

Si siri kila Mtanzania ni fisadi kwa namna yake moja au nyingine. Leo watu wanatoa rushwa kama ni haki yao kutoa rushwa na ni jambo la kawaida ili wapate leseni au kibali cha gari.

Watu hawafuati taratibu na sheria wti hawataki bugudha, hivyo kiulani wanatoa kitu kidogo bila hata kuombwa au kulazimishwa!

Let Lowassa take the reigns and you will se the change that we can all believe in!

Amen to that mkubwa.
Tutake tusitake, sisi domo jingi na kama Rev. alivyosema mtu mwenye uwezo wa kusema na kusikilizwa ni EL ingawa ana mapungufu yake kwenye barbara ya km 10 atajenga 9 aibe 1. tofauti na hao magaigoi ambao wanaiba kila kitu na wanaibiwa pia.
 
Competings in doing sins...kama imefikia hatua ya kukata tamaa mpaka unam-support "fisadi" ambaye amepewa kila kitu i.e cheo (PM), marupurupu, usafiri bure, housing bure, etc etc..bado anajiingiza kwenye deals mbaya mbaya ni aibu kubwa kwa mtu kudiriki kum-support..hiyo ni sawa na wale wanaoshindana kufanya madhambi..lol
EL alitakiwa awe anafanya mahudhurio kisutu..toka siku alipostaafu mpaka...kieleweke..
 
Rev, sasa naona tunakosa dira na muelekeo.Not meaning to dis, lakini by any chance Eddo ame ku enlist ulipokwenda last time?

I am aware of the few pickings we have, especially at the national level.I am aware that Eddo can be an efficient bureaucrat, if that is not an oxymoron.

But Eddo is too arrogant and too much of a glutton, Eddo alikuwa hasubiri wahindi waje ofisini kwake, alikuwa anawafuata mwenyewe Upanga.

As much as I have reservations against Nyerere, alipowaua Kikwete na Lowassa kwamba hawafai mimi niliona sawa kabisa.

taja mwingine, lakini si Lowassa.
 
Hivi mmeshawahi kujiuliza ni vipi Watanzania wanakuwa expoited au ni jinsi gani Ukoloni ulifanikiwa?
 
Rev. Kishoka,
I can see your frustrations, nchi yetu imebarikiwa na kila kitu lakini inaongozwa na vilaza.

Ukweli ni kuwa Lowassa licha ya kupenda rushwa, asingeacha nchi ikaingia gizani. Lakini je ni kweli kuwa ni Lowassa tu anayejua kazi? Sidhani kama hii ni kweli. Ukweli ni kuwa EL alikuwa ana ubavu juu ya JK, kwani alishiriki kumuweka madarakani, kitu ambacho Pinda hana. Pinda anaonekana kama vile ni outsider na too loyal to be vocal.

Tatizo hapa ni kuwa na raisi wetu hajui kazi na kibaya zaidi akachagua mawaziri wasiojua kazi vilevile.

Solution hapa sio kumrudisha Lowassa, bali ni kumfukuza kazi Kikwete.
 
Amen to that mkubwa.
Tutake tusitake, sisi domo jingi na kama Rev. alivyosema mtu mwenye uwezo wa kusema na kusikilizwa ni EL ingawa ana mapungufu yake kwenye barbara ya km 10 atajenga 9 aibe 1. tofauti na hao magaigoi ambao wanaiba kila kitu na wanaibiwa pia.
Hapana. Kwenye barabara ya km 10 atajenga 3 na nyingine kujenga mahekalu yake.
 
"He stinks, a deep foul smell of corruption, greed and power mongering. He has proven time and time again that he is not attentive to details, he is not efficient nor wise. His descisions have costed our nation Millions of money through a dirty contruct and a slup in our economy as a result of forcing a bogus contract between Tanesco and Richmond." Rev Kishoka.

Is this the right guy to lead us really in the 21 century?
 
Back
Top Bottom